Dawa inayodaiwa kutibu UKIMWI yagundulika nchini Israel

Dawa inayodaiwa kutibu UKIMWI yagundulika nchini Israel

Status
Not open for further replies.
"Inasemekana", "Inapunguza". Kusemekana na kupungua sio kutibu. Hivyo hii si tiba, ni aina mya ya ARV.
 
Ukimwi ulitengenezwa na wanasayansi wa marekani na kwa kawaida mwanasayanc akitengeneza kitu huwa anatengeneza kwa formular ko walivyotengeneza ukimwi pia wakatengeneza na solutions ya ukimwi... Jaman dawa ya ukimwi ipo.. Nijuavyo mimi jaman
Wewe una uhakika kuwa UKIMWI ulitengenezwa na wamarekani?

Hiyo dawa ya UKIMWI iko wapi?
 
View attachment 479797

MAMILIONI ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ulimwenguni, sasa wanaweza kupata tumaini jipya baada ya wanasaynsi wa nchini Isreali kugundua dawa ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ukimwi.

Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Hebrew kilichopo Jerusalem nchini Israeli wamegundua dawa yenye protini ambayo wanadai inaweza kupunguza virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa mgonjwa kwa asilimia 97 ndani ya siku saba tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Times la Israel.

Ugunduzi huu mpya sasa unatoa tumaini jipya katika utafutaji wa dawa ya ungonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba ukiwa umeshaua watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka 2015 pekee.

Virusi vya Ukimwi hushambulia chembe chembe nyeupe za damu zinazojulikana kama CD4 ambazo husaidia kupigana na magonjwa yanayoingia mwilini.

Virusi vya Ukimwi huingia ndani ya chembe chembe hai nyeupe na kujizalisha kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa CD4.

CD4 zinapokuwa chini ya 200 kwa kyubiki milimita za ujazo wa damu, mgonjwa anahesabika kuwa tayari ameanza kuugua Ukimwi.

Ugunduzi huo mpya umehusisha majarabio ya dawa hiyo mpya ambayo iliwekwa kwenye damu ya wagonjwa 10 wa Ukimwi iliyokuwa kwenye chupa maalumu kwa ajili ya majaribio.

Sehemu kubwa ya dawa hiyo ambayo ilipewa jina la Gammora na watafiti, ilisababisha uzalishaji wa DNA ya virusi hao ndani ya CD4 iliyoathirika kujizalisha kwa wingi badala ya utaratibu wa kawaida ambao huzalisha moja au mbili.

Hii inasababisha chembe chembe nyeupe zilizojeruhiwa kujiharibu zenyewe na kuzifanya zishindwe kusambaza virusi zaidi.

Majarabia yanahusisha dawa hii mpya ya Gammora yataendelea kukiwa na matumaini makubwa kuwa itaweza kuua asilimia 100 ya seli zilizoathiriwa na Virusi vya Ukimwi.

Abraham Loyter mmoja ya wagunduzi wa dawa hiyo mpya, aliliambia gazeti moja la Israeli kuwa ugunduzi huo mpya unaleta tumaini jipya.

“Tunachokifanya sisi ni kuharibu seli ambazo zimeathirika na kwa hiyo zitakufa moja kwa moja na hazitaweza kusambaza tena virusi,” anasema.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Israeli ilitangaza kwa mara ya kwanza kugawa dawa zenye uwezo wa kuzuia maambukizi kwa makundi yenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya. Dawa hizo zinazojulikana kama prophylactic drugs zinapomezwa mara kwa mara zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi.

Kwa sasa, dawa pekee kwa watu wenye virusi vya ukimwi, ni dawa za kupunguza makali ambazo humezwa kila siku ambazo pia hupunguza uwezekano wa maambukizi mapya.

Historia inaonyesha kuwa VVU ilitokea kwa nyani waliopo katika Afrika ya kati katika miaka ya 1900. Kutokana na mwingiliano kati ya tamaduni tofauti na mataifa, vilianza kusambaa duniani.

Ukimwi uligundulika nchini Marekani miaka ya 1980 na ulijulikana kama Ukosefu wa Kinga kwa Mashoga (GRID). Kadiri muda ulivyokwenda, wagonjwa wengine watano waligundulika nchini humo, wote wakiwa ni mashoga mwaka 1981.

Wakati watafiti na wanasayansi wakiendelea kuumiza vichwa kupata majibu ya dawa ya ugonjwa huu unaendelea kugharimu maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kila mwaka, bado tiba au kinga yake ya uhakika imekuwa mtihani mkubwa ambao hadi sasa hakuna aliyeufaulu. Hata hivyo, wugunduzi huu wa wanasayansi wa Israeli unaweza kubadilisha matokeo.

Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini zina asilimia ndogo mno ya maambukizi yanayokadiriwa kuwa 0.1. Hii ni tofauti na nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo karibu asilimia tano ya watu wake wanakadiriwa kuwa wameaambukizwa VVU.

Kwa sasa tuna watu 7,500 ambao wanaishi na VVU hapa Israeli,” anasema Dk. Margalit Lorber ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Afya cha Haifa's Rambam kinachoshughulika na magonjwa yanayotokana na upungufu wa kinga ya mwili. Wagonjwa wapya 450 huripotiwa kila mwaka,” anaeleza.

Wakati asilimia ya watu walioathirika na VVU nchini Israel ikiwa ni asilimia 0.1, nchi hiyo ilianza tafiti kuhusiana na ugonjwa huo miaka 1990 wakati kulipokuwa na msukumo mkubwa duniani juu ya utafiti wa VVU na Ukimwi.

Wanasansi walioshiriki katika utafiti wa dawa hiyo mpya wanasema, majaribio ya ufanisi wa dawa hiyo yataanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na wanatarajia kuifanya tiba hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko dawa zozote za ugonjwa huo.

Gammora: The Possible Israeli Cure for AIDS - The Media Line
La muhimu hapo ni kuangalia kwa nini sehemu zenye watu wengi wa hiyo dini nyingine,maambukizo yao yao ni asilimia ndogo sana,ukilinginisha na sehemu zenye watu wasiokuwa na dini hiyo unayosema hawatatumia hizo dawa.Soma hiyo habari,mashariki ya kati na Afrika kaskazini,maambukizo ni asilimia ndongo,kuliko kwingineko.La muhimu ni sisi kuwafatilia hawa kujuwa kuna mbinu gani zinazofanya mpaka,kukawa na maambukizo ya asulimia ndogo sana
Nadhani wamekosea kusema wayahudi/Israel ndiyo wamegundua, ilipaswa waseme kuwa Marekani au nchi nyingine ndiyo wamegundua ili kutoa fursa kwa waathirika wa dini nyingine kuweza kutumia hiyo dawa.
Sasa kwa kutangaza hivyo wengine hawatatumia kwa kuwa bidhaa za nchi hiyo zimesusiwa na dini Fulani pia ni maadui wakuu
 
Mkuu mie sioni kama kuna shida yoyote hapo.
Unafikiri ni Dini gani watakwepa kutumia dawa hizo!?
 
Kama wanaruhusiwa kula nguruwe ili wasife, sidhani kama watakatazwa kutumia dawa ya waisraeli ili wasife pia. Wachague wenyewe, kifo au tiba.
Sima vizuri maambukizo yao ni asilimia ndogo sana,sehemu wanazoishi hao wa dini nyingine,angalia hapo maambukizo mashariki ya kati na Afrika kaskazini.Kuliko sisi tunaowasema wao.
 
Mungu ni mkubwa aendelee kutupa maalifa ya kupambana na ili janga. Hakika akuna kinachoshindikana chini ya jua I hop soon dawa itapatikana ya uhakika 100percent.na itasambazwa duniani kote.......tuzidi kumuomba mungu.
AMEN
 
Ukimwi biashara z watu hakuna dawa hivi karibuni mpk wakusanye fungu la kutosha na roho nyingi zipotee mavumbini ndio wataileta but sio sasa. But sio kwamba haipo hata kwetu za asili zipo but ukojitokeza tu either upotezwe au dawa yako ipotezwe au wote mpotee
 
pengine kuna ugonjwa mwingine wanataka kutuletea
 
Dawa ipo, kaka yangu alikua HIV positive tena alikua ameshapata AIDS kabisa, katibiwa na profesa flani wa pale SUA, Katumia dawa iyo miezi 18. Sasa ivi ni negative huu mwaka wa 3. Dawa zipo ila zinapigwa vita sana
EXPOSE MORE PLEASE
 
Nadhani wamekosea kusema wayahudi/Israel ndiyo wamegundua, ilipaswa waseme kuwa Marekani au nchi nyingine ndiyo wamegundua ili kutoa fursa kwa waathirika wa dini nyingine kuweza kutumia hiyo dawa.
Sasa kwa kutangaza hivyo wengine hawatatumia kwa kuwa bidhaa za nchi hiyo zimesusiwa na dini Fulani pia ni maadui wakuu
Hao wa dini nyingine,ni asilimia 0.1.Wakati sisi ni asilimia 5.Yaani hao wa Dino nyingine wanaoishi wengi wao masahariki ya kati na Afrika kaskazini,hata asilimia moja hawajafika kwa wenye UKIMWI,0.1% ni ndogo sana,ukilinganisha na Afrika peke Yake ya kusini mwa jangwa LA Sahara ni 5%.Na hiyo 0.1 katika hiyo mashariki ya kati,wapo wanaishi wa ile dini yatu 'pendwa' walio wachache huko mashariki ya kati na Afrika kaskazini.
 
Nadhani wamekosea kusema wayahudi/Israel ndiyo wamegundua, ilipaswa waseme kuwa Marekani au nchi nyingine ndiyo wamegundua ili kutoa fursa kwa waathirika wa dini nyingine kuweza kutumia hiyo dawa.
Sasa kwa kutangaza hivyo wengine hawatatumia kwa kuwa bidhaa za nchi hiyo zimesusiwa na dini Fulani pia ni maadui wakuu
ACHA UDINI
 
Isee wewe ni fundi wa propaganda si CDM wakuchukue tu

Haaa haaa teeeh teeeh acha nicheke.

Mimi Nina life yangu , siasa hizo za maji taka za bongo sitaziweza aisee.
Halafu, na chama ulichopendekeza hata nijiunge nacho ni uchwara tu maana kila siku nasikia wao ni kukimbia kimbia barabarani aisee hapana.

Mfano, hadi leo sina chama maana sitaki kuwa mnafiki, na mzandiki kama wanasiasa wengi walivyo hapo Tanzania.

Maana siasa, unaona kitu ni black wewe unaambiwa kasema hicho ni White. Siwezi.

In politics , white color turns to black color and the vice versa is true. I can't afford such a crazy life style!

Japo, nilichoandika ndiyo ukweli, japo na wengine wataongezea wanachofahamu juu ya dawa ya HIV/AIDS.

Ahsante pia kwa kuona kuwa naweza kufanya propaganda maana ni kazi inayohitaji akili sana, hadi sasa ni watu wachache sana wenye huo uwezo na hasa wako vitengo vya kijasusi vya nchi kama USA, Russia na baadhi ya nchi za Ulaya, Africa wapo pia, sema wanaweza wakatumika vibaya na watawala uchwara.
 
Nadhani wamekosea kusema wayahudi/Israel ndiyo wamegundua, ilipaswa waseme kuwa Marekani au nchi nyingine ndiyo wamegundua ili kutoa fursa kwa waathirika wa dini nyingine kuweza kutumia hiyo dawa.
Sasa kwa kutangaza hivyo wengine hawatatumia kwa kuwa bidhaa za nchi hiyo zimesusiwa na dini Fulani pia ni maadui wakuu

HAO HAO MAYAHUDI NDIO WALIKUWA MADAKTARI ENZI ZA MTUME MUHAMMAD {SWALLAHU ALAYH WA SALAM }

MTUME MUHAMMAD CHINI YA UTAWALA WAKE ALIWAPA ENEO LINAITWA KHAYBAR WAKAWA WANAISHI MAYAHUDI NA NDIO WALIOKUWA MABINGWA WA FANI YA UTABIBU MIAKA/ENZI HIZO.

NIHITIMISHE KWA KUSEMA KUWA MTUME MUHAMMAD ALIWAKUTA WAYAHUDI WANAISHI MJI WA MADINA.

Nilikuwa tu nakufahamisha ewe usiejua.
 
Ukimwi biashara z watu hakuna dawa hivi karibuni mpk wakusanye fungu la kutosha na roho nyingi zipotee mavumbini ndio wataileta but sio sasa. But sio kwamba haipo hata kwetu za asili zipo but ukojitokeza tu either upotezwe au dawa yako ipotezwe au wote mpotee

Kweli , kabisaaa.
 
Nadhani wamekosea kusema wayahudi/Israel ndiyo wamegundua, ilipaswa waseme kuwa Marekani au nchi nyingine ndiyo wamegundua ili kutoa fursa kwa waathirika wa dini nyingine kuweza kutumia hiyo dawa.
Sasa kwa kutangaza hivyo wengine hawatatumia kwa kuwa bidhaa za nchi hiyo zimesusiwa na dini Fulani pia ni maadui wakuu
Mbavuuu zangu kwahiyo haters watachukia na wasitumie.....
 
Mi nafikiri waarabu wana chakujifunza hapa!! ISRAEL imeanzishwa 1948 lakin hawamatch technologia yao!!
Waache kuvaa mabomu na kulazimisha watu kufuata wanachoamini....waanze kuonesha umuhimu wao kwa dunia....
Sio wao n kununua mtutu na mabomu tu....wawekeze ktk kusave life na technologies kusolve worlds challenges...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom