TONY MTAKAYOTE
Senior Member
- Jan 24, 2013
- 150
- 69
Je, Umewahi kujiuliza, kwa nini baadhi ya familia watoto wanakuwa na maadili mema, huku nyingine wakiwa na tabia mbaya?
Jibu lipo wazi, Binadamu unaweza kuandaa aina ya mtu/mtoto unayemtaka, kwa kuandaa mfumo wa mitazamo na fikra kulingana na tabia unayotaka awe nayo na kuzilisha kwenye ufahamu/akili yake. Mfumo huo utaendesha matendo yake yote, kuanzia namna ya kuongea, kutembea na kila kinachohusu tabia.
Hivyo basi mafisadi wote tulionao katika nchi ya Tanzania na duniani kote, wametengenezwa kwa namna hiyo, iwe kwa kutambua ama kwa kutokutambua, Kadhalika waadilifu.
Mfumo wa Mitazamo na fikra huingizwa katika ufahamu/akili ya binadamu kwa njia kuu mbili:
1. Kwa kusikiaJibu lipo wazi, Binadamu unaweza kuandaa aina ya mtu/mtoto unayemtaka, kwa kuandaa mfumo wa mitazamo na fikra kulingana na tabia unayotaka awe nayo na kuzilisha kwenye ufahamu/akili yake. Mfumo huo utaendesha matendo yake yote, kuanzia namna ya kuongea, kutembea na kila kinachohusu tabia.
Hivyo basi mafisadi wote tulionao katika nchi ya Tanzania na duniani kote, wametengenezwa kwa namna hiyo, iwe kwa kutambua ama kwa kutokutambua, Kadhalika waadilifu.
Mfumo wa Mitazamo na fikra huingizwa katika ufahamu/akili ya binadamu kwa njia kuu mbili:
2. Kwa kuona
Fisadi wa sasa hajatokea tu ghafla, bali aliandaliwa kwa muda mrefu aidha na jamii yake au na wazazi wake. Ufisadi ni matokeo ya mfumo wa mitazamo na fikra za ubinafsi, wizi na kutokuwajibika aliolishwa mtu kwenye ufahamu/akili yake kutoka kwenye jamii inayomzunguka au familia, kupitia kusikia au kuona.
Wengi wetu tumejikuta tukilaumu na kulalamika juu ya baadhi ya viongozi mafisadi wa serikali, pasipo kuzingatia ya kuwa viongozi hao wametoka katika jamii yetu, ni ndugu zetu, hawajatoka nje ya nchi.

NAMNA MAFISADI WALIVYOTENGENEZWA:
Mafisadi walitengenezwa kwa namna kuu tatu;
(a) Mafisadi waliotengenezwa utotoni.
Wakati mtoto anazaliwa akili yake haikuwa na kitu chochote, ilikuwa tayari kwa ajili ya kulishwa fikra, mitazamo na maarifa ya namna yeyote, mema au mabaya. Akili ya mtoto ilianza kulishwa mfumo wa mitazamo na fikra za kwamba chochote anachohitaji lazima akipate. Sambamba na hili mtoto huyu alikuwa na majivuno, ulafi na uchoyo. Wazazi hawakujisumbua kumkemea juu ya tabia hizi, pasipo kujua ya kwamba wanadumisha/kulea roho ya ubinafsi ndani yake, ambayo ndiyo mzizi mkuu wa ufisadi. Walidhani, kutokumkemea ni kumwonyesha upendo. Katika jamii yake wezi hawakupewa adhabu, hivyo kumjengea fikra nyingine ya kwamba, “ukiiba hapewi adhabu yeyote, na mali inabaki kuwa yako”. Na hapo uzalishaji wa Fisadi ukawa umekamilika.
(b) Fisadi aliyetengenezwa ukubwani
Kipindi fisadi huyu akiwa mtoto, akili yake ililishwa mfumo wa mitazamo na fikra nzuri ambazo zilimfanya awe mtu mwema na mwenye maadili katika jamii. Lakini Kutokana na Wezi na mafisadi kutokuwajibishwa katika jamii yake, ilimjengea mtazamo na fikra za kutokuwepo madhara yeyote endapo akiiba au kufanya hujuma ya namna yeyote katika jamii yake. Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana la jamii, na mtu huyu akawa ametengemaa na kukomaa kama fisadi zao la jamii. Kwa hiyo jamii ilihusika moja kwa moja kumtengeneza fisadi huyu.
(c) Fisadi aliyetengenezwa wakati wa uongozi.
Hapo kabla, mtu huyu alikuwa mwadilifu. Lakini, baada ya kuingia kwenye mifumo ya uongozi, akili yake ililishwa mfumo wa mitazamo na fikra mbaya juu ya mali za umma. Viongozi katika ofisi yake walikuwa ni wezi, mamlaka haikuwahi kuwachukulia hatua, japokuwa walitiwa hatiani kwa wizi wa mali za umma. Kwa kuona hayo, Naye alianza rasmi kuiba mali za Umma, kwa sababu hakuna adhabu. Hapo mfumo ulitengeneza fisadi.
Idadi ya Mafisadi waliotengenezwa kwa njia (b) na (c) ni wengi sana kuliko waliotengenezwa kwa njia (a). Mafisadi hawa wamekomaa kwa sababu katika maisha yao hawajawahi kuona fisadi akiwajibishwa, hivyo kuuona ufisadi na wizi kama kitu cha kawaida kisicho na madhara na chenye faida kubwa sana kwa muda mfupi. Fikiria, ikiwa mafisadi wa miaka ya nyuma wangeuawa hadharani au kuchomwa moto au kupewa adhabu nyingine yeyote kali, unadhani leo tungekuwa na mafisadi?
Chimbuko la matatizo haya yote ni uwepo wa jamii isiyojali juu ya mustakabali wa taifa na vizazi vijavyo. Kutokujali kwa wananchi hupelekea ubinafsi wa hali ya juu sana na kuwapa viongozi ujasiri wa kutumia au kuiba mali za umma bila wasiwasi wowote.

NAMNA YA KUONDOA UFISADI:
Mtazamo na fikra ndicho kinachoongoza matendo ya binadamu. Ubinafsi unatokana na mfumo mbaya wa fikra anazofundishwa mtu kwa kuona au kusikia. Na ubinafsi ndiyo chanzo kikuu cha ufisadi. Jamii ijikite Zaidi katika kubadili na kuboresha mitazamo na fikra za wananchi, iwafundishe juu ya umuhimu wa umoja, ushirikiano na upendo.
Njia zifuatazo zitaondoa kabisa tatizo la ufisadi katika nchi yetu:
(1.) Kuandaliwe somo la maadili mema litakaloratibiwa kitaalamu na wanasaikolojia liweze kubadilisha “mindset” ya watoto/vijana/wananchi iweze kuelekea kwenye kutokuwa wabinafsi na mafisadi. Watoto wote wafundishwe kuanzia wakiwa na umri mdogo, na liendelee kufundishwa katika madarasa yote hadi chuo kikuu. Hii itasaidia kupandikiza mfumo wa mitazamo na fikra za maadili mema katika akili zao. Imani ndiyo kiongozi cha matendo yote ya mtu, ukiweza kudhibiti jinsi mtoto anavyoamini na kufikiri ni rahisi Zaidi kuibadili tabia yake. Tukifaulu katika hili ndiyo tutaweza kupata waadilifu na wawajibikaji, wenye kuipenda nchi yao. Na kwa kufanya hivyo ufisadi utabaki kuwa historia katika nchi ya Tanzania.
(2.) Adhabu kali zitolewe kwa wale wote watakaopatikana na hatia ya wizi na ufisadi. Hili litaleta hofu na hivyo kuingiza mfumo wa mitazamo na fikra mpya katika akili za wananchi na viongozi za kuuona wizi na ufisadi kuwa kitu kibaya. Tusiwaache kusubiri hukumu ya Mungu, tuanze nao hapahapa duniani kwanza. Fikra za watoto na vijana zimeharibiwa na jamii kwa kutokuwachukulia hatua wezi na mafisadi. Sheria ipitishe Adhabu kali ikiwezekana kunyongwa hadi kufa hadharani, kwa wale wote watakaotiwa hatiani kwa kosa la kufanya ufisadi na wizi wa mali za umma. Hii itawajengea watoto na vijana fikra na mtazamo mpya juu ya ubaya wa ufisadi.

HITIMISHO:
Kupitia andiko hili, ni ombi langu kwa mamlaka na jamii, kuyachunguza maoni haya kwa umakini, endapo yatathibitika kuwa ni yenye tija kwa mustakabali mzuri wa taifa, basi yafanyiwe kazi mara moja.
Mungu awabariki sana.
Upvote
2