Dawa ya muwasho

Pole,

Kwa jinsi ya mgawanyo wa muwasho huu, inaelekea zaidi kwenye Scabies.

Hii hutokea pale unapopata mgeni mwenye shida husika, mwanafamilia aliyeenda kwenye shughuli kama msiba au harusi na kurudi. Kwa sasa ni tatizo zaisi kwa watoto wa shule walioko boarding na bodaboda. Mambo huwa magumu zaidi usiku.

Pamoja na dawa za muwasho(Cetirizine mg10 kwa siku au Loratadine mg10 kwa siku) pamoja na hayo matumizi ya Prednisolone yanahitaji umakini sana hasa kwa mtu mwenye shida ya sukari, ni vyema kuzingatia.

Mambo mengine muhimu ni:

1: Paka dawa ya BBE mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 7

2: Fua nguo zako zote ulizot7mia tangu muwasho uanze pamoja na shuka na kuzipitisha kwenye maji moto.

3: Fanya famigation kwa kupiga dawa kwenye kuta, sakafu na chaga za vitanda.

NB: Dawa ya famigation utapata kwa wauza dawa za mifugo. Ni dawa ambazo hutumika kuosha mifugo ili kuua kupe kweny mifugo, watakueleza jinsi ya kuchanganya.
 
Yeah itakusaidia mara moja kwa wiki ila paka.na calamine lotion pia itakusaidia na hautakiwi ugusane na mtu Sasaivi physically kiswahili tunaita UKURUTU pia tafuta sabuni nzuri yakuogea kwa afya nzuri ya ngozi yako
 
Hizo ni scabbies,
Vipele vinatokea sehem ya mikunjo?
Na je viko mikonon kwenye katikati ya vidole? Na mapajan vipo?
Kama ndio jibu nikupe dawa maana nilikuw na uginjwa wa hvo nilipew dawa nimepona,
Umenisumbua mda mrefu sana
 
Hizo ni scabbies,
Vipele vinatokea sehem ya mikunjo?
Na je viko mikonon kwenye katikati ya vidole? Na mapajan vipo?
Kama ndio jibu nikupe dawa maana nilikuw na uginjwa wa hvo nilipew dawa nimepona,
Umenisumbua mda mrefu sana
Toa dawa mkuu
 
Toa dawa mkuu
Dawa yake anunue scabona cream, inauzwa elfu sita
Pia atumie dawa ya vidonge inaitwa IVERMECTRIN hyo dawa inatolew kwa uzito wa kg, kwa mg
Hyo dawa inaua vimelea vyote, inategemea daktar atakuandikia dozi ya sku ngap kulingana na uzito wako,

Nenda pharmacy tu kubwa yeyote, unapata,
Mimi niliandikiwa vidinge vinne kwa siku moja
Nimepona kabisa,
 
Tumia BBE, bei yake haizidi elfu tatu; oga jipake asubuhi na jioni kwa siku 7 (1 x 2 x 7) tatizo litaisha.
 
CETRIZINE, Dawa hii ni nzuri sana kukusaidia kama una tatizo la kujikuna kwenye ngozi kutokana na allergy ya matumizi ya vitu mbali mbali
Hilo tatizo la jamaa lilishanipata niliteseka nilikuwa silali usku, nashindwa kutulia ofsini ..hiyo cetrizine nilitumia ila ni takataka haisaidii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…