Amani iwe nanyi
Mtakumbuka raisi wenu mpendwa, mimi simo maana sipendi watawala, napenda viongozi tena wapenda haki na usawa yeye sio mmoja wapo.
Raisi wa Tanzania ameshawahi kuuhadaa umma wa Watanzania kwamba kuna dawa ya Corona imepatikana huko Madagascar na kwamba dawa ile inatibu COVID 19.
Akaenda mbali na kumtuma Waziri wake wa mambo ya nje akitumia ndege ya umma aliyoiagiza akiwa ndani na mtengeneza ndege bila hata kufuata sharia zetu za manunuzi.
Waziri akaenda na akarudi na michupa ya juice kama ya AZAM. Ni muda sasa tangu waziri na raisi wake wajitape kwamba wanawajali sana wa Tanzania na kwamba wamepeleka lindege wao kwenda kuchukua maji yale huko Madagascar.
Mbona hatujaambiwa dawa ile walikunywa Watanzania gani au tuseme watanzania waliokunywa ni wao wenyewe?
unatuma ndege yetu mpaka madagascer bila kutuambia matokeo ya safari. sisi wavuja jasho wa KARIAKOO tunauliza hivi:
Je, dawa ile walikunywa kinanani maana huku Kariakoo haijafika?
Je, gharama za kurusha ndege mpaka Madagascar zinaendana na faida za dawa ile?
Kama dawa ilikuwa na matokeo chanya au hasi.
Kama dawa ilinywewa. walikunywa wakina nani na kwanini wasipewe watu wote?
Mwisho, msituambie tu COVID-19 imeisha, twambieni wamekufa wangapi mkijumuisha na wale mliokuwa mnawazika usiku kule makaburi ya Kondo njia ya Ununio.