CARIFONIA
JF-Expert Member
- Aug 17, 2013
- 616
- 1,453
Msanii maarufu wa Afrobeats, Davido, ameibua gumzo baada ya kutoa tahadhari kali kwa Waafrika walioko ughaibuni na Wamarekani Weusi wanaopanga kuhamia Afrika. Katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye podcast ya Big Homies House, Davido alisema wazi kwamba hali si shwari barani Afrika, hasa nchini mwake Nigeria.
Akitolea mfano wa Nigeria, alifafanua kuwa licha ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta, wananchi wanalipa bei ya juu kuliko nchi zinazolazimika kuagiza mafuta hayo kutoka nje. "Uchumi uko kwenye mtikisiko mkubwa, na kiwango cha kubadilisha fedha kimevurugika vibaya," alisema msanii huyo.
Davido pia aliongeza kuwa tasnia ya burudani kama muziki wa Afrobeats inafanya Afrika ionekane nzuri machoni pa ulimwengu, lakini hali halisi ni tofauti kabisa. "Hatuwezi kufurahia rasilimali zetu wenyewe. Ninapokuwa nyumbani, huwa sionyeshi sehemu mbaya za maisha, lakini ukweli ni kwamba uongozi wetu haujafikia kiwango kinachohitajika," aliongeza.
Huku akiweka wazi kuwa hataki kuharibu sura ya Afrika, Davido aliwataka wale wanaofikiria kuhamia bara hilo kufikiria tena mpaka hali itakapokuwa bora.