Davido (David Adedeji Adeleki): They cheated again! (as Idris wins)!

Siungi mkono matusi,ila naomba niulize chris na kerucho sijui walikua big brother??angalia tweets zilizofata chini,bila davido dai angesimama tu!
 

Nassib alifanya maamuzi bila ya kutafakari, uamuzi wake ulikuwa kama kuamrisha Jeshi lake kwamba anzeni kumjibu huyu mtu.
Ni wazi fans wake walimheshimu Davido kwa sababu ya Nassib na pengine kwa hili wangemvumilia kwa sababu ya Nassib.
Sasa kitendo chake cha kumjibu kilikuwa na maana kwamba hata yeye (Nassib) alikereka na tweet ya Davido kwa jinsi alivyoielewa.
Kama mwanamuziki mwenye nia ya kujitanua barani Africa na kwingineko ulimwenguni huhitaji kuanzisha malumbano na nchi nyingine.
Bila ubishi, kwa hali ya kimuziki kwa sasa, Nigeria ndio mlango wa kutokea kwa kujitanua nje ya bara la Africa, tumeona Davido alivyomsaidia Nassib.
Malumbano yasiyo na msingi nadhani hayana tija kwa maendeleo ya entertainments za Tanzania, zaidi yanatuchafua tu kwa watu ambao tunategemea watushike mkono ili nasi kutoboa. So tuweke silaha chini tusonge mbele, hilo tuhesabu limeshapita na aliyekosa ameshakosa.
Ova
 
so kwanini a-direct kwa Diamond ujumbe huo? na mbona huwa afanyi hivyo kabla? Usitufanye sisi punguani kwa taarifa yako tunawajua Wanigeria kuliko wewe unavyowafahamu! BTW Diamond amejibu vizuri na kiustaha namsifu na ukizingatia katika ile remix walisema lagos will make Tanzania famous unfortunately not to know at what extent! That is over run even the master himself oyooooo :A S-rap:
 
Matola that's too much bana.....

Kwa hiyo vile anavyoongea katika interview huwa inakuwaje??...

Kiroho safi tu, kingereza cha kuongea na cha kusoma na kuandika kuna tofauti kubwa sana huenda nisieleweke hapa.

Mimi nimepata mwanga kidogo kuhusu hiyo tweet ya Davido baada ya Mrembo by Nature kufafanuwa na nashindwa kuingia deep kwa sababu mimi hata maana ya BBA sijui ni nini na wala hata mshindi anapatikanaje pia sijui na isitoshe mimi kwangu kwa maoni yangu BBA ni upuuzi tu na ushetani unaorasimishwa kinguvu sawa na tunavyolazimishwa kutambuwa haki za mashoga.

Therefore kwangu either wamechit au hawajachit hiyo kitu haina impact yoyote kwangu.

Last but list kutokujuwa kingereza siyo ulemavu Diamond ametusuwa kimaisha kuliko Maprofesa wengi tu wa chuo kikuu.
 
Last edited by a moderator:
Wewe I think,think again.Kwa wale tulokuwa tunafatilia bba na kupiga kura Kwa sana tunajua ni ushindan gan ulokuwepo kati ya idris na tayo. Jumlisha na suprise davido aliyo ipata tuzo za channel o ni ngumu Kwa yy kuficha hisia zake.UKWELI NI HUU😀avido anaamini tuzo za ch.o ni cheating na ushing wa idris ni cheating as well.Wanaigeria wanaamini south Africa na SADC wanataka kuwaharibia. Sasa Wewe mtetee David with ur shallow argument.
 
Na Wewe mmoja ya waliomtukania marehemu mama ake?

Si tu davido ni mwanamziki ninayempenda bali hata kama kuna mtu namchukia to the max. Siwezi mtukania mama yake, nawaheshimu sana wanawake hasa anayeitwa MAMA
 
hahahahaaa na mimi ndio najiuliza hapa labda huwa anakuwa amemeza memory card iliyorekodiwa majibu,
mtu akiamua kukuchukia bana!!!

Haya ni maneno ya kila siku tumeshayazoea nimchukie Diamond kwa lipi? Mtu ambaye hanijui wala mimi simjui na sijawahi kumuona popote zaidi ya kwenye media.

Kama chuki au wivu tungewaonea kina Bakhresa zawadi aliyoshinda huyo Idrisa BBA Bakhresa anaspend kununuwa gari moja tu la kumpeleka ofisini, achilia mbali mikwaju ya watoto wake.
 

Daimond aliwahi kuadmitt kuwa ras simba wake ni Wema so upo sahihi!
 
Mi ni Fan wa Diamond lakini simsupport kwa hili. Kuna mambo mengine ni busara kukaa kimya. Kwanza wataalamu wa lugha mtueleze vizuri maana kuna baadhi ya mitandao inasema Davido alimaanisha vingine. Maana nakumbuka hata mtu akisema X ame-cheat Kifo maana yake ni nini?Allin all hata kama ingekuwa maana halisi ile ya kiswahili ya kudanganya kwa kuwa ukweli unajulikana wa ushindi wake Diamond ange kaa kimya naamini ingekuwa busara zaidi.
 
usipende kujumuisha mambo ina watz hatuna dharau.tatzo n kukurupuka katutukanaje hebu nipe maana ya
na wametudanganya tena lol! Wewe au watz ndo waandaaj wa tuzo na mmedanganya vp status haituhusu

huyo mtoa mada na yeye kakurupuka au labda ni mfuasi wa stori za vijiweni,Ile tweet moja kwa moja ilikuwa inawalenga bba na wala sio chris brown na malaya wake ila alichokikosea diamond ni kuitafsiri kwa haraka zaidi matokeo akakurupuka akapost dongo akihisi kama alilengwa na yeye...mwisho wa siku huyo davido bado boya tu iweje ye ablame kwamba naija wanaonewa ina maana we ddnt deserve it?
 

Mkuu.. naomba niweke neno hapo la kuweka sawa.. kama ulifatilia vizuri wimbo ulochukua tuzo zooote tatu ni MY NUMBER ONE original na sio remix yake!!. Na pia hata ktk mualiko wa kule Big Brother aliimba original ambayo ilimwongezea hali ya ushindi in one way or the other!!
 

Ndugu afadhali umeliona hilo. Wabongo tunapenda sana kujidharau. Daima hatujiamini, ata akija mgeni akitutkana sisi poa tu. Kisa, nchi ya amani.

Baada ya ile tweet ya davido, wanigeria wenzake wametukana sana kuhusu Mtanzania kuchukua hiyo tuzo. Lakini watu hawaoni hilo, wako hapa kumtetea Davido kisa mgeni. Shame to us Tanzanians.

Wageni wanakujaga hapa wanadhalilisha dada zetu hapa huwa tunatulia tu, kisa nchi ya amani. Sijawahi kuona nchi kama hii duniani kote. Hii amani ni ya kishamba na kutojiamini aisee. Nimekaa korea, russia. Kule ukimdharau au kumtukana mwenyeji afu we raia wa kigeni, cha moto utakuona na hutarudia. Ila tz hapa utapigiwa makofi.

Angalia hiyo link hapo chini

http://viroba.blogspot.com/2014/12/davido-david-adedeji-adeleki-they.html
 

Lakini tweet yake ilianza na neno 'X', ambalo ndilo jina la album Mpya ya Chris Brown. Na tweet hiyo ameitoa katikati ya mgogoro wa kimapenzi wa Chris Brown na Karrueche Tran.
Ukitafakari kwa kina tweet ya Davido unaweza ukaona imelenga sana kwenye mgogoro wa Chris na Karrueche kwa sababu ya lile neno 'X'.
Pia, Chris na Karrueche wamekuwa wakiachana na kurudiana mara kwa mara, na safari hii inaweza kuwa mara ya tano au sita.
Kwa sababu hiyo watu wengi wamekuwa wakidai kwamba huwa wanadanganya kuachana. Sasa ni rahisi kwa Davido kuwa amezungumzia jambo hilo.
Pia, Davido ana sababu ya ziada ya kuzungumzia na kucheka kuhusu drama za Chris Brown, kutokana na kuimba na hasimu wake Wizkid, na kama unakumbuka naye Davido ametangaza kujiandaa kufanya collabo na Aubrey Graham Drake, ambaye ni hasimu wa Chris.
Kwa hiyo kabla ya yote waweza kutumia muda wako kutafakari hiyo tweet yenye fumbo, ambayo kama ulivyo ujumbe wa muziki, kila mtu anaweza kujidhani inamhusu yeye.
Ova
 

Haya basi sawa humpendi wala humchukii ila basi tu unajiskia tu kumaliza bandle lako kumponda.
 

Acha kutetea ujinga wa kutojiamini na kujifariji . wewe Mtanzani na jamaa amekuponda. Angalia hiyo tweet na comments zake below. Kuweni realistic acheni kutetea wageni na kuwaogopa ata akikutukana

http://viroba.blogspot.com/2014/12/davido-david-adedeji-adeleki-they.html?
 
Tatizo ni shule na level ya uelewa,Diamond na kiingereza chake cha kufundishwa na Wema unaadhani ageelewa zaidi ya alivyoelewa?
 
Kiumbe cha ajabu anaitwa amani michael kuptia twitter akamwandikia davido https://jamii.app/JFUserGuide you,your papa and your dead mama...ashoole!.davdo almjbu god bless u.

Mnanshangaza mnachekea davido kutukaniwa mama yake alyefark amani michael we n mtanzania mwenye maadili fikr vyema.

Inaumiza mzaz upendae amekufa watu wanamtukana muulzen kabwe anajua maumivu haya na alyepoteza mzaz yeyote.
 
Mimi hata sielewi mnaongea vitu gani, ngoja nirudi jukwaa la Wakubwa nikimalizie siku yangu
 

Ufafanuzi wangu hauzungumzii comments mkuu. Nazungumzia tweet ya Davido. Na wote walio comment tofauti huenda nao wameelewa vibaya kama Nassib na baadhi ya Watanzania wengine.
Ndio maana nikasema, hiyo Tweet ya Davido imekuwa kama ujumbe wa muziki (hasa Taarab) kwa anayesikiliza kuhisi kaimbwa yeye wakati mtunzi wala hamjui.
So usiunganishe maudhuhi ya tweet na comments za watu wengine, Kwani wewe hiyo comment yako inaendana na kilicholetwa na mleta uzi huu?!
Labda ungesema wagomvi wetu ni wale waandika comments kwenye tweet ya Davido, lakini kuwaacha hao na kumng'ang'ania Davido naona nasi tunakuwa hatujaelewa tweet.
Halafu hayo mawazo ya anayekutukana nawe mtukane unayatoa wapi? Yaani kutukana watu mtandaoni ndio solution ya tatizo kwa Watanzania?!
Kiukweli tumewazidi sana busara Wanaija, ukiishi nao japo kidogo utaelewa nachokisema. Kwa linaloendelea mtandaoni ni sawa na kujiweka kapu moja na vichaa.
Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…