- Kama ninavyosema siku zote uongo usipojibiwa na ukweli na mapema sana hugeuka kuwa ukweli, ukweli ni kwamba:-
1. Mimi na Davis Mosha bado ni wamiliki wa AST, tulifika mahali tukakubaliana kwamba ili kupata faida KUBWA kuliko tuliyokuwa tunapata ni bora kukodisha TV na Radio zetu kwa yoyote anayeweza kuiendesha na kutulipa kila mwisho wa mwezi.
2. Walitokea watu wengi waliotaka kukodisha, lakini kwa pamoja tukaamua kuwakodisha tunaowafahamua zaidi yaani DIZZM.
3. Mimi na my patner Mosha hatujawahi kugombana wala haitakuja kutokea kwa sababu tunazo biashara nyingi zaidi ya TV na Radio, infact kila jioni ya mwezi huu wa Ramadan Mosha ana tabia ya kuwaomba marafiki zake wote kufika nyumbani kwake kufuturu na huwa ninahudhuria sana.
- Hii chuki na wivu wa my lifstyle haikuanza leo najua kwamba haitaisha leo, kwa taarifa yako ni kwamba hata kwenye my Online TV & Radio Mosha yupo very much involved, poleni sana ndio mawazo ninayoyaita ya masikini ukiwazidi huwa kazi yao ni kuombea uanguke uwe kama wao....hahahahahahaha.....tafuteni lingine kwenye hili mmekosea sio ukweli kama mengine yote ambayo huwa mnahangaika nayo!
- Otheriwse, ninawashukuru sana kwa free media coverage maana siamini mpaka leo 2018 bado Brand yangu "Le Mutuz Superbrand" ina nguvu ya kupata page 11 hata bila mimi mwenyewe kuwepo, nilikua busy sana ndio maana sikuwepo.
- Nilisafiri Cape Town/SA nilialikwa na Cape Town International Jazz Festival kwenye maonyesho yao ya Dunia ya kila mwaka, niliporudi nilisaifiri kikazi Mbeya, Mwanza, Mbeya nikarudi Mwanza tena na majuzi nilikua Dodoma, ndio maana sikuwepo hapa muda mrefu sana ila sasa nipo Dar.
le Mutuz Superbrand