Dawa ya kitambi hii hapa

Dawa ya kitambi hii hapa

Vijana wengi Africa wanakufa Kwa sababu ya mangonjwa yanayosababishwa na mafuta mabaya mwilini. Nina kuhakikishia wala nyama choma, na bia wote wakipimwa lazima washauliwe wafanye mazoezi ya kupunguza mafuta mabaya mwilini. Hepburn siku moja nenda hospital na umwambie daktari unataka kuangalia cholesterol level yako. Hiyo ndiyo siku utajua umuhimu wa mazoezi. Ushahidi ni wangu mwenyewe. Chukua hatua Kijana.
 
Kama ninavyojua mimi kitambi ni matokeo ya mtanuko wa misuli ya tumbo inayosababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kula kupita kiasi.Sasa mleta mada anajaribu kutuelimisha eti ukinywa juice ya mchanganyiko wa ukwaju unavyoweza kumsaidia mtu kuondoa kitambi. Hili linawezekana lakini hakuna budi jitihada zingine zifanyike ikiwa ni pamoja na mazoezi na kula kwa kufuata wataalamu wa lishe bora wanvyoshauri. Mazoezi ndio sehemu kbwa ya ufumbuzi wa tatizo hili la kitambi, mazoezi yanasaidi kukaza misuli ya tumbo itakayolegea baada ya mafuta kupungua mwilini kupungua.

Mkuu siyo kweli. Kitambi ni mafuta yanakuwa mengi kuzunguka tumbo. Na mafuta hayo ni uzao wa kula hovyo. No balanced diet. Ngoja tuu kisu tukiite kisu na siyo Shoka.
 
Wandugu msaada,

Mke wangu ana kitambi mpaka namuogopa, je akiwa mjamzito si kitaburuza chini? Msaada jamani, afanyeje kiondoke kabisa kama si kupungua?
=========================
upload_2017-1-4_19-28-38.jpeg

Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi kikubwa.

Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani. Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.

Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.

Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango madhubuti kulikabili. Tatizo hili limezidi kuwa kubwa kwa vijana wengi miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya aina ya maisha wanayoishi (lifestyle), ambapo hula vyakula na vinywaji vyenye wanga kwa wingi (junk foods) kama vile chips, pizza, soda, bia na hawana muda wa kufanya mazoezi, na hata kufanya shughuli ambazo zitaushughulisha mwili (mazoezi, kutembea umbali mrefu, kukimbia,kubeba mizigo). Ukiwa na kitambi, maana yake ni kwamba, unakula chakula kingi mno kuliko mahitaji ya mwili wako, hivyo kupelekea chakula/nishati ambayo mwili wako hauhiitaji kubadilishwa na kuwekwa katika mafuta (fat), na kuhifadhiwa katika maeneo ya tumbo lako.

Vitambi vina madhara mbalimbali kiafya ikiwemo

1.Kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo- Tafiti zinaripoti kuwa, mtu mwenye kitambi, yuko kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya moyo, mara 5-10 zaidi ya mtu asie na kitambi

2.Kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya kisukari, saratani ya tumbo; watu wenye vitambi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa wa kisukari kuliko wale wasio na vitambi.

3.Kupunguza uimara wa mwili (physical fitness), na kumfanya mtu awe mzembe; mtu mwenye kitambi hana uwezo mkubwa wa kuwa na mwili ambao ni imara, na wenye kuhimili shughuli zinazohitaji nguvu na pumzi kama vile kukimbia, na hivyo kumfanya awe mzembe na goigoi

Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.

Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.

Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari,na si mbogamboga na matunda.

Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu.

Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.

MAGONJWA

Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya watu duniani kote. Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa ya moyo, kansa. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo na ndipo matatizo yanapoanza.

USHAURI WA KUJIKINGA NA KITAMBI



1.Hakikisha unapata walau nusu saa kila siku ya kufanya mazoezi/kutembea umbali mrefu/kukimbia hadi utokwe na jasho; hii itakusaidia kuondoa mafuta ya ziada katika mwili wako

2.Punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi kama vile chips, vyakula vya kukaanga; pia punguza matumizi ya sukari; na hakikisha katika mlo wako unakula matunda na mboga za majani kwa wingi (inashauriwa kuwa uwioano wa chakula cha wanga na mboga za majani/matunda uwe nusu kwa nusu katika kila mlo wako)

3.Achana na matumizi vinywaji vyenye sukari vya viwandani kama vile soda, pia epuka matumizi ya pombe hasa bia.

“Kitambi sio afya, ni dalili ya magonjwa, piga vita kitambi”

SIGNATURE

 
nimecheka kweli.jee yeye yupo tayari kufanya hayo mazoezi?maana kuna wanawake wengine,wanajikubali jinsi walivyo.ingia youtube kwenye search andika sit up workout for women.hayo mazoezi ni maaluma ya kupunguza tumbo.bila kusahau maji ya moto asubuhi lita 2 kabla ya kula,pamoja na kupunguza kula vyakula vya mafuta.
 
hata mimi jamani, mwambie aje tuungane tunakaribia kutolewa nje ya ulingo.
 
nimecheka kweli.jee yeye yupo tayari kufanya hayo mazoezi?maana kuna wanawake wengine,wanajikubali jinsi walivyo.ingia youtube kwenye search andika sit up workout for women.hayo mazoezi ni maaluma ya kupunguza tumbo.bila kusahau maji ya moto asubuhi lita 2 kabla ya kula,pamoja na kupunguza kula vyakula vya mafuta.

Kisukari thanks my dear, kumbe mimi nilikuwa nakosea kufanye situps. Du! watanikomaje mtaani, leo naanza
 
nimecheka kweli.jee yeye yupo tayari kufanya hayo mazoezi?maana kuna wanawake wengine,wanajikubali jinsi walivyo.ingia youtube kwenye search andika sit up workout for women.hayo mazoezi ni maaluma ya kupunguza tumbo.bila kusahau maji ya moto asubuhi lita 2 kabla ya kula,pamoja na kupunguza kula vyakula vya mafuta.

Hivi naweza kukopi kwenye CD ili niwe nafanya hm kwenye TV?
 
Jaribu kuwa karibu na rastafarian people wakuelekeze vyakula gani ni bora kwa afya yako na mwisho kabisa fanya mazoezi na mwisho kabisa pendelea kunywa maji moto/vuguvugu angalau lita mbili kwa usiku mzima na lita tatu kwa kutwa nzima.

Au rejea maoni ya mpungara hapo juu.
 
Mwambie apunguze kula kula
na afanye kazi za kutosha

mimi nimejinyima at least toka 2012
hadi leo nimeweza kupunguza kama
kilo nne hivi na kitambi kimepungua.
 
Fanya naye mapenzi mara kwa mara kuanzia asubuhi uamkapo, mchana na usiku kabla ya kulala siku zote za uhai wako kamwe kitambi hakitatokea ni kwa wanawake tu
 
Jaribu kuwa karibu na rastafarian people wakuelekeze vyakula gani ni bora kwa afya yako na mwisho kabisa fanya mazoezi na mwisho kabisa pendelea kunywa maji moto/vuguvugu angalau lita mbili kwa usiku mzima na lita tatu kwa kutwa nzima.

Au rejea maoni ya mpungara hapo juu.

sie tunapunguzwa na bhange tuuu.
 
Hivi naweza kukopi kwenye CD ili niwe nafanya hm kwenye TV?
unaweza,mimi mazoezi yangu ni ndani tu,sijawahi kuenda gym.ingawa mazoezi ya peke yako sometimes yanatia uvivu.kuna siku nafanya mazoezi kuna siku naacha
 
Pole sana mtu mzima. Ni muhimu sana kupenda kutunza afya yako na ya mwenzako pia. Watu wengi wanatakiwa kufahamu namna na umuhimu wa kutunza afya kwa mtu binafsi na kwa wengine. Hii ya kupunguza uzito na unene ni muhimu na nzuri sana kuweza kumudu japokuwa wengi hawapendi mazoezi na hawataki kujichosha. Uzito na unene unakuwa na madhara sana mwilini na kama mtu hawezi kuona madhara yake mara moja anaweza kuyaona baadaye ikiwemo ya kusumbuliwa na joints, mzunguko wa damu mwilini, cancer, kukosa usingizi, nk. Fuatilia njia njema ya kuweza kuondoa tatizo la unene/uzito bila kupata tabu zisumbuazo mwili kama geam, kujinyima chakula nk. Lishe muhimu iliyoandaliwa kiasilia na iliyofanyiwa utafiti muda mrefu na kuonekana njema sana kwa ajili ya afya.

MAGILIM

Inatokana na majina ya Magic-Slim, jina hili likabadilishwa na kuitwa Magilim.
Imetengenezwa kwa mimea kadhaa, mimea hiyo ni;

  • Seamen cassie
  • Cassia bark
  • Mullberry leaver
  • Fago fyrum tataricum
Ikiingia katika utumbo mdogo huyeyuka kuwa ute ute na gel husaidia kugandisha mafuta uliyokula ili yasitumike mwilini, na kufanya mwili kutumia mafuta yaliyoko wilini tu, hivyo kusaidia kupunguza mwili na uzito.
Ikiingia kwenye utumbo mkubwa inasaidia kugandisha maji ya nyongo na chumvi chumvi zake.
Ini huwa inavunjavunja mafuta na kutengeneza;

  • Maji ya nyongo
  • Nguvu ya mwili(glucose)
  • Uric acid
Magilim ukiinywa inasaidia kugandisha maji ya nyongo na mafuta, pia husaidia kwenda kwenye damu kutoa sukari na uchafu kupitia kwenye figo.
Matokeo yake mwili hukosa nguvu kwa kutoa sukari na mafuta, kugandishwa pamoja na maji ya nyongo kwenye utumbo mkubwa na mdogo.
Kufanya mwili kulazimika kutafuta nguvu kwenye hifadhi zake, sehemu zenye mafuta mfano kitambi, ------ na mikononi wanawake. Wanaopunguza unene na uzito hivyo mwili unatengeneza kemikali inayosaidia kutoa mafuta kwenye mwili na yanasafirishwa na damu kupelekwa kwenye ini pale ambapo ini huvunjavunja yale mafuta na kutengeneza vitu vitatu; maji ya nyongo, nguvu ya mwili ana uric acid. Wakati huo maji maji ya nyongo yanazidi kugandishwa na mafuta kwenye utumbo mkubwa na mdogo.

  1. Uric acid na sukari inatoka kupitia figo kwenye mkojo na kufanya mwili unazidi kutoa mafuta kwenye hifadhi zake mwilini na kufanya mtu azidi kupungua(kukonda).
Magilim inasaidia kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu na kuzuia mwili kunyonya vyakula vya wanga kwenye utumbo mdogo na kutoa sukari kwenye damu kupitia figo, huleta faida kwa wagonjwa wa kisukari na wale wanaotaka kujizuia kupata matatizo ya sukari.
Magilim ikiwa kwenye ute ute(gel) kwenye utumbo inasaidia kusafisha utumbo mkubwa na mdogo na kusafisha mfumo wote wa kusagia chakula.

KAZI YA MAGILIM

  • Kupunguza uzito na unene
  • Kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu
  • Kusafisha mfumo wote wa kusagia chakula
  • Inapunguza uwezo wa mwili kunyonya lishe
  • Kutoa sumu mwilini
  • Kutoa chunusi mwilini
  • Kutibu matatizo ya tumbo

CORDY ROYAL JELLY

Bidhaa hii imetokana na mmea wa cordy ceps sinensis na Royal jelly.
Royal jelly – Inatokana na chakula maalum cha malkia wa nyuki.

FAIDA ZA CORDY ROYAL JELLY

  • Ina vitamin A,B,C,D,E na K ni chakula kilichokamilika.
  • Inaondoa cholesterol
  • Inaimarisha mfumo wa damu mwilini.
  • Ina faty Acid
  • Inaongeza nguvu na kutoa uchovu na kutoa sumu mwilini
  • Inakufanya usizeeke haraka(anti aging)
  • Kulainisha ngozi na kufanya ngozi kuwa nzuri
  • Inafanya damu kuwa nyepesi
  • Inaimarisha usafirishaji wa damu mwilini
  • Kuweka kiwango cha mafuta na cholesterol sawa.
  • Mafuta yaliyoganda kuzunguka moyo na kwenye mishipa ya damu huyeyusha na kulainisha mishipa ya damu.

GOLDEN SIX

Golden Six imetokana na mimea sita(six golden herbs) inamaanisha mimea sita yenye thatmani.

Golden six inahusika na sehemu zifuatazo;

  1. Mishipa ya hisia
  2. Figo
  3. Kuinua kinga ya mwili na kinga ikiwa nyingi kwenye mwili inasaidia uroto kwenye mifupa(born marro), ndiyo inatengeneza cell za mwili.
  4. Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee.

Utendaji kazi wa Golden six;

  • Golden six ina kinga kubwa kwenye mwili, ukiitumia vizuri inakwenda kusawazisha kinga kwenye mwili.
  • Inarutubisha uroto kwenye mifupa nah ii hutengeneza chembechembe nyeupe za damu kwa haraka.
  • Golden six inasafisha figo kwa kuipa nguvu ya kusafisha damu, kuondoa sumu mwilini kama vile uric acid.

Uric acid ikiwa kwenye viungo husababisha kuumwa kwa viungo.

  • Kuhisi uchovu
  • Kutokwa na jasho sana
  • Kuumwa sehemu ya chini ya mgongo na pia kukosa usingizi.

Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee mfano;

  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kutoona vizuri
  • Misuli kukosa nguvu
  • Chembechembe za mwili kufa kwa haraka
  • Inajenga mishipa ya hisia na kuondoa matatizo ya kupooza
  • Kwa waliopooza na kuathirika kwenye mdomo (mdomo kupinda) katika mazungumzo inawasaidia na kurekebisha mazungumzo yao.

FAIDA ZA GOLDEN SIX

  • Stroke(kupooza)
  • Kukosa usingizi
  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kuumwa na viungo
  • Kusafisha damu
  • Husaidia presha ya kupanda inayosababisha mishipa kubana hii hutokana na aina Fulani ya Adrino gland ambayo hutoa kemikali, husababisha kubana kwa mishipa ya damu.
  • Matatizo ya wanawake na ukomo wa wanawake


Yeyote anayehitaji msaada zaidi labda kutaka kuuliza au ushauri anaweza kunipigia kupitia namba 0776491294 pia anaweza kuniandikia ujumbe kupitia ishealthy@hotmail.com
Gharama za MAGILIM ni Tsh. 62500/-, CORDY ROYAL JELLY 68000/- na GOLDEN SIX 38000/-
 

Attachments

  • MAGILIM.jpg
    MAGILIM.jpg
    15.2 KB · Views: 491
  • CORDY ROYAL JELLY.jpg
    CORDY ROYAL JELLY.jpg
    15.7 KB · Views: 470
  • GOLDEN SIX.jpg
    GOLDEN SIX.jpg
    14 KB · Views: 465
Back
Top Bottom