Dukani
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 1,136
- 1,652
Jamani naomba kwa anayejua dawa ya vidonda kama hiki tupeane ushauri.
Historia ya kidonda
Alipata ajali miaka mitano iliyopita ametibiwa KCMC, Mt. Meru, Mawenzi, St. Joseph, NSK Arusha, bila mafanikio.
Amefanyiwa operation mbili kuondoa tissue zilizokufa, amefanyiwa skin draft mara mbili bila mafanikio.
Vipimo
X ray mara tatu
Sukari hana
UKIMWI hana
Amefanyiwa vipimo vyote kabisa hana tatizo lolote ila kidonda hakiponi.
Ni matumaini ya kuwa kwenye jukwaa hili kuna wajuzi wa mambo haya.
MCHANGO WA WADAU:
Sent using Jamii Forums mobile app

Hiki kidonda ni kizuri kina matumaini ya kupona.
Kwanza zingatia sana chakula cha mgonjwa, immune system inajengwa na chakula bora hasa nyama. Mboga, matunda na nafaka pia ni muhimu.
Kama ataweza kutokitia maji au kidonda kioshwe mara akimaliza kuoga.
Kuosha kidonda: hakikisha unazingatia usafi.
Chemsha nusu litre ya maji, yakiwa yanachemka weka chumvi 1/2 ya kijiko cha chai.
Taarisha bakuli, weka maji yaliyochemka na uweke vipande vya pamba au gauze hii utaipata pharmacy.
Acha maji kwa nusu saa mpaka yapoe. OSHA mikono yako na kisha chuku a pamba usafishe kidona. Pamba uliyosafishia weka kwenye mfuko wa uchafu.
Funika kidonda kwa plasta au bandage. Hivi utanunua pharmarcy. Kama utaweza kupata bandage za silver ni nzuri. Kipe kidonda nafasi ya kupona unaweza kusafisha kila baada ya siku moja. Kikiwa kinatoa maji mengi itabidi usafishe kila siku.
Ukiona dalili za usaha nendeni kwa daktari.
Sent using Jamii Forums mobile app