KERO DAWASA kuna rushwa kwenye ufungaji wa maji

KERO DAWASA kuna rushwa kwenye ufungaji wa maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu hiyo barua kwanza hadi imfikie mhusika sio leo. Na ataisoma baada ya miezi. Tumeshafuatilia sana ofisi zao na tumekwama.Lengo la kuleta uzi humu ni kuwataka waache upuuzi na wawajibishwe sababu hata mawaziri wanasoma humu.
Unaipeleka mwenyewe mguu kwa mguu... ofisi zao si zinajulikana zilipo...ukifika unamuulizia meneja wa Tawi...!​
 
Niliomba huduma ya maji safi, wakaja saveya, wakasema nyumba yako iko nje ya mita 50.
Andika barua kwenda kwa meneja, kwamba uko tayari kulipa gharama za mita zilizoongezeka. Nika andika huo mwezi wa August 2023.
Safari za nenda rudi zikaanze, mara hakuna mita, mara vile.

January 2024, jirani yangu ambaye yuko mbali zaidi yangu aliletewa maji ndani ya masaa 2.
Jirani wewe umefanya nini? akaniambia nimetoa rushwa ya laki tisa.

Nipe namba za wadau,
Kwangu waliomba 1.2milioni. Nikalipa laki tisa, na nikatumiwa control number saa moja jioni! siku iliyofuta nikaletewa maji safi.

Tunatumia ofisi ya dawasa salasala.

Kuna wadau hawa:

saveya mmasai
saveya mchaga (kaoa mwaka jana mwishoni)

Kuna wawekezaji wagiriki, wamewapiga pesa za kutosha.

Acha niishie hapa!
Umekuja kutuchoma sio? Tutadili na wewe
 
Watu msiogope wala msiwe na makasirikio kutoa rushwa. Mimi nikienda hospital, Tanesco, Dawasa, Polisi, na hata trafiki akinipiga tochi natoa rushwa na maisha yananiendea swaaafii.

Nyie mnaojitia wagumu kutoa rushwa, mtàlalamika mpaka Yesu atakaporudi.

Hii ni Tanzania bwana. Kama Magu aka jiwe kweri kweri aliruhusu tutoe rushwa, wewe ni nani ukatae?
 
KWA WEWE MWENYE UWEZO RUSHWA NI KITU KIZURI NA NI SHORT CUT,
KUNA WENZETU HAWANA UWEZO.
USISAHAU RUSHWA SIO PESA TU, KUNA WENGINE WANAOMBA MAPENZI.
JE UKO TAYARI KUONA MAMA,DADA, BINTI YAKO AKIFANYWA KWA AJILI YA KUPATA HUDUMA FLAN?

Mhadhiri wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Haliye Haliye amefikishwa mahakamani ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kuomba rushwa kwa wanafunzi ili kuwasaidia wafaulu mitihani wa marudio.

Muuguzi matatani kwa kumuomba rushwa Mjamzito, adaiwa kumsababishia maumivu makali​

Watu msiogope wala msiwe na makasirikio kutoa rushwa. Mimi nikienda hospital, Tanesco, Dawasa, Polisi, na hata trafiki akinipiga tochi natoa rushwa na maisha yananiendea swaaafii.

Nyie mnaojitia wagumu kutoa rushwa, mtàlalamika mpaka Yesu atakaporudi.

Hii ni Tanzania bwana. Kama Magu aka jiwe kweri kweri aliruhusu tutoe rushwa, wewe ni nani ukatae?
Wangetuambia toka mwaka jana kuwa tutoe rushwa watufungie maji, sio kutuzungusha miezi mitano wameishiwa vifaa. Si wafunge ofisi basi
 
Back
Top Bottom