Dawa ya kidonda sugu

Habari!

Pole kwa yote yaliyowasibu kama familia.

Ni vyema kweli kufanya biopsy, maana ipo nafasi ingawa ni kidogo sana kwa aina ya kidonda husika kugeuka kuwa kansa bila kujali kilianzaje. Laki pia, uoteshaji wa usaa ni muhimu ili kujua mwelekeo wa dawa ipi itumike kwa mafanikio zaidi. Unaweza kukuta anatumia dawa ambayo tayari wadudu wamejenga usugu.

Aina ya kidonda hiki ni Venous Ulcer.
Kwa muda ambao kimedumu hiki ni Chronic Venous Leg Ulcer (CVLU).

Aina hii ya vidonda huweza kujianzisha vyenyewe au baada ya mchubuko/ajali au kuziba kwa mshipa wa damu unaosafirisha damu chafu/vein eneo husika.

Huwa vinaweza kupona kama vidonda vingine au kuchukua muda mrefu au kutopona kabisa. Hii yote hutegemea na usahihi wa huduma ambayo mhusika huweza kupata na hali yake ya kiafya kwa ujumla.

Uhudumiaji wa vidonda vya aina hii huitaji multidisciplinary approach:
1: Daktari bingwa wa mishipa ya damu
2: Mtaalamu dedicated wa uoshaji vidonda/wound specialist.
3: Afisa wa lishe
4: Daktari wa upasuaji nk.

Kwa hapa kwetu ukipata kliniki iliyobobea kwenye uoshaji wa vidonda inayofaa unaweza kusaidia pia. Ukifika kwenye hospitali za juu zaidi kama Aga Khan, sina uhakika wa kitengo husika kwa Muhimbili kipoje. Ila naamini ni uhitaji wa mtu mwenye experience nzuri na dedicated na awe na upendo kweli. Pia kuwe na positive supporting staff.

Mambo ya muhimu:
1: Uoshaji ukizingatia utaalamu
2: Kufahamu nini cha kuondoa au si cha kuondoa
3: Elastic bandage
4: Compression stocking
5: Kuunyanyua mguu wakati wa kupumzika
6: Kufanya mazoezi mepesi
7: Kupata virutubisho cha kujenga mwili
8: Antibiotics

NB: Wakati mwingine unaweza kwenda kwenye hospitali kubwa na kufanya consultation baada ya hapo unaweza kumpata mtoa huduma/muoshaji personally baadaye mkayajenga pale mambo yanaendelea vyema kwa mgonjwa wako. Ni nini cha kufanya.

Nawatakia matibabu mema.
 
Nakupa dawa konki, Tafuta ganda la kononkono lile kubwa kabisa liunguze upate jivu lake, utakuwa unaweka hapo kwenye kidonda kitakauka hata kama umetupiwa jini.
 
Pole sana mkuu, unamaanisha ni Donda ndugu au??

Kama ni kidonda kisichopona kwa zaid ya miez miwili ni kidonda ndugu, kinapona kwa urahisi mno ila matibabu yake huchukua zaidi ya miezi miwil.
 
Pole sana kwa huyo mgonjwa wako ninakupa huduma ya kwanza kabla hujanitafuta kwa wakati wako kila anapo amka asubuhi akojoe mkojo wake wa kwanza katika glasi kisha amwagie katika hicho kidonda afanye hivyo kila siku asubuhi kama ni kidonda cha kawaida atapona lakini kama ni kidonda cha uchawi itabidi unitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kumtibia apate kupona maradhi yake augue pole.
 
Akishindwa Bingwa mzizikqvu udisite kunitafuta nitakuelekeza la kufanya
 
Mkuu umefunga PM yako, mtu akitaka huduma yako private anakupataje?
 
Nawashukuru wote walionitia moyo mungu awabariki sana,,mgojwa alipona kabisa ni Jambo la kumshkuru mungu[emoji120][emoji120][emoji120]
Hongera sana aisee
Mmeteseka mno.

Mungu awasimamie,magonjwa na shida zisiwe upande wenu tena.
 
Nilipata wafadhili ndugu alitibiwa nairobi hospital

Inafikirisha. Ugonjwa ulioshindwa kutibiwa Tanzania umewezekana Kenya?

Mlijaribu pia MNH? Unajua matibabu sahihi yanategemea diagnosis sahihi.
 
Inafikirisha. Ugonjwa ulioshindwa kutibiwa Tanzania umewezekana Kenya?

Mlijaribu pia MNH? Unajua matibabu sahihi yanategemea diagnosis sahihi.
Kote huko tulienda ngoma ikawa ngumu,,,ushauri wangu kwa wanajamiiforums wote tutafuteni hela,,,kama siyo mkono wa mungu na fedha mgonjwa angepotea,,,namshkuru mungu sana[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…