Dawa ya kumrudisha mpenzi, mume/mke mliyeachana inawezekana kweli?

Kimbisa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2020
Posts
479
Reaction score
645
Habari wana JF! mimi si member mpya katika kijiwe chetu pendwa ila nimeweka ID mpya sababu ya kulinda kujulikana ni nani maana wengi wananifahamu ID yng humu JF.

Jamani wakuu naombeni msaada, tumekwazana na mpenzi wangu kama yalivyo mapenzi ila amebadilika ghafla, yaani ninavyosema ghafla namaanisha, maana hakuwa na huwa hana tabia kama hizi alizonazo. Kuna muda anabadilika, mara anakaa sawa, nimekaa naye chini kiupole sana kumuuliza tatizo ni nini hana cha maana anachojibu.

Yaani kiufupi amekua haeleweki, kibaya zaidi ananiambia tuachane. Yezekana naonekana kama mjinga ila kiukweli moyo wangu unakataa kabisa kabisa kumuacha aende, tumekua kwenye mahusiano kwa muda mrefu tumefanya vingi, hii hali imenifanya siwezi kabisa kumsahau nimejitahidi nashindwa.

Nalala usiku naweweseka, nashindwa kula kabisa imefikia hatua kichwa kinauma upande mmoja naenda hospitali kupima nikidhani ni ugonjwa daktari akaniambia nina msongo wa mawazo(depression).

Nimejaribu sana kufanya uchunguzi kujua labda huyu mwenza wangu kapata mtu mwingine, kwa uchunguzi wa awali kwenye simu yake kwa siri sijapata baya lolote na kwa nje hivi pia sijasikia lolote. Nimehama hadi mazingira niliyokua naishi naye lakini wapi, hali inazidi kuwa mbaya kiupande wangu!

Kichwa hakiachi kuniuma, nashindwa kula, kulala, yaani kuna muda natamani kuwa kama watu wengine wenye furaha ila kwangu ni tofauti. Nimejaribu kubadili mazingira, kukaa na watu lakini haijasaidia, nimepiga magoti nimeomba mno lakini wapi!

Sitegemei mtu anihukumu, ila kiukweli nilipofikia nimesikia mengi kuhusu mambo ya wataalamu (mafundi) au waganga wa kienyeji, kama kuna mtu ambaye aliwahi kusaidiwa au anamfahamu mtu aliyewahi kusaidiwa jamani anisaidie PM au kwenye maoni mimi ntamfata PM kwa taarifa zaidi, maana natamani hadi kufa wakuu!

Haya mambo yapo na hayajaanza jana wala leo, jamani namuhitaji sana bado mpenzi wangu. Nashindwa hata kuendesha vizuri shughuli zangu za kila siku sababu ya maumivu niliyonayo moyoni. Mwenye msaada anisaidie, natamani arudi tena kwangu maisha yaendelee kama kawaida.

Nawaombeni sana.[emoji1431][emoji24]

 
kamloge tu ila dawa ikiisha ujiandae kwa maumivu ya moyo maana lazima akuache 😛

Atleast roho yangu itulie kwa sasa hvi maana hali nnayopoitia ni ngumu
 
Mkuu ina maana kwa uchunguzi wako hujajua hata kijisababu kidogo kinaweza kuwa nini??
 
Dada,pole Sana..ila nakushauri ukubaliane na Hali... Itachukua muda but utapita. Achana na Mambo ya waganga, Mapenzi hua yanaisha japo ningumu but utapata Mwingine

Najua saiv unawaza utampata wapi but jipe muda fanya Mambo yako tu.. concentrate kwenye vitu vingine kabisa. With time utasahau

Pole Sana dear

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mimi ni ke dada ningekua na hizo nguvu za chapa nipote hivi mbona ningepumua! Sisi ndio wale mabozozo tukipenda tumependa
 
Mkuu ina maana kwa uchunguzi wako hujajua hata kijisababu kidogo kinaweza kuwa nini??

Alinikwaza na mimi nilimkwaza ila hazikua sababu zenye mashiko kabisaa kufikia huku na kiupande wangu niliomba msamaha kwa pale nilipokosea tena mapema kabisa baada ya kuona nimemkosea...akawa km amekubali mara aniambie tuachane kuna siku akainsist sana nimuache nikajibu kiunyongr tu sawa maana sikua na jinsi baada ya siku mbili akanitafuta kutaka yaishe na alikosea nikamwambia its okay yameisha....ila tena ghafla hata siku mbili hazijapita ananiambia anaona bora aniache yaani inshort yupo km psycho kuna muda anakua sawa kuna muda anazingua mwisho wa siku ikafikia hapokei cm wala hajibu txts
 
mkuu hapo siyo dawa tena ya kumrudisha bali huwa ni dawa ya kumtuliza,wanawake huwa wanakumbwa na mambo mengi sana hasa mapepo na mavitu mabaya hasa ule mda ambao wanakuwa hedhi,ambao naweza kusema milango ya mapepo kuingia inakuwa iko wazi sana ndo sababu kubwa hasa kwa mapepo kuwa kwa wingi sana kuwa kwa wanawake na siyo wanaume,
2,dawa ya kumrudisha mpenzi pia wapo watu wanazo ila hizo huwa zaidi zinafanywa hasa kipindi kile mwenzako yuko mbali may be china kimasomo but unakuwa humuelewi basi ikifanywa hyo dawa ndani ya muda mfupi anaweza kudandia hata ndege ilimradi tu arudi kwako
Kama huyo ni mke wako ningekusaidia mtu,ukaenda kabisa nyumbani kwake na hela ya huduma unamlipa baada ya kufanikiwa hutoi sent,sema kam siyo mkeo hawez kukubali katu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…