Dawa ya muwasho

Dawa ya muwasho

Pole sana mkuu, niliwahi kupatwa na tatizo hilo niliteseka zaidi ya miezi 7 ndo nikapona.

Nilichofanya mimi niligeukia upande wa tiba ya kienyeji kuna dada mmoja nilikutana nae akaniambia kwao tanga kuna majani fulan unayasaga kisha unachanganya na mafuta ya nazi unakuwa unapaka ukioga ndo nikapona.

Niliteseka sana nilikua silali usiku,kazini nashindwa kabisa kukaa na nikiwa hom navaa taulo tu maana nguo zangu nilikua siziamini tena..

Nilihama mpaka chumba nacholala nikasusia nguo zote na kila kitu ila wapi, kiufupi niliteseka.

Ushauri jaribu kwanza kwenda hosptal yenye madktari maalumu wa ngozi .
 
Habari ndugu
Nasumbuliwa na muwasho mikononi, tumboni,mapajani,nyuma ya goti, sehemu za siri,makwapani na sehemu za viungio nilikuwa na mba nimetumia dawa ya mba mba umeisha ila bado muwasho upo nikijikuna sana hutokea vipele na baada ya muda hukauka na kupona
Sasa nikijikuna sana ngozi inatoa kama vumbi vumbi
Hata sehemu za siri huota pia na kupona ukijikuna huja tena kende kuwa gumu na kuota gamba
Nimebadili nguo mara kwa mara na kujitahidi kuwa msafi
Naomba msaada naweza kutumia dawa gani nikapona muwasho
ushapona kaka
 
Back
Top Bottom