Ufafanuzi wangu hauzungumzii comments mkuu. Nazungumzia tweet ya Davido. Na wote walio comment tofauti huenda nao wameelewa vibaya kama Nassib na baadhi ya Watanzania wengine.
Ndio maana nikasema, hiyo Tweet ya Davido imekuwa kama ujumbe wa muziki (hasa Taarab) kwa anayesikiliza kuhisi kaimbwa yeye wakati mtunzi wala hamjui.
So usiunganishe maudhuhi ya tweet na comments za watu wengine, Kwani wewe hiyo comment yako inaendana na kilicholetwa na mleta uzi huu?!
Labda ungesema wagomvi wetu ni wale waandika comments kwenye tweet ya Davido, lakini kuwaacha hao na kumng'ang'ania Davido naona nasi tunakuwa hatujaelewa tweet.
Halafu hayo mawazo ya anayekutukana nawe mtukane unayatoa wapi? Yaani kutukana watu mtandaoni ndio solution ya tatizo kwa Watanzania?!
Kiukweli tumewazidi sana busara Wanaija, ukiishi nao japo kidogo utaelewa nachokisema. Kwa linaloendelea mtandaoni ni sawa na kujiweka kapu moja na vichaa.
Ova