Davido Alivuta Dolla 40,000 Fiesta

Davido Alivuta Dolla 40,000 Fiesta

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
Kwa mujibu wa MwanaFa akiwa kwenye kipindi Choice fm ni kuwa Davido alilipwa Dolla 40,000 kupiga show Fiesta.

Fa alihoji kwa nini waandaaji wasiwalipe dolla 10,000 wasanii wanne wa Bongo wapige show kali kuliko kuzipoteza kwa show mbovu ya Davido?

Je wadau wa Fiesta ni kweli kuwa show ya Davido haikuwa na thamani hiyo au ni kujikweza tu kwa Fa na wenzake?
 
nimehudhuria hiyo show,hana lolote,kucheza hajui,kinachombeba ni umaarufu wa nyimbo zake kwakuwa wabongo wanazijua.Sijui kwanini Clouds waliamua kupoteza hela kwa huyo, mbona TI alikuwa anatosha tu.Hizo hela za Davido wangewapa Weusi, MwanaFA, Mr. Blue, Stamina, Alikiba na Youngkiller maana walifanya show nzuri kumzidi
 
Huwezi jua biashara ya watu inawezekana Davido kawavutia wateja wakapata zaidi ya hapo,sasa mnalalamika nini wakati inajulikana wasanii wa bongo hamna mvuto kwa mashabiki
 
kwa nini hao kina mwanaFA wasijikusanye wakafanya shoo yao wenyewe wakajilipa wenyewe? Hii ndio tabu ya wabongo. mwanaFA ana masters, tena ya mamtoni, yule Nikki sijui ana masters na nasikia anataka kutafuta PhD,....Hivi akili hizi zote hawana ujanja wa kufanya shoo zao bila Clouds ya kina kibonde? Bakhresa kaishia la saba.....
 
Kaka hapa umechemsha!
 
Kwanza nasikia Davido alionekana anashangaa Big Screen wakati Weusi wanavyo floor nakuwapandisha watu mizuka na akauliza hawa jamaa ni nani akaambiwa ndio Miamba ya Kaskazini!
 
Show IPI bongo inavuta watu,kati ya wasanii Wa nje na ndani?
Lakini kama na wewe utakua ni mmoja wanao Support wanamuziki wa bongo hata sisi tunaweza - Mkataa kwao ni mtumwa kaka!
 
kwa nini hao kina mwanaFA wasijikusanye wakafanya shoo yao wenyewe wakajilipa wenyewe? Hii ndio tabu ya wabongo. mwanaFA ana masters, tena ya mamtoni, yule Nikki sijui ana masters na nasikia anataka kutafuta PhD,....Hivi akili hizi zote hawana ujanja wa kufanya shoo zao bila Clouds ya kina kibonde? Bakhresa kaishia la saba.....

MwanaFa ana masters ya mambo ya finance, kutoka Coventry univ.
Ktk music hatumii masters yake, bali anatumia div zero yake ya pcm na ile certificate yake ya IT kutoka ifm!
 
swali lingine ninalojiuliza hao Times fm walikubaliana nae kiasi gani mpaka jamaa akakubali kuchukua pesa ya Clouds!?
 
Davido aliomba kutumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta na akaomba alipiwe Ticket, Malazi 5 Star Hôtel, na hela kidogo Haikufika $ 40000.
 
Lakini kama na wewe utakua ni mmoja wanao Support wanamuziki wa bongo hata sisi tunaweza - Mkataa kwao ni mtumwa kaka!

Kaka wasanii Wa bongo hawana ushirikiano,kama miaka yote wananyonywa hivo kwenye show wangesikilizana,msanii Wa nje akiletwa basi wao wote wagome show halafu tuone hao wasanii Wa nje wanaolipwa mkwanja mrefu wavutie watu kama waandaji hawajapata hasara,wasanii wa bongo hawajielewi na hata wakipanga ni vigeugeu
 
Davido aliomba kutumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta na akaomba alipiwe Ticket, Malazi 5 Star Hôtel, na hela kidogo Haikufika $ 40000.

unachekesha Ndugu! yaani aharibu show yake na Times kwa show ya kubembeleza ya Fiesta!? bado haiingii akilini!
 
Alijulishwa kuwa Times ni kituo kidogo cha Radio Tz na Tamasha lao lisingefana, pia hakuwa akifahamu kama Fiesta ni week zile.
Kilichomrudisha tena ni kukata kiu za mashabiki wake ambao anaamini hakuwatendea haki katika Tamasha la Fiesta la mwaka jana kutokana na hitilafu ya umeme iliyokatisha onyesho.
 
kwa nini hao kina mwanaFA wasijikusanye wakafanya shoo yao wenyewe wakajilipa wenyewe? Hii ndio tabu ya wabongo. mwanaFA ana masters, tena ya mamtoni, yule Nikki sijui ana masters na nasikia anataka kutafuta PhD,....Hivi akili hizi zote hawana ujanja wa kufanya shoo zao bila Clouds ya kina kibonde? Bakhresa kaishia la saba.....

Kisomo cha makaratsi na mtaani ni vitu 2 tofauti.Kuna watu wana akili za darasini lakin za maisha ni 0.

Kazi kulalamika tu kwanini wasiunganishe nguvu wakaandaa show zao
 
Alijulishwa kuwa Times ni kituo kidogo cha Radio Tz na Tamasha lao lisingefana, pia hakuwa akifahamu kama Fiesta ni week zile.
Kilichomrudisha tena ni kukata kiu za mashabiki wake ambao anaamini hakuwatendea haki katika Tamasha la Fiesta la mwaka jana kutokana na hitilafu ya umeme iliyokatisha onyesho.

kwamba Times ni kituo kidogo si kweli. kwani alitakiwa kufanya show bure!? je angealikwa na mtu tu mwenye pesa yake angekataa kwa sababu hana jina yaani sio maarufu!?
 
Wenzetu wana vitu vingi sana wanaangalia katika kujenga Brand zao Duniani.
Hawaangalii Pesa tu peke yake.
 
Naomba unitajie baadhi ya hivyo vitu tafadhali!
 
Back
Top Bottom