Dawa za kuongeza akili zaingia nchini

Dawa za kuongeza akili zaingia nchini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
akili.jpg

KWA UFUPI
Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.

Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.

Dawa hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye vyakula vya kila siku, zina uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa mwanafunzi au mfanyakazi.

Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ'.

Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka.

"Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda katika mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu," anasema Haule na kuongeza: "Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali."

Haule ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea anasema kwamba mtindo wa maisha na vyakula vinavyoliwa na watu mara kwa mara kwa sasa huufanya mwili kuhifadhi sumu nyingi mwilini.

Anasema kuwa dawa hizo pia zina uwezo kuondoa sumu mwilini na kuufanya mwili wa binadamu kurejesha rangi yake halisi na kumeng'enya vizuri chakula anachokula.

Haule anayefanya kazi pamoja na Shirika la Nativa linalotengeneza dawa hizo la nchini Afrika Kusini, anaeleza kuwa tangu kuingiza dawa hizo nchini watu wengi wamejitokeza kuzihitaji.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza anasema kuwa mamlaka hiyo inazitambua dawa hizo kama virutubisho vya chakula, zimesajiliwa na ni salama kwa binadamu.

"Tuna taarifa kuwa bidhaa za ‘Go Woman' na ‘Go Man' zimesajiliwa na ni salama," anasema.

Dawa nyingine zinazotengenezwa na kampuni hiyo zimetajwa kuwa na uwezo wa kuunda mifupa kwa watu wazima na majeraha ya wagonjwa wa kisukari. "Ni vigumu kwa watu wazima wenye miaka 50 na kuendelea kupona haraka wanapopata ajali, lakini hizi dawa zinaponya majeraha na kuunga haraka mfupa," anasema Haule.
Anasema kuwa kadri umri wa binadamu unavyoongezeka mwili wake unashindwa kuzalisha baadhi ya virutubisho vinavyoupa mwili uimara.

Dawa hizo zina mchanganyiko wa madini, vitamin, viondoa sumu pamoja na dawa za mitishamba.

Virutubisho vya chakula kwa kawaida hupungua ubora wake kwa sababu ya udongo, mionzi au kuweka vyakula hivyo katika majokofu.

Mambo mengine yanayofanya virutubisho vya chakula visifanye kazi yake sawasawa ni msongo wa mawazo na uchafu wa mazingira.

Ugonjwa wa kukosa raha na kusononeka kila wakati au sonona, pia unaweza kutibiwa kwa dawa hizo.

"Sonona inaua. Hata wataalamu wa afya wa nchi za Ulaya wamethibitisha, lakini dawa hii ina madini ya amino acidi ambayo hupatikana baada ya mtu kucheka," anasema.

Anabainisha kwamba dawa hizo zina vitamin maalumu zinazoweza kuongeza kinga ya mwili na kuondoa sumu mwilini.

"Zina vitamin a, c na e, madini ya zinki na selenium na zina uwezo wa kuongeza nguvu ya mwili," anasema.

Anadokeza kuwa kati ya dawa hizo, zipo pia dawa kwa ajili ya wanawake na wanaume pekee, zilizo na kazi maalumu.

Kwa mfano dawa ya wanawake ina uwezo wa kumsaidia mwanamke apate raha ya tendo la ndoa, inarutubisha nywele zake na kuzifanya zikue kwa haraka.

Vilevile, dawa hiyo inasaidia kuimarisha ngozi ya mwili kwa kuondoa sumu mwilini. "Hii dawa kwa ajili ya wanawake ina Vitamini maalumu za kukuza nywele kama ‘Omega3 na Omega 6,'" anasema Haule.
Kwa upande wa wanaume, dawa hiyo itawasaidia kuongeza uwezo wa tendo la ndoa, kuimarisha mifupa pamoja na viungo.

Dawa zote mbili, yaani ile ya wanawake na ya wanaume zina uwezo wa kuimarisha ubongo na kumbukumbu.

Haule anaongeza kuwa ipo dawa kwa ajili ya wanawake wenye tatizo la kutokwa damu kwa wingi kunakosababishwa na hedhi au maradhi mengine.

Hata hivyo, Dk John Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kuwa ni vigumu mtu kupata tiba ya akili akiwa tayari ni mtu mzima, kwani uwezo wa kiakili unajengwa kuanzia utotoni.

"Lakini suala hili linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kama hujafanya tafiti, huna haki ya kuzungumza," anasema Dk Semkuya.

Anasema ikiwa virutubisho hivyo vya chakula vitatumiwa tangu utotoni basi vinakuwa na manufaa zaidi kuliko kutumiwa ukubwani.

Wagonjwa wa Ukimwi

Miongoni mwa dawa hizo ipo dawa ya ‘Life Gain' mahususi kwa kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi.

Haule anasema kuwa kwa virutubisho vilivyo katika dawa hizo vina uwezo wa kupandisha kinga ya mwili kwa haraka, bila kumwathiri mgonjwa.

Mwananchi ilifanya mazungumzo na mwanamume mmoja mkazi wa Tandika (jina linahifadhiwa) anayeishi na VVU ambaye alitumia dawa ya Lifegain.

Mtu huyo alisema alikuwa hoi kwa maradhi, lakini baada ya kutumia dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili, alinyanyuka na sasa anaendelea na shughuli zake za kawaida. Haule anasema kampuni hiyo imefika baada ya kuona kuna upungufu mkubwa wa dawa zinazotumia virutubisho vya mimea huku watu wengi wakinywa dawa za kemikali.
"Dawa zenye kemikali zinasaidia, lakini zikitumika kwa muda mrefu huchosha ini, figo kwa sababu hutunza sumu," anasema Haule.

Haule anasema amerithi elimu hiyo ya tiba mbadala kutoka kwa babu yake, Mzee Fungafunga.

Anasema alijifunza tiba kwa kutumia mimea, kutoka kwa babu yake, ambaye licha ya kuwa alikuwa mhunzi, alitibu kwa njia ya mimea.

Haule anasema aliamua kujikita zaidi katika tiba asilia baada kukosa ushirikiano katika fani aliyosomea ya ufundi makanika.

chanzo. Dawa za kuongeza akili zaingia nchini - Kitaifa - mwananchi.co.tz

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

attachment.php

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.

attachment.php

Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.

attachment.php

MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.

NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.

KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Attachments

  • vyakula.jpg
    vyakula.jpg
    61.9 KB · Views: 2,547
  • eggs.jpg
    eggs.jpg
    15.5 KB · Views: 2,339
  • pilipili.jpg
    pilipili.jpg
    48.7 KB · Views: 2,303
VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

attachment.php

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.

attachment.php

Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.

attachment.php
8

MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc' ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.

NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene' chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.

KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Hapa nakubaliana na wewe
 
akili.jpg

KWA UFUPI
Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.

Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.

Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.

Dawa hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye vyakula vya kila siku, zina uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa mwanafunzi au mfanyakazi.

Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ'.

Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka.

"Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda katika mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu," anasema Haule na kuongeza: "Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali."

Haule ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea anasema kwamba mtindo wa maisha na vyakula vinavyoliwa na watu mara kwa mara kwa sasa huufanya mwili kuhifadhi sumu nyingi mwilini.

Anasema kuwa dawa hizo pia zina uwezo kuondoa sumu mwilini na kuufanya mwili wa binadamu kurejesha rangi yake halisi na kumeng'enya vizuri chakula anachokula.

Haule anayefanya kazi pamoja na Shirika la Nativa linalotengeneza dawa hizo la nchini Afrika Kusini, anaeleza kuwa tangu kuingiza dawa hizo nchini watu wengi wamejitokeza kuzihitaji.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza anasema kuwa mamlaka hiyo inazitambua dawa hizo kama virutubisho vya chakula, zimesajiliwa na ni salama kwa binadamu.

"Tuna taarifa kuwa bidhaa za ‘Go Woman' na ‘Go Man' zimesajiliwa na ni salama," anasema.

Dawa nyingine zinazotengenezwa na kampuni hiyo zimetajwa kuwa na uwezo wa kuunda mifupa kwa watu wazima na majeraha ya wagonjwa wa kisukari. "Ni vigumu kwa watu wazima wenye miaka 50 na kuendelea kupona haraka wanapopata ajali, lakini hizi dawa zinaponya majeraha na kuunga haraka mfupa," anasema Haule.
Anasema kuwa kadri umri wa binadamu unavyoongezeka mwili wake unashindwa kuzalisha baadhi ya virutubisho vinavyoupa mwili uimara.

Dawa hizo zina mchanganyiko wa madini, vitamin, viondoa sumu pamoja na dawa za mitishamba.

Virutubisho vya chakula kwa kawaida hupungua ubora wake kwa sababu ya udongo, mionzi au kuweka vyakula hivyo katika majokofu.

Mambo mengine yanayofanya virutubisho vya chakula visifanye kazi yake sawasawa ni msongo wa mawazo na uchafu wa mazingira.

Ugonjwa wa kukosa raha na kusononeka kila wakati au sonona, pia unaweza kutibiwa kwa dawa hizo.

"Sonona inaua. Hata wataalamu wa afya wa nchi za Ulaya wamethibitisha, lakini dawa hii ina madini ya amino acidi ambayo hupatikana baada ya mtu kucheka," anasema.

Anabainisha kwamba dawa hizo zina vitamin maalumu zinazoweza kuongeza kinga ya mwili na kuondoa sumu mwilini.

"Zina vitamin a, c na e, madini ya zinki na selenium na zina uwezo wa kuongeza nguvu ya mwili," anasema.

Anadokeza kuwa kati ya dawa hizo, zipo pia dawa kwa ajili ya wanawake na wanaume pekee, zilizo na kazi maalumu.

Kwa mfano dawa ya wanawake ina uwezo wa kumsaidia mwanamke apate raha ya tendo la ndoa, inarutubisha nywele zake na kuzifanya zikue kwa haraka.

Vilevile, dawa hiyo inasaidia kuimarisha ngozi ya mwili kwa kuondoa sumu mwilini. "Hii dawa kwa ajili ya wanawake ina Vitamini maalumu za kukuza nywele kama ‘Omega3 na Omega 6,'" anasema Haule.
Kwa upande wa wanaume, dawa hiyo itawasaidia kuongeza uwezo wa tendo la ndoa, kuimarisha mifupa pamoja na viungo.

Dawa zote mbili, yaani ile ya wanawake na ya wanaume zina uwezo wa kuimarisha ubongo na kumbukumbu.

Haule anaongeza kuwa ipo dawa kwa ajili ya wanawake wenye tatizo la kutokwa damu kwa wingi kunakosababishwa na hedhi au maradhi mengine.

Hata hivyo, Dk John Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kuwa ni vigumu mtu kupata tiba ya akili akiwa tayari ni mtu mzima, kwani uwezo wa kiakili unajengwa kuanzia utotoni.

"Lakini suala hili linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kama hujafanya tafiti, huna haki ya kuzungumza," anasema Dk Semkuya.

Anasema ikiwa virutubisho hivyo vya chakula vitatumiwa tangu utotoni basi vinakuwa na manufaa zaidi kuliko kutumiwa ukubwani.

Wagonjwa wa Ukimwi

Miongoni mwa dawa hizo ipo dawa ya ‘Life Gain' mahususi kwa kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi.

Haule anasema kuwa kwa virutubisho vilivyo katika dawa hizo vina uwezo wa kupandisha kinga ya mwili kwa haraka, bila kumwathiri mgonjwa.

Mwananchi ilifanya mazungumzo na mwanamume mmoja mkazi wa Tandika (jina linahifadhiwa) anayeishi na VVU ambaye alitumia dawa ya Lifegain.

Mtu huyo alisema alikuwa hoi kwa maradhi, lakini baada ya kutumia dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili, alinyanyuka na sasa anaendelea na shughuli zake za kawaida. Haule anasema kampuni hiyo imefika baada ya kuona kuna upungufu mkubwa wa dawa zinazotumia virutubisho vya mimea huku watu wengi wakinywa dawa za kemikali.
"Dawa zenye kemikali zinasaidia, lakini zikitumika kwa muda mrefu huchosha ini, figo kwa sababu hutunza sumu," anasema Haule.

Haule anasema amerithi elimu hiyo ya tiba mbadala kutoka kwa babu yake, Mzee Fungafunga.

Anasema alijifunza tiba kwa kutumia mimea, kutoka kwa babu yake, ambaye licha ya kuwa alikuwa mhunzi, alitibu kwa njia ya mimea.

Haule anasema aliamua kujikita zaidi katika tiba asilia baada kukosa ushirikiano katika fani aliyosomea ya ufundi makanika.

chanzo. Dawa za kuongeza akili zaingia nchini - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Hapa ni usanii mtupu ,kwa vile watz hatupo makini na serikali yetu ni sikivu jamaa watapiga bingo acha kabisa . Nakumbuka matangazo kama haya ya dawa za kuongeza akili ama za kufanya watoto wapende kusoma yalipigwa marufuku UK na hiyo kampuni ilipigwa faini kubwa mno mwishoni mwa miaka ya 1990 Kama sio mwanzoni mwa miaka ya 2000.
 
Bora zimekuja asee, manake tulikuwa tumefikia pabaya. Kama ilifikia mtu anaona makaburi ni bora zaidi ya uhai wa wagonjwa wanaokufa mahospitalini kwa kukosa dawa basi tulikuwa tumefika kusiko.

Mkuu MziziMkavu, mbona bwana Haule mwenyewe (ikiwa ndio huyo pichani) afya yake haina taswira njema machoni mwangu?
 
Last edited by a moderator:
Naomba zipelekwe bungeni ASAP. Otherwise utasikia bilioni moja imetengwa kwa mazishi ya viongozi watakaokufa mwakani
 
haloooooohizo dawa ningeomba waanze kupewa wabunge na viongozi wa sisiem!!!!!!!!!!!!!!!!! Haraka sana.
 
VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

attachment.php

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.

attachment.php

Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.

attachment.php

MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.

NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.

KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Thankx bro
 
Hili ni somo murua kabisa MZIZIMKAVU nashukuru sana hivyo vyakula vyote maeneo yetu vinapatikana kiurahisi tu. tutalifanyia kazi .
la dawa hizo linahitaji ufafanuzi kiasi uliothibitishwa kitaalamu.
 
Bora zimekuja asee, manake tulikuwa tumefikia pabaya. Kama ilifikia mtu anaona makaburi ni bora zaidi ya uhai wa wagonjwa wanaokufa mahospitalini kwa kukosa dawa basi tulikuwa tumefika kusiko.

Mkuu MziziMkavu, mbona bwana Haule mwenyewe (ikiwa ndio huyo pichani) afya yake haina taswira njema machoni mwangu?
Nilidhani nimeliona mimi tu maana hali ilivyo mtu unaweza pata mashaka kama taifa hili bado tunafikiria sawasawa.
 
Watu wanabubi kila siku jinsi ya kupata hela

Asante MziziMkavu kwa post yako nitajitahidi sana kuongeza pilipili kwenye chakula changu
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka huko zilikotoka watu wana akili sana hadi watanzania wakakumbukwa kuletewa..

Hata mie nimejisemea kuwa...hopefully huko itokako dawa, watu wanachemka kichwani si mchezo.....
 
Back
Top Bottom