Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Duuh nielekeze bas jinsi ya kupunguza makali na kero ya haya makitu
Chemsha maji halafu yaweke kwenye beseni au kisadolini.
Chukua Vicks, weka kwenye kijiko cha chai halafu ichanganye na hayo maji ya moto.
Chukua taulo, inamisha kichwa kwenye hilo beseni, vuta huo mvuke wa maji na Vicks huku ukiwa umefunika kichwa na taulo.
Fanya hivyo kama mara tano na ukimaliza jikandie hayo hayo maji. Jikande kifuani, shingoni, usoni, na kwenye pua.
Ukimaliza hayo tafuna karafuu halafu lala. Pia, kunywa supu yoyote ile ila iwe ya moto.
Ukiamka halafu hayo mafua bado yawe yanakusumbua sana nambie nikupe mbinu nyingine.
Kama nilivyokwambia hapo awali, mafua hayana tiba kabisa.
Huwa yanaisha yenyewe tu. Lakini zipo dawa na mbinu ambazo zinaweza kukupa nafuu ya muda.