Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Habari!Jamani naomba kwa anayejua dawa ya vidonda kama hiki tupeane ushauri.
Historia ya kidonda
Alipata ajali miaka mitano iliyopita ametibiwa KCMC, Mt. Meru, Mawenzi, St. Joseph, NSK Arusha, bila mafanikio.
Amefanyiwa operation mbili kuondoa tissue zilizokufa, amefanyiwa skin draft mara mbili bila mafanikio.
Vipimo
X ray mara tatu
Sukari hana
UKIMWI hana
Amefanyiwa vipimo vyote kabisa hana tatizo lolote ila kidonda hakiponi.
Ni matumaini ya kuwa kwenye jukwaa hili kuna wajuzi wa mambo haya.
View attachment 1290093View attachment 1290094
MCHANGO WA WADAU:
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa yote yaliyowasibu kama familia.
Ni vyema kweli kufanya biopsy, maana ipo nafasi ingawa ni kidogo sana kwa aina ya kidonda husika kugeuka kuwa kansa bila kujali kilianzaje. Laki pia, uoteshaji wa usaa ni muhimu ili kujua mwelekeo wa dawa ipi itumike kwa mafanikio zaidi. Unaweza kukuta anatumia dawa ambayo tayari wadudu wamejenga usugu.
Aina ya kidonda hiki ni Venous Ulcer.
Kwa muda ambao kimedumu hiki ni Chronic Venous Leg Ulcer (CVLU).
Aina hii ya vidonda huweza kujianzisha vyenyewe au baada ya mchubuko/ajali au kuziba kwa mshipa wa damu unaosafirisha damu chafu/vein eneo husika.
Huwa vinaweza kupona kama vidonda vingine au kuchukua muda mrefu au kutopona kabisa. Hii yote hutegemea na usahihi wa huduma ambayo mhusika huweza kupata na hali yake ya kiafya kwa ujumla.
Uhudumiaji wa vidonda vya aina hii huitaji multidisciplinary approach:
1: Daktari bingwa wa mishipa ya damu
2: Mtaalamu dedicated wa uoshaji vidonda/wound specialist.
3: Afisa wa lishe
4: Daktari wa upasuaji nk.
Kwa hapa kwetu ukipata kliniki iliyobobea kwenye uoshaji wa vidonda inayofaa unaweza kusaidia pia. Ukifika kwenye hospitali za juu zaidi kama Aga Khan, sina uhakika wa kitengo husika kwa Muhimbili kipoje. Ila naamini ni uhitaji wa mtu mwenye experience nzuri na dedicated na awe na upendo kweli. Pia kuwe na positive supporting staff.
Mambo ya muhimu:
1: Uoshaji ukizingatia utaalamu
2: Kufahamu nini cha kuondoa au si cha kuondoa
3: Elastic bandage
4: Compression stocking
5: Kuunyanyua mguu wakati wa kupumzika
6: Kufanya mazoezi mepesi
7: Kupata virutubisho cha kujenga mwili
8: Antibiotics
NB: Wakati mwingine unaweza kwenda kwenye hospitali kubwa na kufanya consultation baada ya hapo unaweza kumpata mtoa huduma/muoshaji personally baadaye mkayajenga pale mambo yanaendelea vyema kwa mgonjwa wako. Ni nini cha kufanya.
Nawatakia matibabu mema.