1)Yawezekana una alergy na kitu jaribu kujichunguza mazingira yako labda vumbi au manyoya ya wanyama unaofuga. Au chakula fulani
2) Yawezekana ni infection tu na ikipata dawa itaisha
3) Wahi kwa daktari ila kinga ya kwanza ni kutathmini mazingira yako na chakula kabla ya kuanza kumeza dawa:
Dawa nzuri ya mafua ni kujifukiza kwenye mvuke wenye vicks : yani weka beseni la maji moto weka kijiko cha chai cha viks koroga kisha jifunike na taulo ukiinamia kiasi kwenye beseni uwe unavuta huo mvuke for 5-10 minutes. Pia penda kunywa maji yenye tangawizi na limao na asali kwa mbali. Kama unaweza pia chemsha supu ya mboga mboga (Vitunguu, Karoti, celery, mint) kishwa kunywa ikiwa moto .
Lastly: Fanya mazoezi : mara nyingi ukiuweka mwili katika hali ya joto yani ufanye zoezi la kukutoa jasho mafua hupungua sana , ukilala tu na kujilegeza basi kamwe hayaishi.
Get well Soon