David Kafulila: Utajiri wa taifa lolote duniani si vitu, ni ubora wa watu wake

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
3,629
Reaction score
3,015
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), Bwana David Kafulila, akiwa katika Tengeru Institute of Community Development (TICD) jijini Arusha, amekaririwa akisema kuwa “Kwa mujibu wa sheria, mradi wa ubia ni mali ya umma kabla, wakati na hata baada ya utekelezaji wake. Lengo kuu ni kuboresha maisha ya watu.”

Katika muktadha huo, Kafulila alikumbusha kuwa mwaka 2014, Taasisi ya REPOA kwa kushirikiana na UNDP ilifanya tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa. Tathmini hiyo ilionyesha kuwa ili kufikia kikamilifu Dira ya Maendeleo ya 2025, sekta ya elimu ilihitaji kupewa kipaumbele cha pekee.

Hata hivyo, alibainisha changamoto kubwa: mishahara ya serikali, kutokana na ukubwa wa serikali yenyewe, inakula sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi. “Njia pekee ya kupunguza mzigo huu,” alisema, “ni kukuza uwekezaji, kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza mapato ya kodi.”

Kafulila alionya kuwa njia mbadala ya kutumia rasilimali zilizopo bila kuongeza uzalishaji ni hatari. “Ni sawa na kula mbegu badala ya kuzipanda. Hii ni tricky sana. Ukila mbegu, unakosa mavuno ya baadaye. Huwezi kuboresha elimu ya watu bila kujenga uzalishaji wa taifa. Ukichagua njia hiyo, unajikuta unagawana umaskini,” alisisitiza.

Aidha, Kafulila aliongeza kuwa tafiti nyingi zinasisitiza serikali kutumia angalau 60% ya mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya watu, na 40% kwa ajili ya maendeleo ya vitu. Alisema uwiano huu ni muhimu ili kuhakikisha ustawi wa wananchi unakwenda sambamba na uwekezaji katika miundombinu na sekta nyingine za uchumi.

Akihitimisha, Kafulila alisema kuwa tunahitaji uwiano sahihi kati ya matumizi ya kodi na kukuza uzalishaji ili kufanikisha maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya wananchi.

Huwezi kuwa na watu waliobora bila kuwa na vitu bora. Huwezi kuwa na watu bora bila kuwa na miundombinu bora, huduma bora za jamii zinazotolewa katika miundombinu bora, makazi bora n.k.
Kwa hiyo vitu bora ni hitaji la mwanzo la kuwa na watu bora. Hakuna maendeleo ya watu bila vitu bora.
 
Umegeuza tu hapo, Hivyo vitu kwani vinajitengeneza?
 
Huwezi kuwa na watu waliobora bila kuwa na vitu bora. Huwezi kuwa na watu bora bila kuwa na miundombinu bora, huduma bora za jamii zinazotolewa katika miundombinu bora, makazi bora n.k.
Kwa hiyo vitu bora ni hitaji la mwanzo la kuwa na watu bora. Hakuna maendeleo ya watu bila vitu bora.
Mbagala ya watu kuingilia dirishani kugombania magari Vs Mbagala ya watu kupanda mwendokasi yenye full air condituon,Unasemaje hapo Kafulila,ubora wa watu kuliko ubora wa vitu?
 
Watu wakiwa bora watakuwa na magari yao
 
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), Bwana David Kafulila, akiwa katika Tengeru Institute of Community Development (TICD) jijini Arusha, amekaririwa akisema kuwa “Kwa mujibu wa sheria, mradi wa ubia ni mali ya umma kabla, wakati na hata baada ya utekelezaji wake. Lengo kuu ni kuboresha maisha ya watu.”

Katika muktadha huo, Kafulila alikumbusha kuwa mwaka 2014, Taasisi ya REPOA kwa kushirikiana na UNDP ilifanya tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa. Tathmini hiyo ilionyesha kuwa ili kufikia kikamilifu Dira ya Maendeleo ya 2025, sekta ya elimu ilihitaji kupewa kipaumbele cha pekee.

Hata hivyo, alibainisha changamoto kubwa: mishahara ya serikali, kutokana na ukubwa wa serikali yenyewe, inakula sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi. “Njia pekee ya kupunguza mzigo huu,” alisema, “ni kukuza uwekezaji, kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza mapato ya kodi.”

Kafulila alionya kuwa njia mbadala ya kutumia rasilimali zilizopo bila kuongeza uzalishaji ni hatari. “Ni sawa na kula mbegu badala ya kuzipanda. Hii ni tricky sana. Ukila mbegu, unakosa mavuno ya baadaye. Huwezi kuboresha elimu ya watu bila kujenga uzalishaji wa taifa. Ukichagua njia hiyo, unajikuta unagawana umaskini,” alisisitiza.

Aidha, Kafulila aliongeza kuwa tafiti nyingi zinasisitiza serikali kutumia angalau 60% ya mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya watu, na 40% kwa ajili ya maendeleo ya vitu. Alisema uwiano huu ni muhimu ili kuhakikisha ustawi wa wananchi unakwenda sambamba na uwekezaji katika miundombinu na sekta nyingine za uchumi.

Akihitimisha, Kafulila alisema kuwa tunahitaji uwiano sahihi kati ya matumizi ya kodi na kukuza uzalishaji ili kufanikisha maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya wananchi.

Inaanzia kwenye elimu bora ambayo serikali ambyo hatuna
 
Mbagala ya watu kuingilia dirishani kugombania magari Vs Mbagala ya watu kupanda mwendokasi yenye full air condituon,Unasemaje hapo Kafulila,ubora wa watu kuliko ubora wa vitu?
Sijaelewa unamaanisha nini, lakini sehemu ya pili ya sentesi yako inakubaliana na nilichokisema. Mwendokasi yenye AIC ni matokeo ya kuwa na vitu bora (barabara na magari) ambavyo vimeondoa shida au uduni wa watu (kupandia dirishani). Vilevile inatakiwa huduma ya mwendokasi iendelee kuwa bora ili maisha ya watu upande wa watu uendelee kuwa bora.
 
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), Bwana David Kafulila, akiwa katika Tengeru Institute of Community Development (TICD) jijini Arusha, amekaririwa akisema kuwa “Kwa mujibu wa sheria, mradi wa ubia ni mali ya umma kabla, wakati na hata baada ya utekelezaji wake. Lengo kuu ni kuboresha maisha ya watu.”

Katika muktadha huo, Kafulila alikumbusha kuwa mwaka 2014, Taasisi ya REPOA kwa kushirikiana na UNDP ilifanya tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa. Tathmini hiyo ilionyesha kuwa ili kufikia kikamilifu Dira ya Maendeleo ya 2025, sekta ya elimu ilihitaji kupewa kipaumbele cha pekee.

Hata hivyo, alibainisha changamoto kubwa: mishahara ya serikali, kutokana na ukubwa wa serikali yenyewe, inakula sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi. “Njia pekee ya kupunguza mzigo huu,” alisema, “ni kukuza uwekezaji, kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza mapato ya kodi.”

Kafulila alionya kuwa njia mbadala ya kutumia rasilimali zilizopo bila kuongeza uzalishaji ni hatari. “Ni sawa na kula mbegu badala ya kuzipanda. Hii ni tricky sana. Ukila mbegu, unakosa mavuno ya baadaye. Huwezi kuboresha elimu ya watu bila kujenga uzalishaji wa taifa. Ukichagua njia hiyo, unajikuta unagawana umaskini,” alisisitiza.

Aidha, Kafulila aliongeza kuwa tafiti nyingi zinasisitiza serikali kutumia angalau 60% ya mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya watu, na 40% kwa ajili ya maendeleo ya vitu. Alisema uwiano huu ni muhimu ili kuhakikisha ustawi wa wananchi unakwenda sambamba na uwekezaji katika miundombinu na sekta nyingine za uchumi.

Akihitimisha, Kafulila alisema kuwa tunahitaji uwiano sahihi kati ya matumizi ya kodi na kukuza uzalishaji ili kufanikisha maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya wananchi.

Usafi wa miji mikubwa umewashinda ndio mtaweza utajiri.🚮
 
Back
Top Bottom