babi
Member
- Jul 24, 2012
- 79
- 109
Mfanyabiashara Davis Mosha leo ameongoza Harambee ya ujenzi wa Kanisa, Katika misa ya harambee hiyo iliyoendeshwa katika Kanisa la KKKT usharika wa Arusha Mjini, Davis Mosha aliyeongozana na Familia yake aliweza kuchangisha jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni mia nne.
Akizungumza katika Hafla hiyo fupi kanisani hapo, Davis Mosha alisema yeye pamoja na rafiki zake aliowashirikisha kwa Muda mchache baada ya kujua hitaji la kanisa hilo waliweza kumuunga mkono na kumuomba Mchango wao utambuliwe kama sadaka katika kufanikisha lengo hilo la kanisa. Huku akiahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na kanisa hilo mpaka kuhakikisha lengo kuu linakamilika kwa kiwango kinachohitajika.
"Leo kupitia waumini wenzangu pamoja na Rafiki zangu tumeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni Mia nne, Huu mi mwanzo mzuri katika Ujenzi wa kanisa na kukuza huduma ya kanisa, Nitoe wito kwa yeyote atakayeguswa kushiriki katika jambo hili basi ajiungane nasi katika kukamilisha kazi ya Mungu." Alisema Davis Mosha.
Ikumbukwe kuwa Mfanyabiashara Davis Mosha amekua Mstari wa mbele katika kujitoa katika ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo Misikiti na Makanisa katika maeneo mbalimbali