Dawa ya kutokomeza migogoro inayotokea hapa Afrika hususani ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara

Dawa ya kutokomeza migogoro inayotokea hapa Afrika hususani ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara

Dede 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
1,182
Reaction score
2,248
Habari wakuu!

Kutokana na migogoro ambayo haiishi hapa katika nchi zetu za Afrika hususani kusini mwa jangwa la Sahara napendekeza baadhi ya mambo ambayo yatadumisha amani yetu.

1.Viongozi wa Africa waungane na wamalize tofauti zao zisio na tija kama tunavyoona baina ya Kagame na Tshisekedi. Hii ndo njia pekee itakayolinda Afrika yetu dhidi ya mabepari.

2. Sisi kama waafrika tujenge silaha zetu wenyewe zinazoendana na teknolojia ya sasa tuachane na ma AK 47 na Mabazuka. Serikali yetu ikishirikiana na EAC au SADC ianzishe kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kisasa kama missiles, hypersonic weapons, jets za kisasa na ikiwezekana hata nuclear weapons na submarines. Hii ndo njia utakayotusaidia kulinda mipaka yetu dhidi ya mabepari endapo WW3 ikitokea.

3. Nchi za Afrika zisaidiane katika masuala ya kiintellijensia, hii itasaidia kutuliza na kuzuia mashambulizi ya kigaidi yanayoweza kutokea barani kwetu.

4. Nchi za kiAfrika ziachane na habari za misaada mabepari wanatumia misaada hii kuchukua rasilimali zetu. Haiwezekani karne hii ya 21 bado tunaomba vyandarua na tunaagiza dawa kutoka nje.

5. Hii inaenda kwa viongozi moja kwa moja, waache tamaa waangalie maslahi ya wananchi wao.

Yangu ni hayo tu ila kiwanda cha silaha za kisasa hapa Afrika ni muhimu.
 
Badala ya viwanda vya dawa na tafiti za matibabu ili kuokoa uhai wewe unapendekeza kiwanda cha silaha za kuangamiza uhai!
 
Sahau kuhusu hilo kwa hawa viongozi wa bara hili.
Hapa beberu kuwapandisha kwenye bus moja ila wakirudi Afrika wao ni Mungu mtu.
Screenshot_20250203-132315.jpg
 
Badala ya viwanda vya dawa na tafiti za matibabu ili kuokoa uhai wewe unapendekeza kiwanda cha silaha za kuangamiza uhai!
Hivi unafikiri tukivamiwa hizo dawa ndo zitatusaidia? Au unafikiri magaidi wanaangamizwa kwa dawa peke yake? Tujenge viwanda vya dawa lakini tuunde na taasisi za kutengeneza vifaa vya kisasa tuachane na kuagiza silaha nje.
 
Back
Top Bottom