Davis Mosha akusanya zaidi ya milioni 400 kanisa la KKKT-Arusha Mjini

Davis Mosha akusanya zaidi ya milioni 400 kanisa la KKKT-Arusha Mjini

Wakiulizwa mmetoa wapi pesa nyingi ghalfla hivi wanakwambia tumepokea Sadaka, wakiulizwa nani katoa sadaka nyingi hivi wanasema Davis Mosha, Mosha akiulizwa anasema ni Marafiki zake ndio walimpa apeleke, akiulizwa ni akina nani hao atasema Sadaka ni siri, sipaswi kiwataja, kwisha mchezo
Mungu ndio jaji wa haki.Kanisani kwenyewe ukichimbua kwa jicho la kibinadamu na ukathibitisha hutakaa ukarudi kuabudu.Mwamini Mungu
 
Sasa wewe unataka kumpangia mtu maisha aishi kama upendevyo? Hela atafute mwenyewe matumizi umpangie wewe?

Tafuta hele ndugu uipangie matumizi wewe?

Pia usirudia tena kuniita mjinga maana nikianza kukuporomoshea matusi hii account utaifunga!

Tujibizane tu kwa ustaarabu!
Hujitambui, matusi umeshayaporomosha na account bado haijafungwa. Kichaa mwenye smartphone.
 
Still anahudumia mpaka kesho, Hizi nyumba za ibada ni one time needs. Nafikiri cha Msingi ni mimi na ww kutafuta pesa si kupangia wengine waliotafuta zao jinsi ya kuzitumia

Sent from my SM-G980F using JamiiForums mobile app
Mungu akubariki sana kwa ujumbe huu murua kabisa. Kongole
 
asante kwa utoaji maana imeandikwa " ya kaisali mpe........"
 
Mfanyabiashara Davis Mosha leo ameongoza Harambee ya ujenzi wa Kanisa, Katika misa ya harambee hiyo iliyoendeshwa katika Kanisa la KKKT usharika wa Arusha Mjini, Davis Mosha aliyeongozana na Familia yake aliweza kuchangisha jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni mia nne.

Akizungumza katika Hafla hiyo fupi kanisani hapo, Davis Mosha alisema yeye pamoja na rafiki zake aliowashirikisha kwa Muda mchache baada ya kujua hitaji la kanisa hilo waliweza kumuunga mkono na kumuomba Mchango wao utambuliwe kama sadaka katika kufanikisha lengo hilo la kanisa. Huku akiahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na kanisa hilo mpaka kuhakikisha lengo kuu linakamilika kwa kiwango kinachohitajika.

"Leo kupitia waumini wenzangu pamoja na Rafiki zangu tumeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni Mia nne, Huu mi mwanzo mzuri katika Ujenzi wa kanisa na kukuza huduma ya kanisa, Nitoe wito kwa yeyote atakayeguswa kushiriki katika jambo hili basi ajiungane nasi katika kukamilisha kazi ya Mungu." Alisema Davis Mosha.

Ikumbukwe kuwa Mfanyabiashara Davis Mosha amekua Mstari wa mbele katika kujitoa katika ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo Misikiti na Makanisa katika maeneo mbalimbali

Moshi tunamfahamu kama "YAHAYA"
 
Back
Top Bottom