David Kasesela kinara wa biashara ya kusafirisha Wahamiaji haramu akamatwa jijini Mwanza

David Kasesela kinara wa biashara ya kusafirisha Wahamiaji haramu akamatwa jijini Mwanza

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh Mongela amesema Idara ya uhamiaji mkoani humo imefanikiwa kumkamata David Kasesela ambaye ni master mind wa biashara ya kusafirisha biashara haramu.

Mongela amesema kwa muda mrefu wamekuwa wanamsaka Kasesela na leo wamefanikiwa kumtia mbaroni akiwa na kundi la wahamiaji katika eneo la Majengo mapya.

Chanzo: Star TV!

Maendeleo hayana vyama!
 
Aisee hii biashara ya kuuza binadamu inakuja kwa mifumo mbali mbali kila baada ya muda flani.
 
Wana undugu na Richard Kasesela, Mkuu wa mkoa wa Iringa au ni majina tuu???
 
Siyo wageni tuu hata watoto wetu wa kike na hata wa kiume hapa Tanzania huwa wanasafirishwa kiharamu wanapelekwa Kenya, Afrika ya Kusini, Uarabuni, mpaka Ulaya. Watoto yatima, watoto masikini ndiyo wapo hatari zaidi lakini hata wa familia za kawaida tuu wanawezekana. Human trafficking and sex trafficking is a lucrative industry.
 
Mtoa mada hii wapi haki ya kuwa innocent hadi utakapokuwa umesimama kizimbani?why umeiandika jina la mtu wakati bado ni suspect?ona sasa unaanza kusababisha ukoo mzima kuhukumiwa na media,tuanze kuishi maisha ua mujibu wa kisheria tusilaumu serikali tu wakati sisi wenyewe ni wakosefu wakubwa,tangaza jina la suspect once atakapokuwa ameshafunguliwa mashitaka na kusimama mahakamani.
 
Diwani wa kata ya mapinga.
Ibrahim mbonde mpaka sasa yupo ndani sababu hyo hyo.ya wahamiaji .
 
Back
Top Bottom