David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Hapa sio 10% Bali zaidi ya hapo na ni kwa hiyo miaka 30 na uwezekano wa kuendelea. "Wahuni" hawana nia njema na hili taifa bali wana nia njema na mafisudi.
 
Acha uongo na uzushi wako
Sasa dhumuni la kufanya hivyo ni nini ?? Ikiwa aliyewekeza atapata faida, lakini Sisi hatuitaki hiyo faida, matokeo yake ndio hayo ya kuitwa "wahuni" au hamjui mko hapo kufanya nini
 
Hilo ulilosema Mwisho ndio linatakiwa la kampuni ya wazawa na hisa ziwe DSE
 
Wizi mwingine unaenda kutengenezwa in the name of ubia. Hatuna rangi tutaacha kuona
 
Kanji akiwekq kibunda chake $900 million unadhani anategemea kupata hasara!? Hapo mnaelewa kuwa huyu faida yake ni kiasi gani na kwa muda gani!?? Gautam Adani atawanyoosha!
 
Nchi hii tuna wajinga wengi sana! Sasa Lucas Mwashambwa the headless chicken anashabikia nini hiki?
 
REA wameweza kusambaza Umeme nchi nzima vijijini kwa pesa za Tanzania wapewe kazi ya kujenga miundombinu kusambaza hatutaki matapeli kupitia PPP

Kazi kubwa iko kwenye kuzalisha umeme Tanesco imeweza

Sasa huku kwenye duka la rejareja la kusambaza umeme tu kama kusambaza tu gesi ya kupikia na majiko yake ndio tushindwe locally?
Mbona REA wameweza kusambaza Umeme vijijini kuliko kugumu kama nini

Haya mambo ya kuleta PPP kwenye miradi kama ya usambazaji umeme ambayo REA wameonyesha uwezo mkubwa kusambaza hadi sehemu zisizofikika kwa usafiri wowote nchi nzima tena kwa pesa za Tanzania kuanzia nguzo, nyaya transformer nk

Huyo anayetaka kuleta kampuni ya kigeni ilipwe dola ambazo kwa sasa dola hatuna ukienda benki shida nani huyo hasa ?

Kampuni nyingi mfano za China zinazojenga miradi mikubwa Tanzania ni za serikali ya China zikiwemo zinazojenga reli ya SGR zina ufanisi

Sasa REA wameonyesha uwezo mkubwa wa wazi huyo msambazaji wa kutaka PPP anataka kusambaza kupeleka wapi? Mijini Tanesco wamekumudu vizuri tu ,vijijini wasambaza umeme REA wamemudu huyo wa PPP anataka kusambaza umeme kupeleka wapi ambako Tanesco na REA hawajaweza?
 
Bado haya maneno yanatakiwa kutoka tanesco na bodi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…