Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni janga la kitaifa kwenye kaya zetu linazozidi kuongezeka.
Upungufu wa nguvu za kiume ni kero kubwa kwa zaidi ya 50% ya wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40 na 70% kwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60.
Upungufu wa nguvu za kiume unasababisha karaha, majuto, masikitiko, manung'uniko na huzuni kubwa kwa wanaume wenye tatizo hili. Hii inatokana na kuwa wanaume wenye tatizo hili huingiwa na woga na wasiwasi wa kudumu kutokana na kuhofia kushindwa tena kwa mara nyingine kutimiza matarajio ya wapenzi na wake zao mara watakapokutana kimwili. Hofu na wasiwasi huu utasababisha mwanaume ashindwe kabla ya kuanza tendo lenyewe. Waganga wa kienyeji na tiba mbadala nao wanatumia fursa hii kuwadanganya waathirika ili kujipatia chochote kitu mifukoni.
Chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo hasa cha uhanithi ni ukosefu wa damu ya kutosha inayopelekwa kwenye uume wakati wa kutaka kujamiana. Damu ya kutosha inahitajika kupelekwa kwa wingi kwenye uume ili kuijaza misuli ya uume na kusababisha kiungo hiki kisimame, kinyooke na kiongezeke unene. Kama damu haitapelekwa ya kutosha huko itasababisha uume usisimane na kusababisha kilio kwa mwanaume na hata mwanamke aliyejiweka tayari kisaikologia kupata burudani ya sex.
Sababu zinazosababisha damu isiende kwenye uume ziko nyingi, lakini za muhimu sana ni hizi zifuatazo:
1. Kuwa na msongo mkubwa wa mawazo, wasiwasi na hofu wakati wa kutaka kujamiana kunakotokana na masuala ya kikazi, kifamilia, kijamii au sababu nyingine.
2. Kuwa na maumivu makali sehemu yoyote au kuwa mgonjwa (homa, n.k)
3. Uchovu mwingi na njaa
3. Kuwa mnene kupita kiasi
4. Kuwa na shinikizo kubwa la damu (BP) au shinikizo dogo (low blood pressure)
6. Ugonjwa wa kisukari, moyo na mafigo
7. Kutumia baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya pressure, kisukari, allergy, akili, kupunguza hamu ya kula, na vidonda vya tumbo
8. Uvutaji sigara
9. Kunywa pombe kupita kiasi
Namna ya kuzuia na kutibu uhanithi:
1. Fanya mazoezi kila mara
2. Punguza mawazo (maliza tatizo, pata ushauri, tafuta msaada)
3. Punguza unene wako (angalia vyakula na ulaji wako, mazoezi)
4. pata muda wa kupunzika
5. Mwanamke mpe moyo mwaume anaposhindwa (usimbeze na kumdhalilisha, mpe moyo)
6. Kula vyakula vya asili (muhogo, asali, mtama, ulezi, viazi, n.k)
7. Punguza kula chumvi nyingi na mafuta mengi
8. Kula matunda maarufu yanayoongeza mzunguuko wa damu kwenye penis kama vile mabarungi (grapefruits), nanasi, matikiti maji, mapera, ndizi, strawberries, Kiwi na karanga. Kiwi na Karanga vinaongeza arginine inayozalisha nitric oxide mwilini inayosaidia kutanuka kwa mishipa ya damu na kushusha pressure, hivyo kuongeza usambazaji wa damu kwenye misuli ya uume itakayosaidia penis kusimama.
9. Acha kutumia viagra zina madhara makubwa na zitakusaidia kwa muda mfupi sana tu.
10. Mwambie dk. wako akuandikie dawa za kutibu kisukari na pressure zisizopunguza nguvu za kiume
11. Pateni pamoja ushauri kwa daktari wewe na mpenzi wako pamoja, msilaumiane.
FANYA MAZOEZI, PUNGUZA OBESITY, NA ONDOA MAWAZO KICHWANI