David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

Mbunge wa Chadema mh Silinde ameitaka serikali kuiongezea Tozo mizigo ya Zambia iliyoko bandarini kama majibu kwa wao kutufungia mpaka.

Silinde amesema hayo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya wizara ya mambo ya nje na kutoa mfano kuwa hata Marekani na China hulipana visasi kwenye vita vya kiuchumi.
Hata hivyo waziri Kabudi alimshushua kwa kumwambia kwamba mpaka haujafungwa.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Ghafla Silinde kawa mjinga, anafikiri bandari ni Dar tu; afterall Zambia walishaikimbia Bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi kikubwa na wanapitisha mizigo yao Beira, Durban na Walvis Bay
 
Dar si amini kama ni SILINDE. INAKUWAJE ANANENA KAMA "DRAGON"
 
Ubabe hauleti suluhu, wanaweza kuamua kutumia bandari ya Beira
I had two customers last two years from Zambia.. Hawa jamaa waliniambia DSM port ina bureaucracy sana.

Hivyo walihamia bandari Beira nadhani sio mbali sana na kwao.

Hivyo waache tu wajisahau watabaki na mizigo ya DRC na mdugu yao Kagame.

sent using Simenzi mayai
 
Huyu dogo Silinde amechanganyiwa sasa, nilikuwa upande wake ila naona amepotoka vibaya sana.

Silinde kumbuka bila mpaka wa Zambia pengine wewe usingekuwa mbunge 2010 Jimbo la Tunduma.

Ni fedha za wananchi wa Tunduma zilizotokana na mpaka wa Zambia ndio zilikupatia wewe ubunge, Ile jeuri ya kukuchangia hela ya kampeni, hela ya kula, hela ya mavazi na kila kitu ilitokana na mpaka huu.

Leo unasema serikali iengeze tozo kwenye mizigo ya Wazambia, njoo Tunduma uangalie ndani ya hizi siku tatu uone maisha wanayoishi Wanatunduma.

Hakuna kabisa mzunguko wa hela, hakuna kwacha, hakuna kiazi Wala mchele unaovuka huko....hakuna Nguo Wala vifaa vya ujenzi vinavyovuka huko Ile jeuri ya Wanatunduma imekata kabisa....

Nenda pale Kisimani uone kama watu wameshika hela kama siku zote ..piga simu kwa watu wako waulize nini kinaendelea Tunduma.

Serikali inaathirika ila wananchi wa kawaida ndio tunaathirika zaidi.

Watu kila siku wanaamka asubuhi wanasikiliza serikali ya Zambia itasema nini kuhusu huu mpaka..hakuna tamko lolote zaidi ya gari za Askari zinazozurura kulinda mpaka.

Hivi umejiuliza kuhusu Watanzania waliotapakaa Ndani ya Zambia nzima kuanzia Lusaka,Ndola,Kitwe kote huko Watanzania hawahesabiki...Unataka na wao wapewe masharti magumu ya kuishi huko.?

Umejiuliza Watanzania wenye maduka upande wa Zambia hapa Tunduma maarufu kama eneo la black...mpaka leo mamia ya maduka ya Watanzania yamefungwa na soko lote umejiuliza kuhusu familia zao wanakula nini wanaishije na familia zao.?

Leo Zambia imeruhusu maduka ya vyakula kufunguliwa lakini maduka ya Watanzania hawajaruhusiwa Wala kuvuka hawajaruhusiwa.

Unaongea kama huijui Tunduma kweli wewe Silinde unaetaka kurudi Tunduma kuchukua jimbo unatoa kauli hiyo kweli..

Nakushauri hiyo kauli tolea huko huko bungeni ukija kusemea hapa Tunduma utapigwa mawe mchana kweupe hata usiamini kinachoendela...

Bado WanaTunduma wanaimani na wewe ila kwa kaulizi hizi watakususa mapema sana na hutaamini.

Tena ikibidi waombe radhi Wana Tunduma, hiyo kauli ingetolewa na wabunge wengine tusingeshangaa maana wengi hawajui hali halisi ya Tunduma.ile sio wewe.

Ulietoka Dar na nauli tu kila kitu kuhusu maisha yako kikaanzia Tunduma.

Tunachosubiri WanaTunduma na Watanzania kwa ujumla ni mikakati ya pamoja kati Tanzania na Zambia ili shughuli ziendelee kama kawaida.

Kilichopo sasa ni kwamba serikali ya Zambia haina imani kabisa na Mtanzania yoyote yule kila wanaemwona wanahisi ana Corona.

Jaribu kuwa kiongozi mwenye maono, nchi zetu hizi maskini tunategemeana sana hatuwezi kukomoana ana akapatikana mshindi...

Ulisema unataka kukua kisiasa ila sasa naona unashuka viwango kwa kasi badala ya kupanda....
 
Tujihadhali sana katika maisha tumbo lisiunyang'anye ubongo kazi yake
 
Back
Top Bottom