Dawa zinatengezwa kwa ingredients zilizo kwenye leaflet au kuna vingine wanaweka ila hawavisemi?

kufanakupona

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2015
Posts
522
Reaction score
421
Habari wakuu.
Huwa nikisoma vikaratasi vya maelekezo ya dawa, nakutana na ingredients zilizotumika kutengeneza hiyo dawa.
Najiuliza, wanaotengeneza dawa wametengeneza hiyo dawa kwa kutumia ingredients hizohizo au kuna ingredients nyingine ila hawajazitaja kwa kuepuka msururu wa maelezo ya ingredients?.
Karibuni.
 
Labda kama dawa hizo ni za ujanja lkn kama imethibitishwa haiwezi kuingia sokoni kama leaflet haisemi ukweli
Dhumuni la hili swali, nilitaka kuthibitisha kama dawa zinatengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa ingredoents zilizo kwenye leaflet pekee, na hawaongezi kingine tofauti na ingredients zilizotajwa kwenye leaflet.
Baada ya hapo najitengenezea dawa mwenyewe kwa kuchanganya mchanganyiko wa ingredients zilizo kwenye leaflet.
Sijui kama umenielewa mpaka hapo?
 
Kwahiyo zile ingredients zilizopo kwenye kikaratasi cha maelekezo hazijitoshelezi?, yaani kuna ingredients nyingine bado zimemiss?
Mzungu (kwa kuwa dawa nyingi zinatengenezwa kwake) hawezi akakuweka wazi vitu vyote kwa hiyo jiongeze hapo
 
Mzungu (kwa kuwa dawa nyingi zinatengenezwa kwake) hawezi akakuweka wazi vitu vyote kwa hiyo jiongeze hapo
Siyo wa kuwaamini kumbe, kama ni hivyo, ukitaka kujitengenezea dawa kwa kuangalia ingredients as a complete reference, imekula kwako, kwasababu details zinakuwa bado hazijakamilika.
Duh!!
 
Siyo wa kuwaamini kumbe, kama ni hivyo, ukitaka kujitengenezea dawa kwa kuangalia ingredients as a complete reference, imekula kwako, kwasababu details zinakuwa bado hazijakamilika.
Duh!!
Unajitengenezeaje dawa kwa kufata maelezo ya ingredients pekee!..
Kuna ishu za joto na mazingira ya kuitengeneza sio umekaa chumbani ukaiga ingredient za panadol eti utatoa panadol utajiua!.
 
Kwenye leaflets huwa tunaandika active ingredient tu. Excipients Kama preservatives nk huwa hatuziandiki.

Mfano kidonge cha cetrizene tutakuandikia trimethoprim na sulfamethoxazole. Kuna ingredients nyingine zaidi ya Kumi tofauti na hizo active ingredient mbili.
 
Unajitengenezeaje dawa kwa kufata maelezo ya ingredients pekee!..
Kuna ishu za joto na mazingira ya kuitengeneza sio umekaa chumbani ukaiga ingredient za panadol eti utatoa panadol utajiua!.
Shukrani mkuu.
Dondoo kama hizi za kutengeneza dawa ndizo nilizokuwa nazihitaji. Kumbe kujitengenezea dawa kwa kuangalia ingredients kuna masharti!, ongezea masharti mengine mkuu.
Halafu, ni kweli ingredients za kwenye leaflet pekee ndizo zinazounda dawa?, au ingredients nyingine hawaweki?
 
Hizo ingredients zaidi ya kumi wanazoziacha ni active au inactive ingredients?, kama inactive ingredients yaani excipients au inert ingredients wakiziacha ni sawa tu, kwa sababu kwa maelezo yako umesema excipients (inactive/inert ingredients) huwa haziandikwi.
 
Hizo inactive ingredients huwa hazitibu Bali zinasaidia kuibeba ingredients inayotibu.

Mfano kidonge cha folic acid kina milligram 200. Folic acid yenyewe kwenye hicho kidonge ambayo Ndio active ingredient [dawa yenyewe] ni milligram 5 tu.

Milligram 195 zote ni active ingredient Kama starch, Kuna binders, sorbitol, preservatives Kama sodium propyl paraben. Zipo ingredients kwa ajili ya kusaidia kidonge kiyeyuke haraka ukikimeza, ingredient kwa ajili ya pH nakadhalika na kadhalika.

Inatakiwa ujuwe dawa yako ina active ingredient zipi hizo zingine sidhani Kama zinamsaada Sana kwa mgonjwa Ndio maana huwa hatuziweki.

Pia tunazificha ili kuficha formula zetu tunazotumia kutengeneza dawa.
 
Sio kwenye dawa tu, mi najua kweny vitu vingi hata vyakula huwa haw display ingredients zote zilizotumika Kutengeneza... Sababu ya kibiashara pia..
 
Na mimi nimelenga hapohapo kwenye active ingredients.
Kwa mfano unajua active ingredients za dawa fulani ni hizi, hizi na hizi, je, kuna uwezekano wa kujitengenezea dawa kwa matumizi binafsi?
 
Sio kwenye dawa tu, mi najua kweny vitu vingi hata vyakula huwa haw display ingredients zote zilizotumika Kutengeneza... Sababu ya kibiashara pia..
Kwenye ingredients za vyakula nako nataka nijue, nataka nijue SI unit za vyakula zinazotumika zina maana gani, kwa mfano utakuta vimsamiati vya cal, gram na %, sijui vinamaanisha nini.
 
Sidhani kama inawezekana..alafu pia unadhani dawa huwa na vitu vingi sana??,no.
 
Sidhani kama inawezekana..alafu pia unadhani dawa huwa na vitu vingi sana??,no.
Nilivyokuwa nagoogle active ingredients za dawa za magonjwa mbalimbali, nikawa najifariji kwamba ufumbuzi wa kujitengenezea dawa zisizo na madhara zitokanazo na material asili umeshapatikana, kumbe bado kabisa, ndiyo maana watu wanakwenda kusomea mambo ya kutengeneza dawa kwa miaka na miaka.
Dah!
 
Na mimi nimelenga hapohapo kwenye active ingredients.
Kwa mfano unajua active ingredients za dawa fulani ni hizi, hizi na hizi, je, kuna uwezekano wa kujitengenezea dawa kwa matumizi binafsi?
Kutengeneza dawa kunaitaji utaalamu wa hali ya juu..labda kama unasema za kienyeji..ila hizi dawa zinatengenezwa in such a way that,ukiimeza itasambaa kwenye damu au sehemu inayostahili,bila ya kiharibiwa na nature ya mwili(pH,acidity,temperature na vingine)
 
Mpaka kidonge kinaingia sokoni watu ni kweli wanakuwa wamefanya kazi..maana unaweza kutengeneza ovyo ovyo kumbe kidonge kikifika tumboni tu kinapoteza uwezo wake.
 
Ingredients (active ingredients) nazichukua za kwenye vidonge vya madukani, ila kutengeneza ndiyo natengeneza kienyeji.
Mpaka kidonge kinaingia sokoni watu ni kweli wanakuwa wamefanya kazi..maana unaweza kutengeneza ovyo ovyo kumbe kidonge kikifika tumboni tu kinapoteza uwezo wake.
Pia unaweza kutengeneza kumbe ukatengeneza ndivyo sivyo, matokeo yake unaweza kutengeneza sumu hivihivi.
Bado kuna safari ndefu sana kwa wenye kiu inayohusu dawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…