Dawa za Corona: Bupeji na Covido za Magufuli zinapatikana wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana kwa mujibu wa Rais wetu mpendwa Dr. Magufuli dawa za Corona hazipo huko nje tu.

Amenukuliwa Dr. Magufuli akisema, "Tanzania ina dawa nyingi za kutibu Corona." Ameendelea zaidi kwa kusema, "katika dawa hizo tuna Covido na Bupeji ambazo zina uwezo wa kutibu Corona kwa kiwango cha 99.99999%.

Tufahamishane jamani ni wapi dawa hizi hasa hii ya "Bupeji" zinapatikana wapi?

Ninawasilisha.
 
Nipo hapa kwenye dozi ya bupeji, huku nikisukumia na ile ya Dr. Gwajima!

Hongera Sana awamu ya tano kuturejesha edeni ya mababu zetu!

Kupigana vita na pharmaceutical empire kunataka moyo, japo corona imewafanya wao kwa wao wapigane vita.
 
Nimeipenda hii "Bupeji."

Je ni made in Chatto?
Ofisi zipo gambosh avenue jjrani na ilipokuwa PPF TOWER

turudi kwenye mada ni vyema tukajivunia vya kwetu ikiwa vitatusaidia hongera kwa watengenezaji wa hizo dawa
 
NIMR CAF
Nenda Mabibo External Walipo TMDA Ni Majirani
Dodoma Unawapata Benjamin Mkapa Hospital
Muhimbili National Hospital Nao Wana Dawa Yao
Fika Kitengo Cha Tiba Asili
Tanzania Tupo Salama
 
Asante kwa taarifa.

Hatuna order zozote japo za "Bupeji" tokea hata kwa majirani zetu? Japo tuseme mabeberu wanatuonea gere kujifanya hawaitaki huku wanaitaka?

Vipi na wale wenzetu wa Madagascar? Mh. Kabudi hajawakumbuka japo kwa dozi chache?

Walitufaaga hao wakati wa dhiki!
 
Mkuu
Wakimudu Kuitosheleza Nchi Nzima Ndiyo Tutawakumbuka Majirani Hata Hao Wakoloni
 
Tafadhali.., ebu ngoja kwanza....., Kwahio kuna dawa inayotibu virus.., sio kuongeza / kuimarisha kinga bali inatibu ?.., Haya tuyaache hayo..., nashukuru kuna hio dawa, sasa je hio dawa imepimwa kwa watu wangapi kujua ufanisi wakati hata Covid hatuna nchini ?
 
Mkuu jamaa ni muongo wa kutupa. Hizi dawa za kutibu corona zimethibitishwa na WHO kama zinatibu corona au ni mambo ya KUKURUPUKA!?
Mabibi na mabwana kwa mujibu wa Rais wetu mpendwa Dr. Magufuli dawa za Corona hazipo huko nje tu...
 
Mkuu jamaa ni muongo wa kutupa. Hizi dawa za kutibu corona zimethibitishwa na WHO kama zinatibu corona au ni mambo ya KUKURUPUKA!?
WHO wasiposema basi haitibu. Aisee
 
Asante kwa taarifa.

Hatuna order zozote japo za "Bupeji" tokea hata kwa majirani zetu? Japo tuseme mabeberu wanatuonea gere kujifanya hawaitaki huku wanaitaka?

Vipi na wale wenzetu wa Madagascar? Mh. Kabudi hajawakumbuka japo kwa dozi chache?

Walitufaaga hao wakati wa dhiki!
Ile ya madagascar iliwafaa zaidi pale chatoni ingawa mzee wa jalalani alipiga funda za kutosha palepale kabla haijapanda ndege...
 
Sasa kama inatibu kwanini WHO wasiithibitishe ili Tanzania ikatengeneza kwa wingi na hivyo kuiuza kwa nchi mbali mbali duniani na kujiingizia $$$ in trillions!!!! Think outside the box!!
Achana nae mkuu yeye anafikiri kichama zaidi akiimba na kusifu kila neno litokalo kwa mtukufu wa chattle
 
Mabibi na mabwana kwa mujibu wa Rais wetu mpendwa Dr. Magufuli dawa za Corona hazipo huko nje tu.

Amenukuliwa Dr. Magufuli akisema, "Tanzania ina dawa nyingi za kutibu Corona." Ameendelea zaidi kwa kusema, "katika dawa hizo tuna Covido na Bupeji ambazo zina uwezo wa kutibu Corona kwa kiwango cha 99.99999%.

Tufahamishane jamani ni wapi dawa hizi hasa hii ya "Bupeji" zinapatikana wapi?

Ninawasilisha.
Kwa Dawa ya Bupeji, mgunduzi wa dawa hiyo anapatikana ofisi za SIDO Upanga au unaweza kumpata kwa namba ya simu 0754 343478. Binafsi nina ushuhuda wa watu ambao washawai tumia hii dawa ikawasaidia.
 
Asante kwa taarifa.

Hatuna order zozote japo za "Bupeji" tokea hata kwa majirani zetu? Japo tuseme mabeberu wanatuonea gere kujifanya hawaitaki huku wanaitaka?

Vipi na wale wenzetu wa Madagascar? Mh. Kabudi hajawakumbuka japo kwa dozi chache?

Walitufaaga hao wakati wa dhiki!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom