Davis Mosha akusanya zaidi ya milioni 400 kanisa la KKKT-Arusha Mjini

Mfanyabiashara Davis Mosha leo ameongoza Harambee ya ujenzi wa Kanisa, Katika misa ya harambee hiyo iliyoendeshwa katika Kanisa la KKKT usharika wa Arusha Mjini, Davis Mosha aliyeongozana na Familia yake aliweza kuchangisha jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni mia nne.

Akizungumza katika Hafla hiyo fupi kanisani hapo, Davis Mosha alisema yeye pamoja na rafiki zake aliowashirikisha kwa Muda mchache baada ya kujua hitaji la kanisa hilo waliweza kumuunga mkono na kumuomba Mchango wao utambuliwe kama sadaka katika kufanikisha lengo hilo la kanisa. Huku akiahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na kanisa hilo mpaka kuhakikisha lengo kuu linakamilika kwa kiwango kinachohitajika.

"Leo kupitia waumini wenzangu pamoja na Rafiki zangu tumeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni Mia nne, Huu mi mwanzo mzuri katika Ujenzi wa kanisa na kukuza huduma ya kanisa, Nitoe wito kwa yeyote atakayeguswa kushiriki katika jambo hili basi ajiungane nasi katika kukamilisha kazi ya Mungu." Alisema Davis Mosha.

Ikumbukwe kuwa Mfanyabiashara Davis Mosha amekua Mstari wa mbele katika kujitoa katika ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo Misikiti na Makanisa katika maeneo mbalimbaliView attachment 2010522

Sent from my SM-G980F using JamiiForums mobile app
Yaani kiufupi wewe ulie leta mada hii hapa utakua ndo Davis Mosha,unajaribu kusikia watu watasema nini kuhusu wewe kama wanakujua,yamkini una maovu yako unaenda kujifichia KANISANI
 
Wakiulizwa mmetoa wapi pesa nyingi ghalfla hivi wanakwambia tumepokea Sadaka, wakiulizwa nani katoa sadaka nyingi hivi wanasema Davis Mosha, Mosha akiulizwa anasema ni Marafiki zake ndio walimpa apeleke, akiulizwa ni akina nani hao atasema Sadaka ni siri, sipaswi kiwataja, kwisha mchezo
We unajiongea tu kufurahisha genge.FIU(Financial Intelligence Unit) watakuhoji hii pesa umetoa wapi uwaambie eti Sadaka Ni Siri? Hujui unachokisema mzee.
 
Mfanyabiashara Davis Mosha leo ameongoza Harambee ya ujenzi wa Kanisa, Katika misa ya harambee hiyo iliyoendeshwa katika Kanisa la KKKT usharika wa Arusha Mjini, Davis Mosha aliyeongozana na Familia yake aliweza kuchangisha jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni mia nne.

Akizungumza katika Hafla hiyo fupi kanisani hapo, Davis Mosha alisema yeye pamoja na rafiki zake aliowashirikisha kwa Muda mchache baada ya kujua hitaji la kanisa hilo waliweza kumuunga mkono na kumuomba Mchango wao utambuliwe kama sadaka katika kufanikisha lengo hilo la kanisa. Huku akiahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na kanisa hilo mpaka kuhakikisha lengo kuu linakamilika kwa kiwango kinachohitajika.

"Leo kupitia waumini wenzangu pamoja na Rafiki zangu tumeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni Mia nne, Huu mi mwanzo mzuri katika Ujenzi wa kanisa na kukuza huduma ya kanisa, Nitoe wito kwa yeyote atakayeguswa kushiriki katika jambo hili basi ajiungane nasi katika kukamilisha kazi ya Mungu." Alisema Davis Mosha.

Ikumbukwe kuwa Mfanyabiashara Davis Mosha amekua Mstari wa mbele katika kujitoa katika ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo Misikiti na Makanisa katika maeneo mbalimbaliView attachment 2010522

Sent from my SM-G980F using JamiiForums mobile app
Pesa ya cocaine
 
Wakiulizwa mmetoa wapi pesa nyingi ghalfla hivi wanakwambia tumepokea Sadaka, wakiulizwa nani katoa sadaka nyingi hivi wanasema Davis Mosha, Mosha akiulizwa anasema ni Marafiki zake ndio walimpa apeleke, akiulizwa ni akina nani hao atasema Sadaka ni siri, sipaswi kiwataja, kwisha mchezo
Na hapo ameshakubaliana na mchungaji anapewa % zake fresh kabisa
 
We unajiongea tu kufurahisha genge.FIU(Financial Intelligence Unit) watakuhoji hii pesa umetoa wapi uwaambie eti Sadaka Ni Siri? Hujui unachokisema mzee.
Hahahah, sasa hayo ndio maandiko ya biblia, mengine hayo utajuana nao.., sijasema kwamba utafanikiwa..
 
Yatima hawaishi kama ambavyo kipato chake kinavyoongezeka, mahekalu yanayokaa wazi wiki nzima kusubiri ibada mara moja kwa juma ni upuuzi wakati kuna watoto bado wengi mitaani.

Kwanza hizo sadaka za kujitangaza wakati Biblia yao inawataka mkono wa kushoto ukitoa wakulia usijue naamini hawajaisoma vizuri! Mbele ya fedha hata askofu aweza pindisha maandishi.
Punguza wivu asee wewe una vituo vingapi, au kwa mwaka unasaidia mayatima wangapi
 
Cha msingi ni usinipangie maoni yangu, pesa kila mtu anatafuta, haziokotwi mahali.
Nadhani hili ndiyo jibu sahihi kwa wenye kauli za: "tafuta pesa".

Maana siku hizi hatusemi, "tafuta pesa" limekuwa ndiyo jibu la jumla.

Ukiongea issue yoyote unaambiwa: "tafuta pesa"!

Sijui nani kaanzisha haka kamsemo ka kijingajinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta pesa wewe 😂😂🤣🤣, wanakera sana

Si ndiyoo; wewe utafute pesa then watu waje wakupangie matumizi; sheria ni moja tu kuwaudhi na wao wakatafute pesa waone kama watakubali kupangiwa matumizi
 
Back
Top Bottom