David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

Huyu dogo Silinde amechanganyiwa sasa, nilikuwa upande wake ila naona amepotoka vibaya sana.

Silinde kumbuka bila mpaka wa Zambia pengine wewe usingekuwa mbunge 2010 Jimbo la Tunduma.

Ni fedha za wananchi wa Tunduma zilizotokana na mpaka wa Zambia ndio zilikupatia wewe ubunge, Ile jeuri ya kukuchangia hela ya kampeni, hela ya kula, hela ya mavazi na kila kitu ilitokana na mpaka huu.

Leo unasema serikali iengeze tozo kwenye mizigo ya Wazambia, njoo Tunduma uangalie ndani ya hizi siku tatu uone maisha wanayoishi Wanatunduma.

Hakuna kabisa mzunguko wa hela, hakuna kwacha, hakuna kiazi Wala mchele unaovuka huko....hakuna Nguo Wala vifaa vya ujenzi vinavyovuka huko Ile jeuri ya Wanatunduma imekata kabisa....

Nenda pale Kisimani uone kama watu wameshika hela kama siku zote ..piga simu kwa watu wako waulize nini kinaendelea Tunduma.

Serikali inaathirika ila wananchi wa kawaida ndio tunaathirika zaidi.

Watu kila siku wanaamka asubuhi wanasikiliza serikali ya Zambia itasema nini kuhusu huu mpaka..hakuna tamko lolote zaidi ya gari za Askari zinazozurura kulinda mpaka.

Hivi umejiuliza kuhusu Watanzania waliotapakaa Ndani ya Zambia nzima kuanzia Lusaka,Ndola,Kitwe kote huko Watanzania hawahesabiki...Unataka na wao wapewe masharti magumu ya kuishi huko.?

Umejiuliza Watanzania wenye maduka upande wa Zambia hapa Tunduma maarufu kama eneo la black...mpaka leo mamia ya maduka ya Watanzania yamefungwa na soko lote umejiuliza kuhusu familia zao wanakula nini wanaishije na familia zao.?

Leo Zambia imeruhusu maduka ya vyakula kufunguliwa lakini maduka ya Watanzania hawajaruhusiwa Wala kuvuka hawajaruhusiwa.

Unaongea kama huijui Tunduma kweli wewe Silinde unaetaka kurudi Tunduma kuchukua jimbo unatoa kauli hiyo kweli..

Nakushauri hiyo kauli tolea huko huko bungeni ukija kusemea hapa Tunduma utapigwa mawe mchana kweupe hata usiamini kinachoendela...

Bado WanaTunduma wanaimani na wewe ila kwa kaulizi hizi watakususa mapema sana na hutaamini.

Tena ikibidi waombe radhi Wana Tunduma, hiyo kauli ingetolewa na wabunge wengine tusingeshangaa maana wengi hawajui hali halisi ya Tunduma.ile sio wewe.

Ulietoka Dar na nauli tu kila kitu kuhusu maisha yako kikaanzia Tunduma.

Tunachosubiri WanaTunduma na Watanzania kwa ujumla ni mikakati ya pamoja kati Tanzania na Zambia ili shughuli ziendelee kama kawaida.

Kilichopo sasa ni kwamba serikali ya Zambia haina imani kabisa na Mtanzania yoyote yule kila wanaemwona wanahisi ana Corona.

Jaribu kuwa kiongozi mwenye maono, nchi zetu hizi maskini tunategemeana sana hatuwezi kukomoana ana akapatikana mshindi...

Ulisema unataka kukua kisiasa ila sasa naona unashuka viwango kwa kasi badala ya kupanda....
Juzi nilipita pale kisimani sikuamini wale watu wanaoshika maburungutu ya hela hawapo
 
Niliamini huyu dogo anaakili ila kwa leo ameniangusha.
chadema mnatuangusha kwa hiyo atetee zambia aache kutetea watu wa jimbo lake linalopakana na zambia? yeye ni mbunge wa Zambia au Tanzania? chadema ni chama cha kutetea watanzania au wazambia?

Kila hoja zikija nyie kazi yenu kusimama na watu wa nje madereva wakigoma kuingia nchi fulani ninyi kazi yenu kutetea hizo nchi zingine iwe uganda,rwanda,kenya au zambia!!!

nawauliza CHADEMA HICHO CHAMA NI CHA WATANZANIA AU WAGENI? MJITATHMINI WENYEWE

Silinde yuko sahihi hundred percent anasimama na nchi yake Tanzania na wapiga kura wake wa Momba
 
Juzi nilipita pale kisimani sikuamini wale watu wanaoshika maburungutu ya hela hawapo
Hela hamna mzunguko wa fedha hamna kabisa, wananchi wanasubiria mikakati ya serikali kwa pamoja ili maisha yaendelee kama kawaida hata maumivu yatakuepo yasiwe makubwa sana.
 
Mbunge wa Chadema mh Silinde ameitaka serikali kuiongezea Tozo mizigo ya Zambia iliyoko bandarini kama majibu kwa wao kutufungia mpaka.

Silinde amesema hayo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya wizara ya mambo ya nje na kutoa mfano kuwa hata Marekani na China hulipana visasi kwenye vita vya kiuchumi.
Hata hivyo waziri Kabudi alimshushua kwa kumwambia kwamba mpaka haujafungwa.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Amekua tutusa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chadema mnatuangusha kwa hiyo atetee zambia aache kutetea watu wa jimbo lake linalopakana na zambia? yeye ni mbunge wa Zambia au Tanzania? chadema ni chama cha kutetea watanzania au wazambia?

Kila hoja zikija nyie kazi yenu kusimama na watu wa nje madereva wakigoma kuingia nchi fulani ninyi kazi yenu kutetea hizo nchi zingine iwe uganda,rwanda,kenya au zambia!!!

nawauliza CHADEMA HICHO CHAMA NI CHA WATANZANIA AU WAGENI? MJITATHMINI WENYEWE

Silinde yuko sahihi hundred percent anasimama na nchi yake Tanzania na wapiga kura wake wa Momba
Kwa hiyo hoja Silinde hakuna alipowatetea Watanzania, zaidi amewakandamiza na kuwaumiza zaidi.

Halafu Wazambia hawajafunga mpaka kuwakomoa Watanzania, Bali kufanya tathimini kwa eneo dogo tu la Nakonde kwa wananchi wake.

Tatizo hata wakifanya tathimini haiwezi saidia sana bila kushirikiana na serikali ya Tanzania maana muingiliano wa Nakonde na Tunduma ni mkubwa sana.

Asilimia 90 ya bidhaa za Tunduma tunategema soko toka Zambia,Congo,Malawi na Zimbambwe kidogo.ila mteja mkubwa na kuaminika ni Zambia.

Nenda leo hata kariakoo kumepoa balaa, maana Tunduma ndio hua inachangamsha soko la Kariakoo kwa bidhaa zoote.

Kama umezaliwa Tandale na kukulia Tandale huwezi kuelewa hiki ninachokielezea.

Na huwezi kujua umhumu wa mahusiano na nchi jirani
 
Mbunge wa Chadema mh Silinde ameitaka serikali kuiongezea Tozo mizigo ya Zambia iliyoko bandarini kama majibu kwa wao kutufungia mpaka.

Silinde amesema hayo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya wizara ya mambo ya nje na kutoa mfano kuwa hata Marekani na China hulipana visasi kwenye vita vya kiuchumi.
Hata hivyo waziri Kabudi alimshushua kwa kumwambia kwamba mpaka haujafungwa.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Tangu ayanuwe maji ya mbogamboga amekuwa nyambafu kabisaaa

kifupi CHADEMA ni chama cha kutetea watu wa nje sio watanzania.Pitia nyuzi zote hadi matamko ya viongozi kwenye issue yeyote inayohusu Tanzania na nchi zingine CHADEMA Mara zote husimama upande wa hizo nchi zingine Kukiwa na issue yeyote kati ya Tanzania na nchi zingine

Watanzania tuna haki ya kukipiga chini hata kuiba kura kikishinda sababu ni chama cha foreigners watetea foreigners
 
Kijana mwenye miaka 35 anapokua na mawazo kama haya jua taifa limepata hasara sana ku-invest kwake.
 
Chadema kweli akili hamna
Huyo SILINDE NI MBUNGE wa Momba jimbo linalopakana na Zambia wapiga kura wake ndio wanaumia kwa maelfu sababu zambia ndio tegemeo lao

Kwa hiyo msimamo wa CHadema ni kutaka mbunge wenu atetee wananchi wa zambia sio wa Momba stupid nyie na hilo lichama lenu?

Kama mbunge ni wajibu wake kutetea watu wa Momba SIO WA zAMBIA na kafanya hivyo mnamtukana hivi nyie Chadema vichwa vyenu vikoje?
Kweli wewe akili huna
Uyo ni mbunge wa Ndugai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kifupi CHADEMA ni chama cha kutetea watu wa nje sio watanzania.Pitia nyuzi zote hadi matamko ya viongozi kwenye issue yeyote inayohusu Tanzania na nchi zingine CHADEMA Mara zote husimama upande wa hizo nchi zingine Kukiwa na issue yeyote kati ya Tanzania na nchi zingine

Watanzania tuna haki ya kukipiga chini hata kuiba kura kikishinda sababu ni chama cha foreigners watetea foreigners
Namsema Silinde sababu anaijua Tunduma nje ndani, alipaswa kushauli kidiplomasia na sio jino kwa jino kama anavyotaka.

Maana mpaka sasa wanachi wake hapa Tunduma wanapumulia mipira. Hali mbaya kila kitu kimesimama.

Wanakesha usiku na mchana Zambia iachie mpaka maisha yaendelee kama siku zote.
 
Mbunge wa Chadema mh Silinde ameitaka serikali kuiongezea Tozo mizigo ya Zambia iliyoko bandarini kama majibu kwa wao kutufungia mpaka.

Silinde amesema hayo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya wizara ya mambo ya nje na kutoa mfano kuwa hata Marekani na China hulipana visasi kwenye vita vya kiuchumi.
Hata hivyo waziri Kabudi alimshushua kwa kumwambia kwamba mpaka haujafungwa.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Ndugai constituent at work! A new constituent whose chair is Jiwe and vice chair Ndugai
 
Zambia wasubirie dawa yao iko jikoni
Msichokijua Kwa sasa kuna barabara inatengenezwa Kwa kiwango cha lami pia reli kutoka Beira Hadi Lusaka via Malawi so hivi karibuni watakua na option pia km pungufu.
 
Back
Top Bottom