''Mac Dizo, Pfunky prodakshizo'' alikuwa akipenda kutamka maneno hayo kwenye nyimbo zake.
Lakini huyu Mac dizooo wa mbwembwe hizo si mwenye sifa zilizotajwa !
Kuna jambo hapa , Sisemi RIP hadi uje ufafanuzi muafaka !
Huyu anayezungumzwa na mtoa taarifa,siye huyo unayemsema.
Nzi eh mac dee huyo ni nani na nyimbo gani alizozitoa hewani? Watu wengi Tunajua ni Huyu wa Dar skendo Holla wa pfunky produkshizo holla!
Wakuu nimeongea na mdogo wa marehemu ameniambia si mwanamuziki bali mtalaamu wa Ict. Marehemu nae alikuwa anajiita Mac D na moja kwa moja tafsiri ilienda kwa yule Mac dizo.
Poleni kwa usumbufu.
Nikiri kuwa katika kumfahamu kwangu kote David Mwenda Nkuba,sikuwahi kumjua kwa jina la MacDee.Alikuwa mtu mcheshi na kibonge fulani hivi mweusi.Alikuwa anafanya kazi Shule Kuu ya Sheria(zamani Kitivo cha Sheria) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Alikuwa mtaalamu wa takirishi na programu zake.Ni rafiki wa kila mtu.Lala pema kaka Nkuba...
Ok. Lakini ulikuwa ukimfahamu huyo kaka mtu? Ungeongea kwanza na mtu anayemfahamu ili utoe taarifa sahihi.
Anyway,
R.I.P kaka Nkuba.
Sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki. Kama anayedhaniwa kuwa amefariki ni yule mwanamuziki aliyekuwa chini ya P-Funk,basi huyu ninayemzungumzia siye. Kwa maelezo ya mwanzisha uzi,nina uhakika marehemu siyo Mac Dee aliyekuwa chini ya P-Funk. Labda kama alikuwa mwanamuziki kwa jina lingine;ndiyo maana nimeanza kwa kusema "sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki".
Ninasema hivyo kwa kuwa mke wake ni ndugu yangu kwa mbali.
Ni kweli amefariki,lakini siyo leo,amefariki jana pamoja na mjomba wake mmoja. Walikuwa wakienda Kahama,Shinyanga kupeleka gari jipya (lilitoka kununuliwa Dar) la mjomba wake mmoja aliyekuwa akiumwa Dar.
Inasemekana mjomba aliyekuwa akiumwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari,nafikiri ni maeneo ya Singida ama Manyoni ndiyo walipopata ajali baada ya tairi kupasuka. Nkuba na mjomba wake 1 ndiyo waliofariki (alikuwa na wajomba 2 katika safari). Mjomba aliyekuwa akiumwa,hajafariki.
Msiba upo pale UDSM,Ubungo Flats,eneo linaitwa Geti Maji. Ni geti la kuingilia UDSM kwa kutokea Ubungo. Mipango ya awali inasema marehemu Nkuba anaweza kuzikwa Kahama. Ingawa kwao kabisa ni Kahama. Kuna mtafuruku kidogo wa kindugu.
Bwana alitoa,bwana ametwaa. Jina lake lihidimiwe.
Pumzika kwa amani kaka Nkuba.
Kwa wale wanaomfahu
David Nkuba aka Mc Dee
amefariki leo kwa ajali ya
gari ndogo maeneo ya
Shinyanga.
David alisoma Azania
Secondary, Usagara High
School, alipita pia UDSM
kidogo na baadae
akamalizia masomo yake
Chuo Kikuu cha Mysore,
India alikosemea Shahada
ya Uhandisi na kubobea
katika Ectronics na
Communications.
David ni Mwanataaluma
mzuri wa ICT amefanya
kazi makampuni mbali
mabli na mpaka mauti
inamkuta mwajiri wake ni
Chuo Kikuu cha DSM, kitivo
cha Informatics and Virtual
Eduaction.
Ameacha Mke na mtoto
mmoja Melisa.
Msiba upo nyumbani
kwake Chuo Kikuu,
unaingilia gate la Maji
kama unatokea Ubungo,
unaenda kushoto.
Tujitokeze kwa wingi
kumfariji mjane na mtoto
na kutoa msaada wowote
utakaohitajika
Bwana alitoa na bwana
ametwaa jina lake
lihimidiwe.
basi kamanda omba mods wabadili heding maana mac d mwenyewe atainua bango....Wakuu nimeongea na mdogo wa marehemu ameniambia si mwanamuziki bali mtalaamu wa Ict. Marehemu nae alikuwa anajiita Mac D na moja kwa moja tafsiri ilienda kwa yule Mac dizo.
Poleni kwa usumbufu.
Omba mods wabadili title ya hii habari.......Wakuu nimeongea na mdogo wa marehemu ameniambia si mwanamuziki bali mtalaamu wa Ict. Marehemu nae alikuwa anajiita Mac D na moja kwa moja tafsiri ilienda kwa yule Mac dizo.
Poleni kwa usumbufu.
ni kweli, ka-edit ile taarifa yako ya kwanzaWakuu nimeongea na mdogo wa marehemu ameniambia si mwanamuziki bali mtalaamu wa Ict. Marehemu nae alikuwa anajiita Mac D na moja kwa moja tafsiri ilienda kwa yule Mac dizo.
Poleni kwa usumbufu.