Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mkurugenzi Mkuu wa PPP Mheshimiwa David Kafulila amewatoa hofu watanzania ambao wameonyesha kuwa na hofu kubwa sana juu ya mikataba ya Ubia .hasa kwa kurejea majeraha na makovu ya mikataba mibovu ambayo yamewahi kushuhudia yakileta hasara kwa Taifa letu.ikiwepo IPTL ambayo ilikuwa ni kama Jini Mnyonya Kodi za Watanzania wanyonge.
Ambapo Mheshimiwa David Kafulila Amesema ya kuwa ni katika mafunzo na uzoefu huo wa kuhakikisha hatuingii mikataba mibovu ya aina hiyo ndio iliyopelekea kupitishwa kwa sheria namba 103 ya PPP.Amesema kuwa PPP inatumika maeneo mbalimbali Duniani ikiwepo China ,India,Amerika na ulaya yote.
Hata hivyo amekiri kuwa Watanzania wapo sahihi kuwa na hofu ,hasa kwa kuzingatia yaliyotokea siku za nyuma kuhusiana na mikataba mibovu iliyoligharimu Taifa letu.
Soma Pia: Kafulila: Kama kuna mtu au kampuni wameona kuna mradi serikali inauendesha kwa hasara na wana mbinu za kuifanya serikali na wao kupata faida waje
Na hofu hiyo inakuja wakati huu ambao kampuni ya Adani imeonyesha nia na dhamira ya kutaka kuwekeza katika miundombinu ya Umeme hasa usafirishaji wa Umeme kwa Mfumo wa Ubia.
Ambapo wengi wametoa maoni yao kuwa Kwanini serikali isiifanye kazi hiyo yenyewe kupitia TANESCO kwa kuiongezea Bajeti. Wengine wakasema kuwa kama tumeweza kufikisha umeme hadi ngazi za vitongoji huko vijijini ,iweje sasa tutafute muwekezaji wa kusafirisha umeme wakati hata sisi wenyewe tunaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.