David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Serikali ya CHURA akuna inacho weza zaidi ya udalali TU.
Kenya wanawakataa nyie mnawakumbatia.
Takataka kabisaa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.

"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.

Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.

Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).

Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.

"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.

Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.

Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.View attachment 3116153
Adinani na DP weldi Zote ni wizi, kama nchi kwanini tusiuze hisa au au kama shida ni Sisi wa Bongo na akili zetu za Kibongo , tusiweke Management ya wataalamu kutuendeshea hayo mashirika , baada la kuwapa watu wa nje hiyo Bandari au Umeme au Mwendokasi .maana biashara hizi hazina shida, Sana sana , tatizo ni Uwekezaji na uongozi Bora ambavyo vyote tunaweza kuvipata. Kinyume cha hapo kinacho fanyika ni ufisadi
 
Adinani na DP weldi Zote ni wizi, kama nchi kwanini tusiuze shares au au kama shida ni Sisi wa Bongo na akili zetu za Kibongo , tusiweke Management ya wataalamu kutuendeshea hayo mashirika , baada la kuwapa watu WA nje mgodi iwe Bandari au Umeme au Mwendokasi maana solo lipo , tatizo ni Uwekezaji na uongozi
Kwanza unaelewa maana ya Ubia?
 
Hapa kafulila umechemka ,yaani kusafirisha tu serikali kupitia REA hawawezi? Wizzy Wiizy.

Kama DERM ameweza kutengeneza nguzo na kuna kampuni hapa hapa nchini zinatengeneza transforma na nyaya ,kwanini tusiwape hao na serikali iwe inawalipa kidogo kidogo kuliko kwenda kumpa muhindi aliyefukuzwa kenya kuja kutupiga kama HABINDA SINGI?
Napata shida kukosoa au kukubali huu mradi sababu sijui wamekuja na na hoja gani kutofautisha na walipo kwama serikali kwenye usafirishaji umeme.
Huenda wana jipya au hawana jipya ni miradi ya watu waliomo serikalini. i.e 10% au Wana hisa humo.
Kuweka wazi mapema habari hii kunasaidia watu wanao ijua hiyo kampuni kuweka matatizo yao bayana.
 
Kwanza unaelewa maana ya Ubia?
Kwanza unaijua historia ya ubia maana usikimbilie Tu neno ubia. Na historia ya mashirika ya umma na madhumuni yake na nini sababu ya kuwepo DSE na soko la mitaji. Na la Mwisho mahusiano ya jamii. Au ndio tunataka kurudi kwenye matabaka, walio nacho na wasio nacho, rangi na mengineyo. Nini Sera ya Nchi kuhusiana na mahusiano usifikiri yanatokea Tu kama uyoga, Bali Kwa kupitia Sera na uongozi Bora sio Bora uongozi
 
Moderator ni Kafulila au Kafulila?
Bora umewaambia maana nashangaa kwanini hawarekebishi tangia jana.na wao ndio walioandika hivyo wakati wanabadilisha kichwa cha andiko langu .maana kichwa cha awali niliandika David Kafulila Apiga Simu Kutokea Nchini India kutoa ufafanuzi wa kina juu ya uwekezaji wa Adan katika Miundombinu Ya Umeme kwa Mfumo wa Ubia.
 
Moderator ni Kafulila au Kafulila?
Bora umewaambia maana nashangaa kwanini hawarekebishi tangia jana wao ndio walioandika hivyo wakati wanabadilisha kichwa cha andiko langu .maana kichwa cha awali niliandika David Kafulila Apiga Simu Kutokea Nchini India kutoa ufafanuzi wa kina juu ya uwekezaji wa Adan katika Miundombinu Ya Umeme kwa Mfumo wa Ubia.
 
Tuanzie hapa
Sie tumefeli wapi hadi tutake ubia. Maana uzalishaji tumefanikiwa , je usambazaji tunahitaji a comple overhaul ya haraka had tuhitaji usd 900 mio. Je hatuwezi kendal kwa phases na huku tukiendelea kutoa huduma public goos. Hawa jamaa wanaweza kuingia kwenye procurement kama wauzaji tu sio waendeshaji. Imagine nguzo , chuma liganga na cement za nguzo mufindi na transformer kigamboni
Vifaa baba vifaa, mafundi wapo.ila
Vifaaa.
Jinsi ya kuvifunga
Jinsi ya kuvipata
Mifumo ya uendeshaji ,bila kuwa na PPP hupewi teknolijia ,maana huko pakuvipata wanakwambia ,wasambazaji wao ni asani na hao gridworks ( mfano) ,

Ukisema ukafunge mwenyewe ndio hivyo ujuzi bado .
 
Kwa TZ wala hawakopi,vyote vimeandaliwa twaeni mle. Ukiona mwekezaji kachukua mkopo bank ni kutakatisha hayo mapato bila jasho. Niliwahi kuwa na mazungumzo na dingi mmoja mfanya biashara ana ukwasi wa kutisha kwa sasa. Kipindi cha PSRC alikwapua deal moja tu. Alisema hata cabinet paper aliambiwa aandike yeye.Kuhusu package ya facilitators inatisha.
 
Hawa Adani inatakiwa waje baada ya uchaguzi tukiwa tumepata rais mwenye akili na siyo mwendawazimu
 
Back
Top Bottom