Dawa ya ajabu ya kuzuia kutapika niliyokutana nayo kwenye basi

Dawa ya ajabu ya kuzuia kutapika niliyokutana nayo kwenye basi

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
salamu,

Naomba kuwashirikisha tukio moja nililolishuhudia nikiwa safarini (kwenye bas) Wote tunafahamu kuna watu wakipanda gari huaptwa na hali ya kutapika sana! Hii huwalazimu wengine kutokula chakula safarini majuzi nikiwa safarini,dada mmoja alianza kutapika, hali hii ilimpa shida sana!

Moja wa abiria alimwita konda na kumuuliza kama ana Gazeti, konda alimwambia analo! Akamwambia chukua Gazeti hilo mwambia huyo dada (aliye kuwa anatapika) alitandaza na kuliweka chini ya kitikisha alikalie! Yule dada bila ajizi alitekeleza maelekezo hayo!

Kabla hata kuona matokeo ya ile dawa, nilishindwa kujizuia na kumuuliza yule"mganga 'kuwa ile ni dawa alichoonijibu bwana yule kuwa ni subiri matokeo ndiyo nitajua kuwa ni dawa au sio yule dada hakutapika tena hadi mwisho wa safari nilijiuliza sana nini mechanism ya ile dawa naelewa kuwa sampuli ya mgonjwa mmoja sio sahihi sana lakini inafikirisha!
 
aiseee.

Mimi pia niliwahi kusikia kuhusu Hilo ingawa sijawahi kuthibitisha..

nipo siti ya mbele.
 
Nina ugonjwa huo wa kutapika nikipanda basi.
Hua maskio yanaziba kabisa.
Hua natumia kila aina ya dawa nikiwa nasikia kichefu chefu kwenye basi.
Hizo ni baadhi ya mbinu.
  • Nakula pipi kifua
  • Nakaa Na Rambo pembeni
  • Nakula Pemba (udongo mweupe wanaokula wajawazito unatoka kigoma
  • Nakula limao Na kunusa
  • Hiyo ya gazeti nilifundishwa Na Mmama mmoja nilikua natoka mwanza.
  • Tembea ujionee..
~Da'Vinci
 
Ha ha a ha nimekumbuka kuna watoto huwa tunawatania wakiwa wanapanda boti wanunue magazet wakalie wasitapike sijajua logic yake ki ukwel
 
Wataalam wa dawa wanapofanya majaribio huwa wanatumia dawa halisi na dawa bandia. Hizi dawa bandia zinaitwa placebo na kawaida huwa ni sukari au kitu kingine kisichodhuru. Kuna wagonjwa wengine wakipewa placebo wanapona.

Imani ya mtu ni kitu hatari sana.
 
Kula pemba siyo crime kabisa, wewe endelea kula tu.
Sema huwa najiuliza kama JKT kama ile ya zamani ingekuwepo sijui kizazi hiki mngeishije.
Unaweza kuona nimeandika pumba ila MTU mwenye tatizo hilo akisoma halo anaweza pata kitu cha kufanya!
Mama yangu anafanya biashara ya kubumba Pemba hivyo nilikua namsaidia Mara nyingi tulikua tunahonja I'll kujua kama hazina mchanga..
Endeleeni kuniona mjinga
 
Unaweza kuona nimeandika pumba ila MTU mwenye tatizo hilo akisoma halo anaweza pata kitu cha kufanya!
Mama yangu anafanya biashara ya kubumba Pemba hivyo nilikua namsaidia Mara nyingi tulikua tunahonja I'll kujua kama hazina mchanga..
Endeleeni kuniona mjinga
Duuh dogo sikuoni mjinga bwana..
Kwahiyo wewe unaweza kuwa mjasilia mali mzuri tu halafu unazingua!
 
Back
Top Bottom