Davido (David Adedeji Adeleki): They cheated again! (as Idris wins)!

Davido (David Adedeji Adeleki): They cheated again! (as Idris wins)!

Nchi yetu imeshafeli kama Taifa na mtu mmojammoja hata Membe kwenye sakata la meno ya Tembo amelihutubia bunge kwamba wazungu wanatuonea "gere".

Hivyo usiwashangae wale wa vibundle vya promosheni vya mb50 kumponda Davido without know how.
Matola watu tunatofautiana uelewa, na pia tonafutiana jinsi ya kuhandle hisia zetu. Inawezekana wengi wetu tulielewa ndivyo sivyo, its ok. But reactions zetu hazikuwaa nzuri. Sijapenda walivyomtukana davido, kuna njia za kistaarabu tu za kumfikishia mtu ujumbe kuwa ulichosema hatujakipenda. Why insulting his dead mother?
 
Last edited by a moderator:
Hii ishu ya 'cheat' mnaikuza mashabik tu.

Wapuuzi ni walio mtusi DAVIDO.,, hakukua na haja.
 
Hukumbuki p-square walivyokuja bongo wakasema eti hawamjui diamond wala hawajawahi msikia. Wakati Obama "the world's president" alivyokuja bongo alimtaja hasheem thabit ambaye ata NBA hafanyi vizuri, just Because ya ustaarabu na kuthamini mchango wa watanzania.

So kama Obama anamjua hasheem basi ni lazima psquare wamjue Nassib?

Ana kweli kutumia smartphone haimaanishi kuwa na smart brain!!
 
Kiukweli tuache ushabiki maandazi.Waliomtukana davido kwa hali yakibinadamu wamemkosea sana.Yani tumeshindwa kureason kabisa kwa kauli yake kabisa kwa uelewa tu mdogo wa kauli yake ilikuwa inawahusu BBA maana ndio wanaojua utaratibu wa kumpata mshindi.
 
Mleta uzi umebugi meeen!! Tena sana

Kama Davido kajitetea kwa style hiyo basi sawa lakini ukweli haingii akilini kusema kuwa Alikuwa ana waongelea Criss brown na gf wake. Sisi sio watoto

Halafu Huu mtindo wa watanzania kujidharau na kukubali kuchukuliwa poa uishe aisee. Una mtetea kwa grounds za kitoto mno,

Utakuwa hawajui vizuri wanigeria wewe na Watu wa afrika magharibi kwa ujumla. Wana nyodo hakuna mfano,wanajiona wao ndio top kwa Afrika.

Davido hana lolote,he deserved all the insults. Kauli yake alimaanisha kuwa tuna pendelewa.

Big up Dimond,Hata kama Davido ndio alikutoa kimziki nje ya mipaka Lakini usikubali kudhalilishwa namna hiyo.

Mleta mada nenda kajipange,wanigeria sio watu,afadhali ya jirani zetu wakenya kuliko hao watu
 
Mleta uzi umebugi meeen!! Tena sana

Kama Davido kajitetea kwa style hiyo basi sawa lakini ukweli haingii akilini kusema kuwa Alikuwa ana waongelea Criss brown na gf wake. Sisi sio watoto

Halafu Huu mtindo wa watanzania kujidharau na kukubali kuchukuliwa poa uishe aisee. Una mtetea kwa grounds za kitoto mno,

Utakuwa hawajui vizuri wanigeria wewe na Watu wa afrika magharibi kwa ujumla. Wana nyodo hakuna mfano,wanajiona wao ndio top kwa Afrika.

Davido hana lolote,he deserved all the insults. Kauli yake alimaanisha kuwa tuna pendelewa.

Big up Dimond,Hata kama Davido ndio alikutoa kimziki nje ya mipaka Lakini usikubali kudhalilishwa namna hiyo.

Mleta mada nenda kajipange,wanigeria sio watu,afadhali ya jirani zetu wakenya kuliko hao watu

like like like
 
Chibu kachukia haswa... Hii ndo comment yake kule fb...

Instead of artists being role models and agents of unity, bringing our countries together to build a strong, prosperous peaceful continent, Africa. We are the first to instigate hate and regionalism. In this manner are we really building Africa? What is our fate? Continuing divide and rule inherited from the colonial era... Anyway, Happy Independence day Tanzania.....
( Badala ya wasanii kuwa ndio Mfano bora wa kuweka karibu Nchi zao na kujenga Africa yenye upendo na Amani...eti wao ndio Wanakua chanzo cha Kutenganisha nchi zao...Namna hii kweli tutajenga Africa? Anyway, Happy Independence day Tanzania....)
 
Kwa siku hizi tatu nimekua nikifuatilia hili saga alilolianzisha Davido pale alipotweet "They cheated again lol" kwenye ukurasa wake wa twitter. Nimeona bado majibishano baina ya Davido Vs Diamond kwenye kurasa zao za twitter na Instagram lakini pia Watanzania wanavyomshushia matusi Davido na celebs wengine wa Tz wakiendesha kampeni ya #UnfollowDavido

Lakini deep down nikiangalia naona a big hatred for Tanzania from Nigeria, kijana Idris alikua anaandamwa sana na wanaija baada ya kuona ni threat kwa mshiriki wao Tayo. Kwenye mitandao ya kijamii hawajaishia kumtukana Idris tu bali wametutukana na kutudharau hadi sie Watanzania wengine. Chuki iliendelea pale ambapo mshiriki wao alivyopigwa chini na Mtanzania Idris, Davido akatweet alichotweet lakini pia Billionea mmoja wa Nigeria yeye akatoa $ 350,000 kwa Mshiriki wao Tayo as compensation. Nimebaki kujiuliza kwanini atoe zaidi ya grand prize ya Big Brother?? Kwanini atoe usiku ule ule mshiriki wao alivyoshindwa?? Kwanini wasisubiri arudi nyumbani apewe kimya kimya?? Je, hizi si chuki tu na kutaka kujikomba kwamba wao ni zaidi?? Wanaija wanadhani kwamba wao ni zaidi ya kila nchi hapa Africa, even bigger than Africa itself. Mshiriki wao hakuwa na rafiki yeyote wa kweli ndani ya jumba, ndio maana wakati huu wenzake bado wamebaki South Africa kula bata yeye amesharudi kwao..

Nikirudi kwenye Saga la Davido, nimejiuliza ni kwanini katudharau hivi?? Cheated?? Maybe he saw us cheating somewhere, oooh yes sure alituona. Nadhubutu kusema Davido alituona sie ni ovyo kabisa pale alipokuja kwa mkataba wa kufanya show na Times FM lakini Clouds wakampa dau juu kwa juu wakamwiba pale Airport akaperform Fiesta. Times FM wakaenda hadi mahakamani na legal documents lakini bado Mahakama ikaachilia Davido awatumikie Clouds Media. Hapa La hasha Davido alituona sie ni ovyo na tumezoea cheating... Lakini ukweli unabaki pale pale chuki za Naijas kwa Tanzania na Other African countries zitawafanya waishi kwa shida sana nchi zingine za Afrika ukizingatia wao wamesambaa zaidi Africa...

My Take on this saga: Ningemwomba Billionea James Rugemalira nae atembeze mgao wa Escrow kwa huyu dogo Idris angalau kama zile digits za Chenge tuone kama Le Super Billionea Dangote kama atajibu mapigo nae...
 
Umejieleza vizuri.. But the thread ought to be merged to the main one.
 
Haina mahusiano yeyote na hili saga la 'cheat'.

Usitupotoshe.
 
Huwa bado nina mashaka makubwa kama Diamond ndio huwa anapost status zote kwenye hizo account zake, maana ninavyojuwa mimi Domo Kingereza kafundishwa na Wema je Domo ana uwezo wa kusoma kingereza na kupata tafsiri sahihi? Na mbaya zaidi mashabiki zake wanampeleka shimoni kwa nguvu kubwa.

Mashabiki wa Tz hasa wa domo wako emotional Sana. Hata hapa jukwaani angalia watu wanavyoargue kisa ushabiki mbuzi. Ukiwa na mashabiki wa hivi jua watakumislead tu tena kwa akili kashata Kama ya diamond ndo kabisaaaa
 
Back
Top Bottom