Dawa ya asili ya kiungulia ni nini jamani?

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
Nina tatizo la kiungulia kila ninapokula chakula chochote ambacho ni fresh, after five minutes kinaanza kunichoma sana, nimeenda hosp several times wananiambia nina dalili za vidonda vya tumbo wananipa dawa iitwayo Relcer na mavidonge kibao, ila nikagundua dawa ilikua inatuliza kwa muda na si kumaliza tatizo kwani kila dawa zikiisha kinaanza tena. huwa natamani kutapika nyongo ila haipandi kabisa, naomba kusaidiwa hata dawa za asili za kutibu nyongo nyingi na kiungulia kama zipo.
 
KIUNGULIA::

TIBA;:
Changanya glasi moja (250ml) ya maziwa na kijiko kikubwa 10ml) cha mafuta ya habat soda.
Kunywa mchanganyiko huu na urudie kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa siku 5. tumia kisha uje unipe feedback





Nigella Sativa oil au Black seed Oil ;Mafuta ya Habat Soda yanapatikana mjini Dar kwenye Maduka ya wauza Dawa za Kienyeji Karibu na sokoni Kariakoo..............Kaulize utapata huko.Au Uliza kwenya Ma-Super Market Makubwa yaliyopo mjini Dares-Salaam.
 
Nakushaur uwe unakula ubuyu kwa ajil ya kutuliza kiungulia bt cjui km n tiba ya mojakwamoja ila hutuliza kwa haraka au hata kuchanganya sukar na jivu ukalamba kwa pamoja nayo husaidia kupunguza maumiv. Kuhusu nyongo chukua ndimu/limao kamulia ktk kikombe then weka chumvi kdogo halaf unywe hukata nyongo. Ila ushaur wa awal uliopewa ndo mzur huenda n tiba kamil.
 

Ni magadi na dakika tu kiungulia kwishenei.Magadi yapo kila soko. Ukidharau hii basi endelea na huo ushauri mwingine
 
SIKONGE huwa tunatumia Karanga. Ila sema Karanga bana, zinaanzisha matatizo kwa wanaume unapoamka 🙂
Mnyamwezi Sikonge karanga mbichi zinaanzisha kitu gani?wakati unapoamka?Zinapoanzisha hizo karanga vurugu yake si utafutie dawa yake? dawa za karanga umpate mwanamke mzuri tu mambo yote kwishaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
nashukuru sana Dr, wangu nipo arusha nitajaribu kuisakama leo nikikosa nitaagiza huko dar, feedback utapata
 
nawashukuru woote kwa ushauri wenu nitaanza one after another ila huyo wa magadi na majivu nimekula sana sana kwani hata kwenye chakula tunaweka hasa vyakula vya asili kama kiburu, ngararimo na kimamtune lakini waaap, kwa wachaga hapa wanaipata hii milo vilivyo.
 
kunywa mafuta Ya Taa Na spriti vijiko Viwili Vya Chakula!
 
naomba umpe anti yako anywe hiyo spirit na mafuta ya taa then utanipa feedback,. watu wengine sijui wakoje, try to be seriouse watu tupo jf kwa ajili ya kuelimishana na si kuleta utani mahala penye userious,.kama huna la kushauri bora uache na si kumwambia mtu eti anywe mafuta ya taa> its terrible........:A S cry:
 

Kama unaona Ushauri Wangu Hauna Mantiki, Toa Wa Kwako Na Utibu Maswahibu Yanayomsibu!
 
kunywa mafuta Ya Taa Na spriti vijiko Viwili Vya Chakula!

Kama unaona Ushauri Wangu Hauna Mantiki, Toa Wa Kwako Na Utibu Maswahibu Yanayomsibu!
Mkuu Majigo Mbona unashauri mtu anywe sumu vipi mkuu? ushauri wako sio mzuri unaleta ushauri Negative kuwa Serious kuleta ushauri mkuu unaweza kupigwa BAN. Usilete maneno yako ya kihuni samahani kama ninakukwaza.
 
Mkuu, maji unakunywa? kiasi gani katika masaa 24?

Jaribu kila NUSU SAA kabla ya kula chakula unywe maji 500 ml na kisha unahesabu masaa 2 au mawili na nusu kila baada ya kula chakula na unywe tena maji 500 ml, kumbuka unywe maji ya kawaida katika joto la kawaida na siyo ya baridi mnayoweka katika friji.

Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA.
 
maziwa fresh ni dawa tosha,kunywa glass mbili kila siku utapona,nimesumbuliwa sana na hayo makitu sana lakin baada ya kuanza kunywa maziwa nimepona kabira
 
Inaonekana mwili wako unazalisha sana acid, jiwekee utaratibu wa kunywa maziwa fresh kila siku anglau glass moja. Kikemia maziwa ni alkaline, alkal + acid = maji na chumvi. kwa hiyo ukimywa maziwa una-neutralize. Mimi yamenisaidia sana.
 
Pia wawez weka maziwa kwenye kijiko cha chakula ukachanganya na mafuta ya korosho unakunywa mara hii moja tu basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…