==
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akiwa katika mahojiano na kituo maarufu zaidi cha utangazaji cha ITV kwenye kipindi cha DK 45 amesema haya,
Pamoja na mambo mengine mengi Kafulila anasema kama Kuna kitu Rais Samia anaweza kujivunia ni kufanikiwa kutekeleza Miradi yote iliyoachwa na Mtangulizi wake bila kuacha hata mradi mmoja,
Kafulila anasema awamu ya 5 ndio awamu ilianzisha Miradi mingi na mikubwa pengine kuliko wakati wowote wa uhai wa Taifa la Tanzania na baada ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 haikudhaniwa kuwa Miradi hiyo lukuki na yenye gharama kubwa kama Rais anayefuata angeweza kuitekeleza yote na Kwa BOQ zile zile Kwa sababu ya kukosekana Kwa consistency toka awamu moja na awamu nyingine ya Uongozi.
Hata hivyo Mkurugenzi Kafulila anasema baada ya Kifo cha Rais wa awamu ya tano palihitajika Rais mwenye maguvu, Uwezo , maamuzi na utayari zaidi ili kwanza kukamilisha Miradi yote iliyoanzisha na Mtangulizi wake lakini pili ni kuanzisha Miradi mingine mipya na huyo mwenye hizo sifa na uwezo huo ni Rais Samia Suluhu Hassan Kwani ni yeye kamaliza Miradi yote ya awamu ya 5 na kaanzisha Miradi mingine mipya ya awamu ya 6.
Kafulila anasema amesafiri nchi nyingi za Ulaya lakini hakuna nchi yenye reli bora kama reli ya SGR ya Tanzania toka Dar es salaam mpaka Dodoma reli ambayo unaweka juice au maji juu ya meza na haimwagiki mpaka unafiki Dodoma alisifi juhudi za Rais Samia katika Ujenzi wa reli hiyo.
Msikilize Kafulila kwani kaongea mambo mengi tena Kwa kina.
View attachment 3359513