Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,535
- 2,226
- Thread starter
- #21
sio anaweza kuwa Kafulila ni kiongoziAnaweza kuwa kiongozi

David Kafulila ni kiongozi mahiri mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza na kusimamia hoja zenye mwelekeo wa maendeleo. Tunampongeza kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya na tunamtia moyo aendelee kuchapa kazi kwa nguvu, ari na ubunifu zaidi. Tunatarajia kuona akiongeza kasi katika kubuni miradi yenye tija, kuibua mawazo mapya ya maendeleo na kusimamia utekelezaji wa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kadiri anavyoendelea kutumia uwezo wake wa kuchanganua masuala mbalimbali na kutoa suluhisho mbadala, ndivyo anavyozidi kuwa chachu ya maendeleo na msukumo wa mabadiliko chanya katika jamii.Watanzania hawapaswi kubaki watazamaji wakati fursa za uwekezaji na miradi mikubwa ya maendeleo zikiendelea kuongezeka nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amesema ni wakati wa Watanzania kujipanga na kushiriki kikamilifu katika uchumi kupitia ubia na kampuni za ndani na za kimataifa.
Akizungumza na wadau wa biashara na uwekezaji kutoka Mkoa wa Pwani, Kafulila alisema bado kuna uelewa mdogo kuhusu namna wananchi wa kawaida na kampuni za ndani zinavyoweza kushiriki katika miradi ya ubia, jambo ambalo linawanyima fursa nyingi za kiuchumi.
Alieleza kuwa chini ya sera na sheria za ubia nchini, kampuni za nje zinazoshirikiana na kampuni za ndani hupata mazingira mazuri zaidi ya kushiriki na kupata miradi kuliko zile zinazotaka kufanya kazi peke yake.
"Ni wito kwa kampuni za nje kutambua kuwa kushirikiana na Watanzania kunarahisisha utekelezaji wa miradi, lakini pia ni wakati wa kampuni za ndani kuamka na kutafuta ushirikiano wa kimkakati na wawekezaji wa nje ili kunufaika na fursa zilizopo ndani ya uchumi wetu," alisema Kafulila.
Alisisitiza kuwa ushiriki wa Watanzania katika uchumi haupaswi kuangaliwa katika umiliki wa miradi mikubwa pekee, bali pia katika huduma na shughuli zote zinazozunguka miradi hiyo.
Kwa mfano, alisema kampuni ya ndani inaweza isipate zabuni ya kujenga barabara moja kwa moja, lakini bado ikafaidika kupitia usambazaji wa vifaa, huduma za usafirishaji, chakula, malazi, vifaa vya ujenzi na huduma nyingine nyingi zinazounganishwa na mradi huo.
"Miradi mikubwa huibua mlolongo mpana wa fursa za kiuchumi. Tunapaswa kutazama picha kubwa zaidi na kuona namna gani Watanzania wanaweza kuwa sehemu ya thamani inayotengenezwa na uwekezaji huo," alifafanua.
Kafulila pia aligusia mjadala unaoendelea nchini kuhusu nafasi ya Watanzania katika uchumi wa taifa, akisema hoja muhimu si kutafuta nani ni mzawa kuliko mwingine, bali kuhakikisha wananchi wanakuwa washiriki wakuu wa maendeleo ya nchi yao.
"Jambo la msingi ni Watanzania kuwa sehemu ya uchumi wao wenyewe". alisema Kafulila
SahihiApplication ya hayo maneno huku kwenye field ndiyo ukweli ulipo ila siyo huko yanakosemewa
nini sahihiSahihi
MIJADALA YA MAANA SANA HIIKafulila hapa anaangalia zaidi faida za uwekezaji wa nje, lakini hoja muhimu ni nani anamiliki sehemu kubwa ya uchumi baada ya uwekezaji huo kuingia?
Haitoshi kusema Watanzania watanufaika kwa kusafirisha mizigo, kuuza chakula, kutoa malazi au huduma ndogo pembeni ya miradi mikubwa. Huo unaweza kuwa ushiriki, lakini si lazima uwe umiliki wa uchumi.
Nchi inayotaka kujenga uchumi imara lazima ijenge pia kampuni zake ziwe na uwezo wa kuwekeza, kumiliki teknolojia, kupata mitaji na kushindana kwenye miradi mikubwa. Korea Kusini, China na nchi nyingine hazikujenga nguvu zao kwa kuwafanya wazawa wawe watoa huduma pembeni tu; zilijenga uwezo wa kampuni za ndani kuwa wachezaji wakubwa.
Kwa hiyo uwekezaji wa nje ni muhimu, lakini sera iwe na mkakati wa wazi wa kuhamisha teknolojia, kukuza kampuni za Kitanzania, kuongeza local content na hatimaye kuongeza umiliki wa Watanzania katika sekta muhimu.
Tusije tukajivunia kwamba uchumi unakua, wakati Watanzania wengi wamebaki kuwa watazamaji au watoa huduma wadogo ndani ya uchumi unaomilikiwa na wengine.
SawaWatanzania hawapaswi kubaki watazamaji wakati fursa za uwekezaji na miradi mikubwa ya maendeleo zikiendelea kuongezeka nchini.