Dawa ya kidonda sugu

Dukani

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
1,136
Reaction score
1,652
Jamani naomba kwa anayejua dawa ya vidonda kama hiki tupeane ushauri.

Historia ya kidonda
Alipata ajali miaka mitano iliyopita ametibiwa KCMC, Mt. Meru, Mawenzi, St. Joseph, NSK Arusha, bila mafanikio.

Amefanyiwa operation mbili kuondoa tissue zilizokufa, amefanyiwa skin draft mara mbili bila mafanikio.

Vipimo
X ray mara tatu
Sukari hana
UKIMWI hana

Amefanyiwa vipimo vyote kabisa hana tatizo lolote ila kidonda hakiponi.

Ni matumaini ya kuwa kwenye jukwaa hili kuna wajuzi wa mambo haya.


MCHANGO WA WADAU:

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjomba angu alipataga ajali alipata kidonda mguuni! Kidonda kilihangaikiwa hicho watu wakachoka! Sasa mwaka wa 15 huu anakidonda...kipo hivyohivyo, hakina dalili yakupona! Na ukikiacha siku 3 tu haujakisafisha utakutana na funza km Mia hivi! Kina harufu mnoo! Pole Sana...fanyeni maombi mno!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeraha la ajali linaweza kusababisha kansa?

Sent using Jamii Forums mobile app
of course kinasababisha vizuri sana,.jaribuni kupima kansa pia. Mama yangu alikua na jipu likakamuliwa kikawa kidonda na bika kujua akawa anatibu kidonda lakini hakifungi io ni ndani ya mwaka mmoja,.mwezi uliopita akaenda hospital akakutwa ana kansa,uzuri ni kua haijasambaa ipo kwenye kidonda tu.

kwaio kidonda chochote kikikaa mda mrefu hakifungi kinaweza sababisha kansa,mpelekeni mkamcheki kansa pia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri Mkuu,hiki kidonda kina miaka mitano sasa na ilikuwa ni ajali ya kawaida kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sure kabisa mkuu,huenda ni kansa,nashauri akapimwe kwanza kansa,ikimaliza vipimo kama hana kansa njoo pm nikulekeze dawa ya kutibu hiyo kidonda naamini itapona kabisa ikiwa sio Kansas,nb bila majibu ya vipimo vya kansa usinitafute
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasasa mnatumia dawa gani mkuu,?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri mkuu ,dawa za kienyeji tumeshatumia sana kaka bila mafanikio

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia unaweza kwenda kwa Dr ABBAS kariakoo yeye ni hodari wa kutibu vidonda vya kisukari, nashauri hivyo hata kama hana sukari, kwa uzoefu wake nadhani anaweza saidia,

Pili wakati mwingine kisukari hakionekani vizuri au wazi , aidha namna ya kukipima na kugundua naweza sema madaktari hawako makini, kupima mara moja au mbili damu ya mgonjwa na ukaikuta ni ya kawaida haina sukari SIO hakika kuwa hana kisukari, mm sio mtaalam, ila kugundua km mtu hana kisukari panahitaji juhudi za makusudi kwa kula chakula kwa makusudi then apimwe mara kadhaa angalau 4x hasa kwa wale wanao anza tatizo hilo inaweza kukuhakikishia kuwa kweli hana kisukari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…