Dawa kutibu bawasiri

Dawa kutibu bawasiri

Ok nina kazi kidogo ngoja nimalize nitakupa maelekezo kuna Mama hapo ng'ambo sengerema alinisaidia kumtibu mwanangu leo ni miaka 9 hajawahi kusumbuliwa tena
Angesema yuko Dar ungesema kuna mama pale ilala, kind of wote mnajuana mtatupiga ap
 
Nenda hospitali ikakatwe,bawasiri ya nje inatibika kwa mitishamba ,sio ya ndani .
 
Angesema yuko Dar ungesema kuna mama pale ilala, kind of wote mnajuana mtatupiga ap
Sina njaa za kipuuzi namna hii
Na isitoshe kasema anaumwa sitaki hata mia ila nitamwelekeza sehemu niliyoyapatia matibabu ya kijana wangu
 
Hahaha bawasiri haitibiwa kwa dawa za hospitali wala za mitishamba.

Utameza madonge na mizizi mpaka uombe poo. Haitoki.

Bawasiri ikiota inakuwa kama kiungo katika mwili. Hakiondoki.

Dawa ya kufyeka shwaaaaa!
We mongo
 
Huu ushauri ni wa kupuuza Kuna mdada alikata ila nasikia kimerudi tena, so huu ushauri ni wa kuupuuza
 
Habari!

Binafsi ningependa kujua kama hiki unachotibu ni bawasiri/haemorrhoid.

Ombi ni kufika kwa mtaalamu wa afya kuthibitishwa na kupata mwelekeo wa kiasi cha tatizo kwani sijaona ni kwa jinsi gani umefikia kulielewa tatizo. Si kila njia aliyotumia mwenzako huwa pia inafaa kwako kwa tatizo lolote la kiafya. Hii inatokana na maelezo hapa chini.

Tunahitaji kuwa waangalifu tunapo tafuta tiba, suala linaloonekana dogo laweza kuwa kubwa au kutatuliwa kirahisi kulingana na njia utakayochagua kupita.

Wakati mwingine tumejikuta wenye msongo wa mawazo kwa kuona unatumia tiba sahihi lakini haupati nafuu. Kumbe hauko kwenye utaratibu unaofaa.

Mfano:
Bawasiri ni matokeo ya presha kwenye mishipa ya damu/veini kwenye eneo la haja kubwa.

Kuna aina mbalimbali ya visababishi, vyote vikihusishwa na mwongezeko wa msukumo kwenye njia ya haya kubwa:

*choo kigumu(yapo mengi hapa kwenye mwenendo wa maisha: kuto kunywa maji ya kutosha, kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama matunda, mboga za majani, ulaji wa nafaka kamili.

*ujauzito(kwa akina mama).

*kunyanyua vitu vizito.

*asili: kuta za njia ya haja kubwa si imara sana na kwa jinsi tunavyo simama ni rahisi kuachia kutokana na kolamu ya damu ndani ya mishipa husika.

Nk.

Bawasiri hutokea kwa kufuata sehemu ilipo mishipa husika. Kwa kufuata mfumo wa saa, saa 12, 03, 12 na 09. Unaweza kupata eneo moja au zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Pia huweza kujirudia eneo la zamani kama visababishi havikufanyiwa kazi.

Kuna aina ya bawasiri kulingana na sehemu:
  • internal/ ya ndani
  • externa/ya nje

Pia kuna grade za haemorrhoid:
1: grade ya kwanza: yenye dalili, mfano maumivu au kutoa damu lakini haichomozi.

2: grade ya pili: Inayochomoza na kurudi baada ya kujisaidia.

3: grade ya tatu: Inayochomoza na kurudi kwa jitihada/kurudishwa.

4: grade ya nne: Inayochomoza na hairudi.
Hata kwa jitihada binafsi.

Pia kuna acute/ndani ua muda mfupi na chronic/iliyokaa kwa muda mrefu.

Richa ya aina, grade na muda husika(acute/chronic) pia kuna suala la complications/ matatizo ambatanishi mfano: kuwa na mpasuko/fissure, embolism/ kuziba kwa njia husika ya damu, maambukizi/infection kwa eneo husika.

Ili tiba iwe kamilifu ni vyema mtoa huduma na mpewa huduma kuzingatia haya yote.

Hapa ndo uchaguzi wa:

1: Aina ya tiba(kutumia dawa vs upasuaji).
Aina ya dawa vs aina ya upasuaji.

2: tiba mwambata, ili kurahisisha uponaji na kuondoa visababishi vya tatizo kurudia.

NB: Kwa njia yoyote unayoamua kupata tiba, husisha wataalamu wa afya ili uweze kujua ni kitu gani na cha kiasi gani unachofanyia kazi.
Nashukuru docta Mimi Nina bawasiri ya ndani ninapojisaidia hutoka nikitembea hatua kadha inarudi
 
Nashukuru docta Mimi Nina bawasiri ya ndani ninapojisaidia hutoka nikitembea hatua kadha inarudi

Inonekana ni grade 2.:
Mambo mengine ya msingi ni:
1: kuna maumivu

2: ukubwa wake.

3: ina muda gani(acute vs chronic).

4: umewahi kupata damu (uwezo wa uwepo wa mpasuko/fissure na maambukizi).

5: mfumo wako wa maisha: ulaji, unywaji wa maji na upataji choo?

Haya huitaji majibu binafsi na kuangalia tatizo.
 
mimi nlienda kwenye famasi nkaambiwa bawasili inaweza kutibika kwa vidonge vinaitwa sitcom tablet nliambiwa nameza kimoja asubuhi kimoja jion kwa wiki mbili. bei nliambiwa ni 56000/= . Hiyo hela sikuwa nayo so sikununua. KWA mwenye hela ajaribu hvo vidonge halafu alete mrejesho

Vile vile kuna wadau wametoa ushuhuda kwa kutumia mafuta ya mbono. castrol oil... so kwa mwenye kujaribu nayo ni tiba pia.

m natumia dawa ya kunywa ya mitishamba imeondoa maumivu na imemove kutoka stage ya kutokurudi ndani na sasa hv inatoka wakati wa haja nkimaliza haja inakaa kidogo inarudi.... zamani ilikuwa muda wote ipo nje hata kukaa ilikuwa shida sasa hv at least nakaa....
 
hiz daw nilishatumia mm ilinisaidia kuondoa maumiv Yan saiz hakiumi hT kidogo ila hakijaisha bado kipo
 
hiz daw nilishatumia mm ilinisaidia kuondoa maumiv Yan saiz hakiumi hT kidogo ila hakijaisha bado kipo
Kuna dawa za ag nutrition naona zinatibu kabisa bawasiri,Kuna watu wengi wamepona Kwa kutumia hizo tiba
 
Back
Top Bottom