Wana Jf naomben mnisaidie ni dawa gani ya kuua magugu na majani kwenye mpunga bila kuleta madhara kwenye zao? Na kuna majani aina ya NDAGO majani haya huwa yanakuwa na mafundo kwa chini kama vitunguu, yananisumbua sana nini dawa yake maana yameota pamoja na mpunga. Mnisaidie wataalamu.
Tumia 2.4D inasomeka two four D
Hiyo kwaajili ya matembele. Tafuta stomp ya njano
Nakumbushia tena mnisaidie dawa ya Ndago.
khali mkuu,
mwonekano wa ndago ukoje, jani jembamba refu na mistari ya moja kwa moja kama nyasi/mahindi (monocotiledon) au pana na mistari iliyotapakaa kama mkunde au boga (dicotiledon).
Teknolojia hubadilika kila siku, kwa uchache wa nikifahamucho kama mmea (mpunga) na gugu (ndago) vyote ni monocotiledon unaweza kudhibiti gugu kwa dawa muda mchache kabla mpunga haujaota unaweza tumia Atrazine au dawa nyingine inayofanana. Mmea ukishaota dawa inatumika kudhibiti gugu la jamii tofauti na mmea k.m. Mono-cot vs Di-cot. Kwa uhusika wa mpunga jani la jamii ya mboga unaweza kulidhibiti na 2,4,D.Ndago ni monocotiledon.
Nakumbushia tena mnisaidie dawa ya Ndago.
Teknolojia hubadilika kila siku, kwa uchache wa nikifahamucho kama mmea (mpunga) na gugu (ndago) vyote ni monocotiledon unaweza kudhibiti gugu kwa dawa muda mchache kabla mpunga haujaota unaweza tumia Atrazine au dawa nyingine inayofanana. Mmea ukishaota dawa inatumika kudhibiti gugu la jamii tofauti na mmea k.m. Mono-cot vs Di-cot. Kwa uhusika wa mpunga jani la jamii ya mboga unaweza kulidhibiti na 2,4,D.
Salaam.
mkuu pamoja na kuwa ndago (Cyperus rotundus) ni monoxot lakini leaf venation yake sio parrarel kama monocots zingine (graminiae) ndago ina netes leaf vevetio ndio maana inateketea kwa 2 ,4 D Amine