DAWASA bado wanasubiri wakabidhiwe Mradi wa Maji Kiluvya NSSF

DAWASA bado wanasubiri wakabidhiwe Mradi wa Maji Kiluvya NSSF

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Mradi wa Maji Kiluvya NSSF

Eneo la Kiluvya NSSF kwa sasa kuna mradi unaoendelea kutekelezwa na Shirika la hifadhi ya Mifuko ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya wateja ambao waliuziwa viwanja katika eneo hilo.

Mradi huo umehusisha ulazaji wa bomba kubwa la inch 8 kutoka kwenye bomba kubwa la inchi 30 kuelekea kwenye kituo cha kusukuma maji ( Booster Pump) ili kuyafikisha kwenye tank la ujazo wa lita 500,000.

Pia mradi umehusisha usambazaji wa bomba ( line extension) zenye ukubwa tofauti tofauti kuanzia inchi 6, 4, 3,2 zitakazoenda kwenye makazi wa wananchi lengo ni kuwezesha urahisi wa maunganisho pindi wateja watakapo hitaji huduma.

Kwa sasa mradi huu bado upo chini ya usimamizi wa NSSF na upo mbioni kukamilika. Baada ya kukamilika mradi wataalamu wa DAWASA kwa pamoja na NSSF wataukagua kwa lengo la kuhakikisha umekidhi viwango vya ubora ndipo utakabidhiwa DAWASA kwa uendeshaji.

Takriban wateja 1000 wanategemewa kunufaika na mradi huo.

Eng Ramadhani Mtindasi
Kaimu Mtendaji Mkuu
DAWASA
18.4.2024
 
Back
Top Bottom