Sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki. Kama anayedhaniwa kuwa amefariki ni yule mwanamuziki aliyekuwa chini ya P-Funk,basi huyu ninayemzungumzia siye. Kwa maelezo ya mwanzisha uzi,nina uhakika marehemu siyo Mac Dee aliyekuwa chini ya P-Funk. Labda kama alikuwa mwanamuziki kwa jina lingine;ndiyo maana nimeanza kwa kusema "sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki".
Ninasema hivyo kwa kuwa mke wake ni ndugu yangu kwa mbali.
Ni kweli amefariki,lakini siyo leo,amefariki jana pamoja na mjomba wake mmoja. Walikuwa wakienda Kahama,Shinyanga kupeleka gari jipya (lilitoka kununuliwa Dar) la mjomba wake mmoja aliyekuwa akiumwa Dar.
Inasemekana mjomba aliyekuwa akiumwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari,nafikiri ni maeneo ya Singida ama Manyoni ndiyo walipopata ajali baada ya tairi kupasuka. Nkuba na mjomba wake 1 ndiyo waliofariki (alikuwa na wajomba 2 katika safari). Mjomba aliyekuwa akiumwa,hajafariki.
Msiba upo pale UDSM,Ubungo Flats,eneo linaitwa Geti Maji. Ni geti la kuingilia UDSM kwa kutokea Ubungo. Mipango ya awali inasema marehemu Nkuba anaweza kuzikwa Kahama. Ingawa kwao kabisa ni Kahama. Kuna mtafuruku kidogo wa kindugu.
Bwana alitoa,bwana ametwaa. Jina lake lihidimiwe.
Pumzika kwa amani kaka Nkuba.