Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPPC), David Kafulila amesema kitendo cha Rais wa Marekani, Donald Trump kuja na sera za kusitisha baadhi ya misaada kwa nchi za Afrika, kimefungua fursa mpya kwa Tanzania na kwamba serikali iko mguu sawa kuzitumia fursa hizo kwa maendeleo endelevu ya uwekezaji nchini.