Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Napowaambia kuwa David Kafulila ni Chuma nakuwa namaanisha ni CHuma kwelikweli na Mzalendo wa dhati Wa Taifa letu,ambaye huwa hayumbi wala kuyumbishwa wala kutetereshwa wala kuogopa wala kupoozwa wala kuangalia ni nani anayepambana naye au aliye mbele yake.
Chuma David Kafulila ni CHuma ambacho husaga uozo wowote ulio mbele yake .Ni mtu aliyenyooka kama rula ambaye huwezi kumpindisha kwa vihela vyako vya rushwa au hongo.
Sasa nisiwashoshe .ipo hivi jamaa alipoingia Mkoani Simiyu alikuta kuna barabara inajengwa na Mkandarasi,ambapo baada ya kuikagua akagundua kuwa ipo chini ya kiwango na haiwezi kudumu kwa muda mrefu ,na hivyo italeta hasara kwa serikali kwa kuanza kuirudia kwa gharama na kodi za watanzania wanyonge.
Baada ya kugundua uozo huo uliofanywa na Mkandarasi ,alitoa amri kali na maagizo mazito kwa mkandarasi kwa kumtaka arudie barabara hiyo ya urefu wa KM 20 inayogharimu takriban Billion 40 kwa gharama zake mwenyewe Mkandarasi na ikamilike kwa ubora unaohitajika na kwa wakati muafaka. Maagizo hayo yalitekelezwa haraka sana na mkandarasi kurudia ujenzi kwa gharama zake na kuwa fundisho kwa wakandarasi wengine.
Hii maana yake nini ndugu zangu? Hii inamaanisha kuwa kama barabara hiyo ingepokelewa katika ubovu wake huohuo, maana yake ingeshuhudiwa mvua kidogo tu ikinyesha barabara inaanza kukatika na kumomonyoka kila sehemu,lakini pia ingeshuhudiwa barabara hiyo ikianza kuwa na mimashimo mashimo kila sehemu na hivyo kusababisha hata ajali za barabarani.
Lakini kubwa na baya ni kuwa serikali yetu ingeingia hasara ya kuanza kutoa pesa zingine mamilioni kwa mamillioni kurudia na kurekebisha barabara hiyo .pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga miradi mingine kama vile shule,vituo vya afya, zahanati,ununuzi wa madawa na vifaa tiba, usambazaji wa maji safi na salama n.k.
Lakini Chuma Kafulila kwa uzalendo wake na unyoofu wake kimaadili na uaminifu wake kwa Taifa letu akaokoa gharama hizo na pesa hizo. Hii ndio maana tunasema hiki chuma ni habari nyingine,ni CHuma cha moto kwelikweli ambacho hakijawahi kuwa na huruma na mafisadi,wezi na wala rushwa.
Hii ndio maana nampongeza na kumuunga sana mkono Mh kafulila.ndio maana natamani kuona akirejea Bungeni hapo Mwakani,ndio maana nina kiu ya kuona akiendelea kuwepo Serikalini kwa kuwa chochote kinachokuwa chini yake na mikononi mwake kinakuwa kipo mahali salama na penye usalama,tofauti na wengine ukiwakabidhi nafasi fulani wanaigeuza kuwa mrija wa kufyonza pesa na kodi za watanzania kama mchwa wenye njaa .
Naweka kalamu yangu chini ili andiko lisiwe refu kupita kiasi hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa watanzania ni watu wavivu sana katika kusoma vitu na ndio maana ukitaka kumuibia mtanzania basi muwekee jambo hilo katika maandishi na mahali pa kusaini.uone namna atakavyo saini haraka haraka bila kujuwa kilicho andikwa.halafu kesho unaona hata yeye anaanza kushangaa na kutoa macho anapo ambiwa kile alichokisaini.
Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.