David Kafulila: Deni la Tanzania ukilinganisha na Mataifa mengine ya bara la Africa ni nafuu

Kila nchi inakopa, ila inategemea na hizo hela unafanyia nini?
Kama mnagawana au mnafanyia maendeleo

Kwa hiyo kujilinganisha na mataifa mengine ni uzwazwa
Ni kama watu tu wanaokopa Bank kila mmoja anatumia anavyoona yeye kwani wengine watahonga magari na wengine watawekeza kwenye biashara
Kwa hiyo inategemea unapeleka wapi mkopo
 
 
Ogopa tapeli mwenye confidence anaweza kukuaminisha uongo hebu atupe mchanganuo huo wa 25% increment ili tujue deni halisi ni lazima atuambie kabla lilikua kiasi gani? Na sasa ni kiasi gani? Na hapa miaka minne tumeshalipa kiasi gani so far ? Na hizo hesabu yeye amepataje hiyo asilimia
 
Tumbili ni janga la Taifa!! muongo, mnafiki, hatakiwi kuaminiwa!!!
 
Ni kweli ila je tujisifu?
 
Wakati tumapambana kuhalalisha deni kubwa la Taifa Burkina, Mali na Niger wanapambana kuwa self sufficient kwa resources zao za ndani..

Sisi tunakwama wapi?
 
Hii nakubaliana nalo
 
Deni la Tanzània ni stahimilivu sana
 
Kukopa sio tatizo, tatizo letu mikopo yetu tunaitumia ndivyo sivyo. Watu wanatafuta namna ya kupiga hizo hela za wafadhili lakini kufanya kilichoombewa ni kidogo Sana haifiki hata asilimia tano. Mikopo kwa ajili ya corona ilitumika ndivyo sivyo, waliofaidi ni wachache. Magari ya wabunge na mawaziri hizo hela tungefanyia kituo Cha maana kuliko kila bajeti kutenga hela za magari ni ufisadi wa kwanza huu. Mikopo tulipe tujenge hospital na shule kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vijavyo
 
Ni sawa
 
 
Bwana( tumbili) anataka kufananisha wenye maendeleo na sisi vituko...........hao aliowataja wamekopa lakini mataifa yao yana eleweka pesa zilipokwenda na kazi zilizofanyia..... huku kwetu Deni kubwa bado mnapambana na matundu ya choo
 
Unafahamu original ya jina tumbili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…