Dawa hii ya meno, ya mitishamba ipo wapi tena?

Dawa hii ya meno, ya mitishamba ipo wapi tena?

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2019
Posts
442
Reaction score
729
Kuna dawa za mitishamba zinauwezo mkubwa sana.

Kama kuna dawa ilikuwa inaitwa ngetwa dfp kama nitakuwa nimekumbuka vizuri, sijui hii dawa imepotelea wapi, iliokoa jino langu.

Nilikwenda hospitali ya meno, dokta akaniambia hili jino ni la kung'oa, ilikuwa miaka kadhaa iliyopita na upachikaji wa meno bandia haukuwa ukijulikana sana.

Hivyo niliogopa kupoteza jino langu la mbele tena nikiwa katika umri balehe/teenage.

Ninakumbuka niliondoka kwa dokta nikiwa nimefadhaika sana, kwenda kuongeza pesa kwa ajili ya matibabu hayo.

Basi bana nikiwa kwenye dala dala nikasikia kwenye redio tangazo la hiyo dawa.

Nikashuka kwenye dala dala kituo kilichofuata, nikaiulizia nikaipata kwenye duka moja la madawa ya miti shamba!

Ilikuwa ya kusukutua mdomoni mara tatu kwa siku baada ya kuichanganya na maji ya vuguvugu katika kikombe!

Mpaka leo jino langu ninalo na imepita miaka takribani 15! Halijawahi tena kunisumbua!

Kinachonisikitisha ni kwamba nimeitafuta tena hii dawa mpaka leo siioni tena, siipati tena popote!

Msaada wenu tafadhali kwa mwenye kujua inapoweza kupatikana, ili ndugu na jamaa zangu wakipata hiyo shida wapate huduma hiyo!
 
ukifanikiwa kuipata nihabarishe mkuu, meno ni tatizo kwangu, nimeshaziba mpaka nimechoka
 
UYu jamaa aliacha mambo ayo nimelisahau jina lake nkilikumbuka ntaweka hapa.

UIksute makampuni makubwa yamemweka sawa atulie maana jino likioza watu wanauza dawa lukuki
 
UYu jamaa aliacha mambo ayo nimelisahau jina lake nkilikumbuka ntaweka apa.
UIksute makampuni makubwa yamemweka sawa atulie maana jino likioza watu wanauza dawa lukuki
Anaitwa somebody BUBERWA, sujui anamishe gani kwasasa
 
ukifanikiwa kuipata nihabarishe mkuu, meno ni tatizo kwangu, nimeshaziba mpaka nimechoka
Boss habari, aise ulipata dawa ya jino?mana mwenyewe nihatari nang'oa mpka yani pls nitafute unielekeze tafadhali
 
Back
Top Bottom