David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia


Kuna hatari ya kumpa mwekezaji mmoja karibu njia zote kuu za uchumi. Na kunaleta ukakasi pia.
Tukumbuke, kuna leo na kesho. Tanzania inahitaji wawekezaji, ila tusifanye mambo ili mradi tumefanya.
 
Lile karatasi la kununulia luku itakuwa kama mkeka wa betting, kwa hizo tozo
 
Kuna hatari ya kumpa mwekezaji mmoja karibu njia zote kuu za uchumi. Na kunaleta ukakasi pia.
Tukumbuke, kuna leo na kesho. Tanzania inahitaji wawekezaji, ila tusifanye mambo ili mradi tumefanya.
Kifupi anakuja kuwekeza nini..imagine tulipofikia halafu jamaa anakuja kufanya kazi REA. Je tozo zitaondoka?. Kifupi umeme ni public goods hivyo kumpa mfanyabiashara hakuna umeme utafika myipwindi unless tuwe tunamega kwenye kodi na kumpa.
 
Dalali yuko kazini, Tanesco haijashindwa kujenga miundombinu hiyo
Mama Samia wewe Raisi lakini ushike adabu yako tukikwambia usiendekeze wahamiaji haramu akina Kafulila na akina Mwashambwa uwe na adabu wanaokusifia kila kitu unafanya bila kukukosoa usituone sisi wana CCM tunaokukosoa kama mabwege

Husikikilizi tutaacha utajijua mwenyewe hatuna mpango wa kutafuta teuzi kwako
 
Wahindi wametumia ujinga wa watanzania katika kinachoitwa uwekezaji kutupiga.
Siyo mara ya kwanza kutupiga kwenye kutumia miundombinu ya uma (kumbuka TRC).
Hata hapa kutakuwa na maandishi mengi ya mikataba na mwisho wanatumia miundombinu hiyo hiyo iliyopo, baada ya muda mikataba inafutwa.
PPP kwa wageni itumike kwenye miradi mipya kabisa kama migodi na viwanda vya kufua vyuma, umeme wa makaa ya mawe na upepo.
Hii ya usambazaji umeme waachiwe wananchi wazawa. Tusiwape mbwa chakula cha watoto.
 
Tuwe macho Bwana Kafulila. Tumeshapigwa sana kupitia wawekezaji. Tuna uchungu tukikumbuka tiscs. Watanzania wenzetu walitupiga miaka 30 wakijidai ni wawekezaji toka hong kong na wala hawakuwekeza kitu. Huyo Adani ndio tajiri mkubwa india kwa kurukia uwekezaji zilizokua tayari na kuwapiga nchi zenye wajinga kama tanzania. Tunaweza kuendesha mambo yetu kama hatuna serikali legelege kama hii ya saamia inayoturudisha nyuma kuamini kila kitu turuhusu watu wa nje ambao wala hawawekezi ila kuja kuvuna uwekezaji za umma. Mambo mengi ni usimamizi tu kama ule wa awamu ya tano ndio kitu kinahitaji kwa sababu hela tunazo. Magufili aliposema sisi ni tajiri haikua uongo.
 

Hawa watu watatuingiza Chaka na Ubia wao.
 
Kifupi anakuja kuwekeza nini..imagine tulipofikia halafu jamaa anakuja kufanya kazi REA. Je tozo zitaondoka?. Kifupi umeme ni public goods hivyo kumpa mfanyabiashara hakuna umeme utafika myipwindi unless tuwe tunamega kwenye kodi na kumpa.

Na mimi najiuliza pia. Maana sijui exactly nini wanachokifanya kina Kafulila na team yake kwenye huo uwekezaji.
 
Mkuu Adani ni damu chafu,corrupt.
Kafulila acha huyo mhindi atatumeza tukiwa wazima.
Hivi PTA berth no 8,9,10,11 zilichukuliwa na huyo mtu?
 
Baada ya Magufuli kuwekeza 7 trilioni kwenye bwawa la umeme, sasa uhakika wa umeme upo, ndo mnatafuta wawekezaji uchwara ili wapige pesa, Kila siku Bunge linashauri Tanesco igawanywe Mzalishashaji na msambazaji mnakataa, kumbe mmelenga kutafuta makampuni ambayo mtayapa Letter of credit yakope pesa kwa udhamini wenu then waziingize kufanya kazi ambayo inaweza kufanywa na watanzania. Yale yale ya Richmond na Dowans. Upigaji.
Walisubiri nini tujenge bwawa kwa matrilioni?
 
Hii ni Kampeni ya kuzidi kumuumiza mtanzania na kuendelea kujipinga wao wenyewe na serikali Yao.
Wakati mama Yao kina Mwashambwa anapiga kelele kuhusu matumizi ya Nishati safi Kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na afya za watu wa bara la Africa, Kafulila anakuja kupunguza watumiaji wa umeme ambao ni nishati safi.

Ndio anapunguza kwa kujenga mazingira umeme uonekane ni anasa kwa sababu ukiacha mapendekezo ya January ya Kuomba 1Tri. Kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu pamoja na kuwapa tenda wahindi. Sasa Kafulila amekuja kutoa mapendekezo kwa mabepari wengine kuhusu suala la usambazaji. Ccm inajinasibu kwamba imesambaza umeme vijijini kwa asilimia kubwa sana kuliko wakati wowote (availability)
Kinachokuja kutokea ni kuongeza gharama za umeme kwa mlaji Ili kifidia hizo gharama za kiuwekezaji anazoweka mwekezaji. Subsequently umeme unakua tena sio huduma kwa wananchi bali anasa. Angalia kutoka 5000 unit 17 mpaka sasa unit 4 . Kutokana na utitiri wa Kodi na tozo. Tanzania is a fallen states where politicians seeks personal benefits and popularity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…