Watu wanachanganya sana kati ya Anabolic steroids na Whey protein (aka PODA). Hivi ni vitu viwili tofauti aisee.
Anabolic steroids ni synthetic steroidal hormones ni kama artificial testosterone hormone . Hupatikana katika mfumo wa vidonge (pills, Solution kwa ajili kuchoma sindano kwenye misuli, na pia Gel kwa ajili ya kupaka kwenye misuli. Utumiaji wa Anabolic steroids kwa kiwango kikubwa ili kuongeza ukubwa wa misuli ni hatari kwa afya. Maana hupelekea kutanuka kwa moyo, kuharibu ini, kupelekea mabadiliko makubwa ya kiwango cha cholesterol mwilini, kupungua kwa ukubwa wa korodani (kusinyaa), kuepelekea conditions kama gynoecomastia,uchizi (mania) ,hupelekea mtumiaji kuwa na aggressive behaviours hivyo anaweza kudhuru au kujidhuru mwenyewe , upara (baldness) n.k
Hii hapa chini ni picha ya steroids
View attachment 2570999
Wakati Whey protein (Poda) ni dietery supplement inayotumika kuongeza kiwango cha protein mwilini kama vile ilivyo kwa glucose powder inatumika kuongeza kiwango cha glucose mwilini. Whey protein haina madhara mwilini na hutumika duniani kote kwani husaidia kupunguza muda wa misuli kupona mara baada ya mazoezi makali, hupunguza majeraha yanayoweza kutokana na upungufu wa protein mwilini, na pia husaidia kujenga misuli. Ikumbukwe kuwa upungufu wa protein mwilini kwa mtu anayebeba vitu vizito au kufanya mazoezi mazito hupelekea kupunguza uwiano wa kiwango cha nitrogen mwilini ambao hupelekea kusababisha Protein catabolism ( kuvunjwavunjwa kwa protein) hivyo kupelekea kupungua kwa ukubwa wa misuli yaani mwili haujai na badala yake unadumaa, hupelekea pia misuli kuchukua muda mrefu kupoa, inaongea uwezekano wa mfanyaji mazoezi kupata majeraha wakati anafanya mazoezi mazito.
Ukitaka kuona jinsi protein catabolism inavyoathiri mwili waangalie makuli (wabeba mizigo mizito) masokoni, utaona mtu anabeba magunia ya kilo 150 daily ila mwili haujai (umedumaa), ila utaona mtu anabeba chuma cha kilo 60 au 70 tu gym mwili unajaa. Hii inatokana na msosi...unafanya kazi nyingi ila protein unayokula ni ndogo, mwili unaanza kutafuna misuli.
Hii hapa chini ndio picha ya Whey protein (maarufu hapa kwetu kama PODA)
View attachment 2571025